Katiba mpya ni bomu linalosubiri kulipuka

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
Ukifuatilia mijadala bungeni tangu kuanza kwa mchakato wa katiba mpya na huu mjadala unaoendelea sasa kuhusu muswada wa sheria ya kura ya maoni utagundua kuna mgawanyiko mkubwa kwa misingi ya itikadi za kisiasa.Ni jambo la kusikitisha kuwa mijadala ya wabunge juu ya jambo hili iko kisiasa zaidi badala ya kuwa ya kitaifa.

Ninachokiona hapa ni kuwa mgawanyiko huo hautaushia bungeni tu bali utahamia uraiani mara campain zitakapoaanza juu ya upigaji kura ya maoni kuhusu katiba mpya.Campain hizi zitakuwa ni zaidi ya zile za uchaguzi mkuu kwani kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya vyama vya siasa kuunganisha nguvu na hapa ndipo patakapokuwa msingi wa msuguano mkubwa na hatimae machafuko makubwa.

Wanasiasa ndani na nje ya bunge tambueni kuwa mkishindwa kuelewana juu ya jambo hili basi mjue kuwa "katiba mpya ni bomu linalosubiri kulipuka".Tena yawapasa kutambua kuwa hili ni bomu hatari kuliko hata lile la vijana kukosa ajira.
 
Mkuu Salary Slip,
You have a point. Naona mgawanyiko mkubwa kwa mlengo wa kisiasa kati ya ccm na vyama upinzani kwa upande mmoja, na Tanzania bara (soma Tanganyika) na Zanzibar (soma Unguja na Pemba) kwa upande mwingine. Wabunge katika kikao kinachoendelea sasa wana nafasi kubwa sana ya kuhahakikisha kuwa tunavuka salama katika hili.

Lakini, kwa hali ilivyo katika serikali yetu na mawaziri wake 'wanaopenda' majibu mepesi kwa maswali magumu, mbwembwe na kejeli nyingi kwa wapinzani wao, ushabiki wa wabunge wa ccm kwa serikali hata pale ambapo iliyo mezani ina maslahi mapana ya taifa bila kujali itikadi za vyama, nakubaliana na wewe kwa 100% kuwa muda sio mrefu harakati hizi zitahamia uraiani ambako madhara yake yanaweza kuwa makubwa zaidi.

Chonde chonde madam spika na timu yako, hii ndio nafasi pekee ya kulitendea haki taifa hili kwa kutokuchezea muswada wa sheria ya kura ya maoni ulio mbele ya bunge lenu tukufu sasa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom