Katiba mpya na ndoto ya mwendawazimu

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,398
1,006
Kwa hali ilivyo sasa ni ndoto ya mwendawazimu kupata katiba mpya achilia mbali iliyo bora,tatizo ni pale wajumbe walio wengi walipokataa mapendekezo ya tume( wana haki).kwa maini Yang rasimu imejengwa juu ya msingi wa serikali 3.ukitaka tofauti na hivyo inabidi uachane na rasimu an za mchakato mpya kabisa kwani msingi wa serikali 3 umeathiri ibara takriban 87.lakini pia haina sura za mambo yasiyo ya muungano,hebu niambieni wajuzi mnawezaje kufumua ibara 87 halafu isitoshe muongeze sura za washirika,halafu mjadiliane mpaka muafikiane hata tukiwapa mwaka hawawezi kutuletea katiba yoyote(sizungumzii kabisa ubora),lakini ni kawaida watanzania Kuota na tuendelee Kuota,NDOTO YA MWENDAWAZIMU
 
wameshaanza kusalimu amri ndo maana mawaziri wengi hawapo dodoma. pia wajumbe wengi waenda kusaini na kuondoka maana wajadili nini wakati ibara zote msingi wake ni serikali 3. ccm ni wapumbavu sana na wanazidi kujidhalilisha kwa wananchi

QUOTE=ngozimbili;10341808]Kwa hali ilivyo sasa ni ndoto ya mwendawazimu kupata katiba mpya achilia mbali iliyo bora,tatizo ni pale wajumbe walio wengi walipokataa mapendekezo ya tume( wana haki).kwa maini Yang rasimu imejengwa juu ya msingi wa serikali 3.ukitaka tofauti na hivyo inabidi uachane na rasimu an za mchakato mpya kabisa kwani msingi wa serikali 3 umeathiri ibara takriban 87.lakini pia haina sura za mambo yasiyo ya muungano,hebu niambieni wajuzi mnawezaje kufumua ibara 87 halafu isitoshe muongeze sura za washirika,halafu mjadiliane mpaka muafikiane hata tukiwapa mwaka hawawezi kutuletea katiba yoyote(sizungumzii kabisa ubora),lakini ni kawaida watanzania Kuota na tuendelee Kuota,NDOTO YA MWENDAWAZIMU[/QUOTE]
 
Je, itakapofika kuchangia sura za nchi mshirika (Tanganyika) ambazo zitaongezwa kwenye rasimu ya katiba, kama vile Ardhi, Maliasili, Serikali za mitaa etc. Nini itakuwa status wa wajumbe kutoka Zanzibar ambao sura hizo haziwahusu kabisa. Je wajumbe, kutoka ZNZ watachangia na kuzitolea maamuzi hizo sura ambazo haziwahusu kabisa?! Au watatoka nje ya BMK kuruhusu wajumbe kutoka Tanganyika kuzijadili na kuzifanyia maamuzi?! Aidha kama sura hizo zinazohusu Tanganyika zitaingizwa kwenye rasimu nini itakuwa hatima katika upigaji wa kura ya maamuzi (kura ya NDIYO na HAPANA)? Je Wazanzibari watahusika katika kuikubali au kuikataa rasimu ya katiba ambayo ina sura zinazohusu Tanganyika tu!? Je, Watanganyika tutakubari kufanyiwa maamuzi ya mambo yetu na Wazanzibari?! CCM kwa kukataa muundo wa S3 wamelikoroga na kwasababu ya UPUMBAVU WAO WANAENDELEA KUSHUPAA.
 
Back
Top Bottom