Katiba Mpya Haimpeleki Rais Ikulu

Unataka Tanzania iendelee na mfumo wa Rais kumchagua jaji mkuu na jaji mkuu anakwenda. kumuapisha Rais aliyemteua?
 
Is there any reason behind which makes you to use English instead of Swahili, since your main post was in Swahili. Or you think by using English I will consider you as an intellectual?
Dear Expert Member, get to comprehend the concept.
 
UONGO MTUPU, Electoral Votes zinapatikana kupitia Popular Votes. Kila jimbo Marekani lina idadi zake na sheria zake katika utoaji wa electoral votea. Mfano, California yenye Electoral Votes 55 mgombea yoyote wa Urais anaposhinda California hata kwa kura 1 anapewa electoral votes zote 55, ni kinyume cha katiba mjumbe wa electoral college kumpigia kura ya electoral vote mtu ambaye hajashinda Popular votes kwenye hilo jimbo.
Wajumbe wa Electoral College bila kujali vyama vyao ni lazima wapige kura kulingana na mshindi wa Popular votes katika majimbo yao.
 
Wanataka Katiba mpya ili kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi miongoni mwa mambo mengine, wanataka Tume Huru ya Uchaguzi ili washinde uchaguzi kwasababu LENGO LA MSINGI LA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA DUNIANI NI KUSHIKA MADARAKA YA NCHI (Kuingia Ikulu).
Na chama cha siasa ili kiweze kutekeleza sera zake lazima kiwe na madaraka.

Kwani ni kosa chama cha siasa kutaka madaraka ?
 
Is there any reason behind which makes you to use English instead of Swahili, since your main post was in Swahili. Or you think by using English I will consider you as an intellectual?
JF is bilingual.
 
Hoka ya latina mpya ni kupata haki kwa wananch na kuwadhibiti watawala wasiwe wakoloni, hoja ya Ikulu ni matokeo
 
Na chama cha siasa ili kiweze kutekeleza sera zake lazima kiwe na madaraka.

Kwani ni kosa chama cha siasa kutaka madaraka ?
Siyo kosa kabisa mkuu.

Charles Njonjo alipotaka kumng'oa mzee Jomo Kenyatta akaenda kum-consult babake kwanza. Babake akamwambia ebu fungua jokofu hilo hapo, chukuwa kipande cha nyama mpe paka, Charles akafanya hivyo, paka alivyoanza kukila mzee Njonjo akamwambia Charles ebu sasa mnyang'anye paka hicho kipande cha nyama kabla hajakimaliza, Charles akasema haiwezekani, mzee Njonjo akamuuliza kwanini haiwezekani, Charles akajibu paka atanidhuru. Mzee Njonjo akamwambia Charles sawasawa kabisa kumbe umeelewa somo, sasa ukitaka kumnyang'anya mzee Jomo Kenyatta urais jiandae kudhuriwa. Mimi simo! Charles akapanda ndege kurudi London akaghairi mpango huo. Nimefafanua kifasihi zaidi.
 
Kwahiyo hamtaki katiba mpya ili kulinda madaraka ?

Kama nilielewa vizuri thesis yako ilikuwa ni kwamba katiba haiwezi kukupeleka ikulu kwa maana ya kukupa madaraka.

Sasa kama thesis yako ni hiyo mbona jibu lako hili ni contradictory ?
 
Sasa kama hivyo ndivyo, hii hoja kuwa Chadema wanataka katiba mpya ili waingie ikulu inatoka wapi?
Nyuma ya madai ya CHADEMA ya Katiba mpya (mwendelezo wa madai ya viongozi wa vyama vya upinzani) ni dhana yao potofu kuwa vyama vya upinzani vinashindwa kuongoza Dola, kwa maana ya mgombea wao kutokuchaguliwa Rais kwa sababu ya Tume ya Uchaguzi siyo huru. Lakini hawajawahi kutathmini ni kwa nini wagombea wao wa Urais hawapati kura za kutosha.

Kwa kuwa njia ya kuelekea kuongoza Dola inaonekana ni ndefu, kwa Vyama vya Upinzani, viongozi wake wana dhana nyingine (potofu) ya kutaka wigo wa nafasi za kuongoza nchi hii upanuliwe, kwa kudai Muungano wa Serikali Tatu (3). Ikiwa hivyo, wanaamini wengi wao (viongozi wa upinzani) watapata nafasi za madaraka serikalini.
 
Kama hiyo katiba mpya haitamtoa rais wako madarakani, hofu ya nini kwenye kupatikana hiyo katiba mpya?
Naona aibu mie mkuu. Yaani mtu mzima anaandiaka upuuzi kama huu kweli
 
Ulisoma wapi mkuu.
Una elimu gani?
 
Sikwenda shule ila nina elimu ya ufahamu na kujitambua
Ni kweli hujakwenda shule. Na kama umeenda basi ni shule za kata na kusoma vyuo kama CBE, MWALIMU NYERERE na vingine vya mfano huo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…