CHADEMA wamejipambanua wazi wazi ya kuwa nini wanataka. Agenda yao ya uhuru, usawa na haki haipendezi sana miongoni mwa madhulumati na wanufaika wa hali iliyopo sasa.
Rais Samia kajipambanua kuwa hataki dhuluma bali anataka usawa na haki kwa wote. Mama ameonyesha utayari wa kuonana na makundi mbalimbali, vyama vya siasa nk. Mama hayuko mbali sana kimsimamo na Chadema.
Ni wazi kuwa wahafidhina na wanufaika wa bakshish za hali iliyopo hawajafurahishwa na misimamo yake mingi ikiwamo hii.
Wahafidhina hawa wanaomzunguka kwa kila upande, ndiyo lililo tatizo kuu. Wao wamejipanga vilivyo "piga ua" kumfanya mama kubadili mingi ya misimamo yake.
Wamechagua hata kumfarakanisha Mama kwa vyovyote, na kwa yeyote, na kwa lolote (hata kama ni la kijinga). Wanajaribu hata kumwunganisha na JK ili kumfitinisha Mama.
Mzee Warioba yalimkuta hata akamwekwa vibao hadharani walipohisi kuhatarishwa kwa maslahi yao:
View attachment 1839617
Chokochoko za kuhusu mradi wa Bagamoyo, safari za Mama nje ya nchi, misimamo mipya dhidi ya Corona vikiwamo ugonjwa na chanjo, nk yote ni katika kufanikisha mifarakano hiyo.
Dhidi ya CHADEMA wamejipanga vilivyo kuhakikisha kuwa, Mama hakutani nao kwa namna yoyote ile. Ni nia yao kuona mkutano wowote baina ya CHADEMA na Mama hautakaa ufanyike.
View attachment 1839607
Ni wazi kuwa kwa kukutana tu, Mama angeweza kupata picha tofauti kabisa na matango pori anayolishwa kwa makusudi kuhusu Chadema na kila uchao.
Nchi hii ni yetu sote. Tatizo si Mama. bali hila za wahafidhina. Suluhu ya hapa tulipo ni kwa mama kuchanganya na za kwake kwenye akili anazoambiwa. Hata hivyo Mama kesha jipambanua:
View attachment 1839602
Mama si sehemu ya ufedhuli huo.
Kwenye mazingira haya uchaguzi (option) pekee wa haki na unaobakia ni kwa Chadema kuendelea kudai mustakabala mpya wa katiba na kwa nguvu zaidi.
Katiba ni yetu sisi wananchi. Hatutaki kuendelea kubambikiziwa kesi, hatutaki dhuluma, hatutaki kubebeshwa mizigo ya kodi ya wengine, tunataka mihimili ya utawala iliyo na huru kamili, tunataka usawa, tunataka uwajibikaji, tunataka mawazo yetu kusikilizwa nk. Haya si ya kupuuzwa tena. Hayawezi kuendelea kusubirishwa tena na bila ukomo.
Amandla!
Ninawasilisha.
Cc:
BAK Missile of the Nation JokaKuu Pascal Mayalla johnthebaptist