Katiba Mpya: CHADEMA, CUF na NCCR- Mageuzi wakutana na wanahabari Sept 15, 2013

Nawapongeza viongozi wote wa upinzani kwa kuweka tofauti zao pembeni kwa maslahi mapana ya nchi hii, Mwenyezi Mungu awatangulie na kuwaongoza katika juhudi hizi za kupata katiba bora itakayokuwa msingi wa kuikomboa Tanzania na wana wake.
 
Mungu saidia huu muunganiko ili CCM itoke madarakani!...what a favor from God. Imagine hivi vyama vinge achiana majimbo, pale ambapo candidate mmoja wao ni strong then apate support ya vyama vyote. Adui mkuu ni CCM sote tuungane kumwangamiza
 
Hakika hii imenifurahisha, kuona vyama vyetu vya siasa vinavyoweza kuungana kuoka nchi na ...., na baadaye tunasubiri CCM wakubaliane nao halafu utaona la kuona, mara itageuka kuwa kinyume.

Miaka kadhaa nyuma Vyama vya Siasa (katika Upinzani) maana si kweli ni vyama vya upinzani, viliweka nadhiri havitashiriki uchaguzi ujao mpaka KATIBA MPYA, hakuna kulala mpaka KIELEWEKE ilisikika saana. Naomba basi mambo muhimu haya waliyoyaibua yalete maana hata kama na CCM wakisema wanakubali. Ila CCM, CHADEMA, CUF, NCCR say whatever, wao ni nani? kwani wao ndio wananchi? sikweli, wananchi angalieni linalowafaa siyo wanalosema wenye uwezo wa kusema na kushawishi watu nasi tukatumia PEOPLE'S POWER kumbe ni chama's power.

Lile tangazo la Sidanganyiki siku hizi halipo, ila hapa ndio mahali pake. Tuseme wote kwa dhati. Japo sikubaliani na baadhi ya misimamo ya CCM kwenye mchakato wa Katiba mpya, na wala pia sikubaliani na baadhi ya misimamo ya CHADEMA, mimi mkombozi wangu ni mwanachimwenyewe.

Vyama tafuta PLATFORM zungumza sisi tutachambua na kumbuka tuna uwezo wa kujua jema na baya. ALAMSIKI
 
Kwa hili mmenifurahisa.........jmos wa kwanza kuwa jangwani nikawashuhudie makamanda wapya. All the best.
 
Mungu saidia huu muunganiko ili CCM itoke madarakani!...what a favor from God. Imagine hivi vyama vinge achiana majimbo, pale ambapo candidate mmoja wao ni strong then apate support ya vyama vyote. Adui mkuu ni CCM sote tuungane kumwangamiza

Hilo halitokei ndugu yangu sahau kabisaaaaa, maana huu sio muungano wa vyama, ni sehemu wamekaa pamoja kutetea lililo moyoni. Maana viongozi wetu wa-binafsi sana kufanya hivyo. Maana hata CDM wamegoma kuhusisha wengine, wanahusishwa kwenye kulumbana. Huu sio umoja wa vyama ni kukaa pamoja kutoa tamko. Kesho keshokutwa tutasikia mengine, japo ningefurahi kama wangeungana maana wangekuwa na nguvu, ila ndugu hiyo sahau. Kuna waimbaji waliimba wimbo wakasema MKATE unaleta mambo, maana akitokea mwenye mkate akamwambia mmoja unauona huu, achana na hayo hatasita kutetea nafsi yake kutopenda kushirikiana. Alamsiki
 
Leo tena wamekutana Hawa viongozi Wakuu wa vyama hivi vitatu na Tayari wameshaanza kazi na mojakwamoja wameanza kwa kutembelea ofisi za jukwaa la katiba! Nimependa sana hii kitu. Cuf, Cdm na Nccr katika hili swala angalieni mamluki wasiingie!
 
attachment.php

attachment.php

Hii ilikuwa leo katika hotel ya Courtyard Dsm , wameamua kuweka wazi juu ya katiba na mwelekeo wa pamoja.

Wenyeviti wa vyama vya Siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi leo wamekukutana na wahariri na waandishi wa habari kueleza mikakati na mbinu watakazozitumia kunusuru taifa lisiingie kwenye utungaji wa Katiba mpya itakayobeba masilahi ya chama tawala.

Taarifa zaidi za kilichoongelewa zitafuatia

Kwa wale ambao bado wanajiuliza UKAWA ilianzaje anzaje, pengine bandiko hili linaweza kutoa nuru ya maswali ya UKAWA ni nini na wanataka-aje?
 
Back
Top Bottom