Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,489
- 40,999
Katiba pendekezwa ya Warioba, ilisema kuwa mawaziri wasiwe wabunge ili Rais awe na uwanja mpana wa kuwapata wasaidizi kwenye nafasi za uwaziri.
Siku za nyuma, wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, kabla ya mabadiliko ya katiba, mawaziri hawakuwa wabunge.
Leo katiba yetu hii mbovu inamlazimisha Rais kuteua mawaziri kutoka kwenye kundi la wabunge ambao wengi wao uwezo wao ni duni, lakini wanaupata ubunge kwa sababu wana pesa za kuhonga wapiga kura, hata kama pesa zenyewe, kwa baadhi yao, ndiyo hizo walizoziiba au wakati mwingine kukwepa kodi, ingawa wapo wanaotumia pesa zao safi walizozichuma kwa jasho lao, halafu wanaenda kuzitumia kuwahonga wapiga kura.
Mtu aliyeupata ubunge kwa kuhonga wapiga kura, au kuwahonga wasimamizi ili mpinzani wake aondolewe na yeye apite bila kupingwa, akiteuliwa kuwa Waziri, ataweza kuwa ni waziri mwenye maadili?
Serikalini wamejaa viongozi ambao mapito yao yamejaa uchafu tele, halafu tunategemea tupate manukato ya kuvutia.
Waziri Mkuu, mbunge ambaye hakupata hata kura moja.
Waziri wa Fedha, Nishati, Habari, n.k; wote wabunge wa kupachikwa.
Watu wasio na maadili tunataka wasimamie maadili. Haya maajabu yapo Tanzania pekee.