Katiba iwe ya Wananchi sio ya viongozi!

Nape Nnauye

MP Mtama
Dec 26, 2012
99
408
Toka rasimu ya Katiba mpya itolewe viongozi wengi wa kisiasa na kijamii wamekuwa wakitoa maoni yao hadharani juu ya rasimu hiyo, madhara ya hili ni kujaribu ku influence mawazo ya wananchi ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuwa wenye Katiba mpya.

Kwanini viongozi wetu hawa wakijamii na kisiasa tusiwape room wananchi watoe maoni yao kwanza ndipo nasi tupate muda wa kujenga juu ya maoni yao?

TUIFANYE KATIBA YA WANANCHI SIO YA VIONGOZI
 
Narrow mind ..... nini manna ya uongozi ..... representation .... on behalf ... trusted to lead others ....

mbona wananchi wengi tuu wanajadili na kutoa maoni ya rasimu ya katiba huku mtaani, just because they don't have airtime in the media

I am waiting for your lousy views as usual
 
Kumbe unajua mawazo ya viongozi wa Kisiasa yanasikilizwa sana na wananchi sasa wewe na Lameck Madelu kama viongozi wa Chama mnajisikiaje pale mnapotema "pumba" hadharani

Wewe jamaa siasa za dijitali zimeshakushinda sasa ulitaka wasitoe mawazo yao kisa kuna watu watawasikiliza?si ndio vizuri labda na wao watatupa mwanga!
 
Toka rasimu ya Katiba mpya itolewe viongozi wengi wa kisiasa na kijamii wamekuwa wakitoa maoni yao hadharani juu ya rasimu hiyo, madhara ya hili ni kujaribu ku influence mawazo ya wananchi ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuwa wenye Katiba mpya. Kwanini viongozi wetu hawa wakijamii na kisiasa tusiwape room wananchi watoe maoni yao kwanza ndipo nasi tupate muda wa kujenga juu ya maoni yao?

TUIFANYE KATIBA YA WANANCHI SIO YA VIONGOZI

Natamani uliyosema uyasimamie, maana umeandika jambo la maana sana, naamini imetoka akilini mwako si kwa nia ya kuongeza haiba yako uwapo majukwaani wala kukinusuru chama chako.
 
Viongozi wa CCM mmeshatoa msimamo wa kuipinga rasimu hiyo kupitia kwa Kinana. Sasa ni vema kama hoja yako pia ungewataarifu viongozi wako hasa Katibu Mkuu wako kuwa alichokifanya sicho kwa mtazamo wako huu.
Anyway, nawe ukiwa kama mwananchi hebu funguka kuhusu maoni yako binafsi kuhusu rasimu hii. Uzuri wake ni upi na ubaya wake ambao ni subject to discussion ni upi?
 
Toka rasimu ya Katiba mpya itolewe viongozi wengi wa kisiasa na kijamii wamekuwa wakitoa maoni yao hadharani juu ya rasimu hiyo, madhara ya hili ni kujaribu ku influence mawazo ya wananchi ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuwa wenye Katiba mpya. Kwanini viongozi wetu hawa wakijamii na kisiasa tusiwape room wananchi watoe maoni yao kwanza ndipo nasi tupate muda wa kujenga juu ya maoni yao?

TUIFANYE KATIBA YA WANANCHI SIO YA VIONGOZI

Nape watu wanakubali uelewa wako wa mambo ya kijamii tatizo ni chama unachokiongoza.Toka kwa shetani rudi kwa umma.Pokea M4C utakombolewa
 
Ndugu Nape viongozi pia ni wananchi! Hili neno wananchi limeanza kutumika vibaya sana katika nchi yetu. Sote ni watanzania tuache kubaguana kwa njia yeyote ile.
 
Dr Kitila ni sawa viongozi nao ni wananchi lakini kumbuka mwamba ngozi huvutia kwake. Ukiwa Kiongozi unajua na kesho utakuwa Kiongozi au mwanao, ndugu yako naye atakuwa kiongozi siku moja hivyo Katiba inapoonekana inakuwa na uongozi mpana ni lazima wananchi wa kipato haswa kile cha chini wahoji ni kwa nini..nchi itakuwaje na maraisi watatu, how. Kiukweli kabisa viongozi wengi wa nchi yetu haswa wa vyama vya siasa nikizungumzia pia kada pana la upinzani kweli kama siyo ubinafsi na uchu wa madaraka wasingekubali kuwagawanya watanzania kwenye vyama zaidi ya kumi na tano na kukosa haki ya watanzania badala ya kuwa na vyama vichache vya upinzani vyenye nguvu na kuweza kutuletea maendeleo ya haraka kwani kila chama kingejitahidi kuonyesah uwezo wa kusimamia katika haki .. Hapa tunaona wazi kuwa viongozi wetu ki ukweli hawawaangalii wananchi wote kwa ujumla na wananchi wanabaki wanalalamika tu basi.
 
Hii ni rasimu ya katiba ya Tanzania.
Kamwe hii sio rasimu ya katiba ya CCM.
Mwelekeo ni kuwa inaumiza chama tawala.
Ni bora waseme itawaumiza kivipi?
NOTE: Tunatengeneza katiba kwa ajili ya wananchi wa jamhuri bila kujali itikadi.
We are waiting how this game will end-up!
Mungu ibariki Tanzania.
 
Toka rasimu ya Katiba mpya itolewe viongozi wengi wa kisiasa na kijamii wamekuwa wakitoa maoni yao hadharani juu ya rasimu hiyo, madhara ya hili ni kujaribu ku influence mawazo ya wananchi ambao kimsingi ndio wanaopaswa kuwa wenye Katiba mpya. Kwanini viongozi wetu hawa wakijamii na kisiasa tusiwape room wananchi watoe maoni yao kwanza ndipo nasi tupate muda wa kujenga juu ya maoni yao?

TUIFANYE KATIBA YA WANANCHI SIO YA VIONGOZI

Habari za asubuhi? Kumekuchaje leo
 
Hii ni rasimu ya katiba ya Tanzania.
Kamwe hii sio rasimu ya katiba ya CCM.
Mwelekeo ni kuwa inaumiza chama tawala.
Ni bora waseme itawaumiza kivipi?
NOTE: Tunatengeneza katiba kwa ajili ya wananchi wa jamhuri bila kujali itikadi.
We are waiting how this game will end-up!
Mungu ibariki Tanzania.
Katika hali ambayo itaanika rangi za wasomi wetu, tumebahatika sisi wadanganyika kumpata msomi mwengine wa aina ya Dr. Mwakyembe ambaye amejotoa ufahamu kwa tamaa ya vyeo kwa kusema Katiba si kipaumbele cha awamu ya 5. Leo yupo Prof. Paramagamba Kaputi(Kabudi) ambaye ni msomi aliyeandika sana kuhusu Muungano wa Tanzania na Mambo ya Katiba, pia alikuwa kwenye tume ya Warioba kama Polepole amekabidhiwa wizara, Je atahakikisha Tanzania inapata Katiba ya kuibeba CCM au Katiba ya wananchi?
Wakati utaongea lakini tukiangalia historia ya waliyoyafanya na wanayoyafanya wasomi wetu, naamini wengi tumeshajua nini kinakuja.

Mchawi amepewa mtoto ........ Pole sana Prof. Kabuni kwa hapana kazi tu na kwa kuteuliwa kwako ili uje uonyeshe rangi yako rasmi.
 
Ndugu Nape viongozi pia ni wananchi! Hili neno wananchi limeanza kutumika vibaya sana katika nchi yetu. Sote ni watanzania tuache kubaguana kwa njia yeyote ile.
Leo mñajibizana namna hiyo? Naamini Tanzania ndiyo nchi itakayokuwa inaongoza kwa unafiki duniani. Rais Magufuli amewakusanya waliokuwa wanarefusha midomo juu ya Katiba kuanzia Polepole, Kabudi na Kitila Mkumbo. Sasa mko ubavuni kwake, mnaanza kumchokonoa, hamjui hajaribiwi? Nape leo anatafuta huruma ya Watanzania kwa kudhani jamii kama vile haimjui. Ccm walishafunga mjadala kama chama, na Nape anajua hilo. Sasa hii hadaa analeta ya nini?
 
najiraumu maishani mwangu kupoteza dakika zangu kusoma uzi huu, kwann hukuyasema haya before pindi ukiwa katika position nzur chamani, ww subilia kuvuliwa uanachama tu
 
Back
Top Bottom