Mwakaboko King
JF-Expert Member
- Apr 22, 2015
- 1,099
- 207
Kuna baadhi ya watu fulani wamekuwa na hasira kuhusu mamlaka ya Rais yaliyoanishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Sura ya nane,Kuanzia Ibara ya 80 mpaka 98. Watu hao wamefikia hatua ya kutaka apunguziwe mamlaka huku wengine hasira zao zikipitiliza wakitaka hata yale aliyonayo yaondolewe yote kabisa abaki kama mtumishi wa kawaida!
Jambo la kunishangaza ni pale watu hao wanaposhindwa kuelewa kuwa mamlaka au heshima ya mfalme ni wingi wa watu wake!wanashindwa kuelewa kuwa Mamlaka ya Rais ni wingi wa kura zake,hawezi kulinganishwa na mtu yeyote katika nchi.
Tanzania tunao utaratibu wa kumpata Rais kupitia sanduku la kura (nguvu ya umma) ambazo humpa Mamlaka ya kuongoza na kutawala.Rais ni Mkuu wa Nchi,kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa Tanzania Rais ni alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake na pia ni alama ya umoja ,uhuru wa nchi na mamlaka yake!
Sasa inawezekanaje Kiongozi Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama vya nchi ukataka alinganishwe na mjumbe au mbunge au waziri? Hilo haliwezekani fuatilia nchi zote ambazo wamekubali upuuzi huu utaona marais wao ni kama mapambo tu na wana jina lao eti wanabaki kuwa Ceremonial hawana mamlaka ya maamuZi ya nchi wapo wapo tu, hili halikubaliki Tanzania Rais ni MAMLAKA hata UKAWA wanalijua hili ndo maana wanaungana wakiamini kuwa watashinda nafasi ya Rais mwenye ambaye atakuwa na mamlaka!
Mungu Ibariki Tanzania!
Nawasilisha!
Dogo acha kukurupuka, umeelewa mada hapo juu ama unadandia tu gari kwa mbele?Jifunzeni acheni mambo ya kurukia! Huyo Rais wenu wa Serikali 3 ataondolewa with one year
Kuna baadhi ya watu fulani wamekuwa na hasira kuhusu mamlaka ya Rais yaliyoanishwa kwenye Katiba Inayopendekezwa ile Sura ya nane,Kuanzia Ibara ya 80 mpaka 98. Watu hao wamefikia hatua ya kutaka apunguziwe mamlaka huku wengine hasira zao zikipitiliza wakitaka hata yale aliyonayo yaondolewe yote kabisa abaki kama mtumishi wa kawaida!
Jambo la kunishangaza ni pale watu hao wanaposhindwa kuelewa kuwa mamlaka au heshima ya mfalme ni wingi wa watu wake!wanashindwa kuelewa kuwa Mamlaka ya Rais ni wingi wa kura zake,hawezi kulinganishwa na mtu yeyote katika nchi.
Tanzania tunao utaratibu wa kumpata Rais kupitia sanduku la kura (nguvu ya umma) ambazo humpa Mamlaka ya kuongoza na kutawala.Rais ni Mkuu wa Nchi,kiongozi wa Serikali na Amiri Jeshi Mkuu.
Kwa Tanzania Rais ni alama na taswira ya Jamhuri ya Muungano na watu wake na pia ni alama ya umoja ,uhuru wa nchi na mamlaka yake!
Sasa inawezekanaje Kiongozi Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama vya nchi ukataka alinganishwe na mjumbe au mbunge au waziri? Hilo haliwezekani fuatilia nchi zote ambazo wamekubali upuuzi huu utaona marais wao ni kama mapambo tu na wana jina lao eti wanabaki kuwa Ceremonial hawana mamlaka ya maamuZi ya nchi wapo wapo tu, hili halikubaliki Tanzania Rais ni MAMLAKA hata UKAWA wanalijua hili ndo maana wanaungana wakiamini kuwa watashinda nafasi ya Rais mwenye ambaye atakuwa na mamlaka!
Mungu Ibariki Tanzania!
Nawasilisha!
Ego naona hujamuelewa mtoa hoja,wewe umeganda kwenye issue ya ufalme,huo ni mfano tu ila hakuna tofauti ya Rais wetu,kwaniupatikanaji wake unajulikana ni kupitia nguvu ya umma,ballot power sasa usichokijua ni nini,akipigiwa kura na watu milioni 7 kati ya milioni 10 hii si inaonyesha kukubalika kwake?Je hii si ndo nguvu yake na mamlaka yake pia ya kiutawala?katiba lazima impe mamlaka makubwa yeye ndo tunamkabidhi nchi na majeshi yote sasa atakuaje na mamlaka madogo,just kuelewa tu hata baba katika familia ana mamlaka makibwa sembuse Rais?
mimi nadhani hujanielewa nilichokisema.
haijalishi raisi anachaguliwa na watu wangapi bali hoja hapa ni tunawezaje kudhibiti viongozi wasipore madaraka ya wananchi.
ni sawa na watu watatu kuwa na duka mkaamua kumchagua mtu wa kuendesha duka lenu. huyu mnatakiwa muwe na nguvu ya kumthibiti ninyi wenye duka ili asiwapore madaraka yenu ya kufanya anavyotaka.
mnaweza kumpa mtu madaraka kuendesha duka lenu mpaka mkashindwa kufuatilia mwenendo wa duka lenu akaligeuza kuwa lake na kwa katiba yenu akaonekana yuko sahihi kwani yote anayoyafanya ni kwa mujibu wa katiba yenu ya ushirikiano inavyosema.
ni katika dhana hiyo ya kuhakikisha viongozi wanaochaguliwa hawafanyi mambo wanavyotaka hata mkimchagua mtu kuwa raisi akaifanya familia yake kuwa kama wafalme wenu kwa maana kuchukua ukoo wake, ndugu zake na mengine kuwaweka KWENYE nafasi za kitaifa.
tuweke mifumo ambayo raisi wetu tunamheshimu ndio na anatuongoza lakini hatakiwi kuwa na madaraka makubwa ya kufikia hatua ya kuvunja sheria na hakuna wa kuhoji.
bali tunataka mifumo kama ya ulaya kuwa raisi anaweza kuwa madarakani na akapelekwa mahakamani, na lengo hapa si kumfunga raisi bali kufanya mifumo inayoangalia taifa.
Aise... Yaan watanzania wengine akili zao cjui wanatumia kufanyia nini??...
Wakati nchi nyingi duniani zinajitahidi kurudisha mamlaka kwa wananchi.. cha kushangaza Tanzania kuna mijitu inataka Rais awe na Mamlaka ambayo wakati mwingine ndiyo yanachangia ukiritimba na urasimu kwenye maendeleo ya taifa letu..
Toa mifano ya nchi hizo na madaraka yaliyorudishwa na nchi hizo pia useme mfumo wa utawala wa nchi husika sio ukurupuke tu hapa na kuongea ovyo!
Ukisharuhusu kufikiri kwa kutumia makalio huwezi kuelewa.. Maana we unachofikiri ni kuwasifia tu wale wanaokutuma..
Nataka nikwambie hata Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inatambua.. 'Mamlaka ya Utawala yatatoka kwa wananchi'
Sasa kama wananchi ndiyo wanamamlaka juu ya utawala ndiyo maana kuna haja ya kumpunguzia huyu Rais ili mamlaka zaidi yarudi kwa wanaoyatoa
Mburura kasome tena.. sio unakurupuka tu.. huhitaji mifano ya nchi nyingine.. wakati Katiba yetu yenyewe inaelekeza hivyo
Mleta mada ungetoa mifano ya nchi ambazo kwa mfumo huu wa kupunguza madaraka kwa raisi zimeathirika na upunguzaji huo.. No research no right to speak..
Halafu msidhani kwamba raisi atakuwa ni wa ccm milele.. Atakapokuja raisi toka kwa chama kingine ndo mtakuja kulia na kusaga meno maana kwa katiba mlioipitisha wenyewe itaanza kuwala wenyewe..
Ukisharuhusu kufikiri kwa kutumia makalio huwezi kuelewa.. Maana we unachofikiri ni kuwasifia tu wale wanaokutuma..
Nataka nikwambie hata Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977 inatambua.. 'Mamlaka ya Utawala yatatoka kwa wananchi'
Sasa kama wananchi ndiyo wanamamlaka juu ya utawala ndiyo maana kuna haja ya kumpunguzia huyu Rais ili mamlaka zaidi yarudi kwa wanaoyatoa
Mburura kasome tena.. sio unakurupuka tu.. huhitaji mifano ya nchi nyingine.. wakati Katiba yetu yenyewe inaelekeza hivyo
Hapa matusi sio eneo lake kama huelewi mada uliza!
Naona hujaelewa debate inayoendelea hapa kasome vizuri topic ndo uje aisee!
Kuna maada hapa!!????
Huu uharoo usiokuwa na tafakuri ya kutosha unatujia server tu..