Katiba inamruhusu JK kumpa Ubunge Mbatia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katiba inamruhusu JK kumpa Ubunge Mbatia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by AMARIDONG, May 4, 2012.

 1. AMARIDONG

  AMARIDONG JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Jun 24, 2010
  Messages: 2,506
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 0
  IBARA YA 55 INAMRUHUSU RAISI KUMTEUA MBATIA KAMA WAZIRI NA KAMA ATAKUWA NAIBU WAZIRI KAMA INAVYOSEMEKAKA NGUVU YAKE ITAKUUWA NDOGO KWANA HATAKUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAWAZIRI


  55.-(1) Mawaziri wote ambao ni wajumbe wa Baraza la
  Mawaziri kwa mujibu wa ibara ya 54 watateuliwa na Rais baada
  ya kushauriana na Waziri Mkuu.
  (2) Pamoja na Mawaziri waliotanjwa katika ibara ndogo ya (1),
  Rais aweza, baada ya kushauriana na Waziri Mkuu, kuwateua
  Naibu Mawaziri. Naibu Mawaziri wote hawatakuwa wajumbe wa
  Baraza la Mawaziri.
  (3) Rais aweza kuteua idadi yoyote ya Naibu Mawaziri ambao
  watawasaidia Mawaziri katika utekelezaji wa kazi na shughuli zao.
  (4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka
  miongoni mwa Wabunge.
  (5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea
  kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada
  ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye
  alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.
   
 2. Simchezo

  Simchezo JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 225
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Hi Wana JK, Hivi kuna kifungu chochote kwenye sheria zetu kinachomruhusu Rais kuteua wabunge wa upinzani kuwa mawaziri? Thx!!!!!
   
 3. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nimekuwa nikijiuliza sana hili, acha wanaojua watasema tukapanua maarifa
   
 4. a

  afwe JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160

  It is a good piece of information. Thank you
   
 5. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  thank you MINJA kwa kutetea MBATIA

  hii haiondoi ile fact aliyosema halima kwamba Mbatia ni kibaraka wa CCM
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Swali dogo, Ikitokea Chadema wameshinda urais kwa 51% na CCM wakapata 49% ya popular vote, lakini Bungeni majority wabunge CCM kwa tofauti ya viti vichache. Ila CUF, UDP, NCCR ,TLP wabunge wao wanatosha kuipa Chadema majority je Chadema haitahitaji kuwa na mawaziri wa vyama vingine including CCM yenyewe?

  Tafakari...
   
 7. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Sheria haimbani Raisi katika uteuzi wake wa baraza la mawaziri...anaweza kumchagua mbunge yeyote kuwa waziri either kutoka chama chake au chama cha upinzani sema imezoeleka kuwa chama kinachoshinda mara nyingi kinachagua mawaziri watakaounda serikali kutoka miongoni mwa makada wa chama chake bungeni..raisi akitamani mtu flani ambaye sio mbunge awe waziri huwa anatumia uwezo/ mamlaka yake ya kikatiba kumteua mtu huyo awe mbunge kwanza n then baadae namteua kuwa waziri kwa kuwa tayari ni mbunge...aina ya serikali inayoundwa kwa staili hii ndiyo wanaiita serikali ya mseto...
   
 8. S

  SURA SIO SOHO Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ikitokea tutajua cha kufanya
   
 9. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wananishangaza sana; Kama Rais kaamua kumteua Mbatia kwa mamlaka aliyopewa kwenye katiba kuna tatizo gani? Hii ni political maturity; Mbatia ameonyesha nia ya kuwatumikia Watanzania kwa muda mrefu sana. Kagombea Ubunge Kawe, kura hazikutimia. Akaenda Mahakamani, lakini kwa kutumia uungwana wake, akaondosha kesi. Akagombea Afrika Mashariki, mambo hayakuwa mazuri. Sasa Rais, akaona ni vyema aende Bungeni akatoe sauti yake kwenye chombo cha kutunga sheria. Watu hawajaridhika! Hivi kuna kosa Rais kumteua Mbatia? mie naona ni ukomavu wa siasa
   
 10. W

  WildCard JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Makame,
  Nakuunga mkono sana kwa JMK wetu kutumia ukomavu wake wa kisiasa kumteua Mbatia kuwa Mbunge. Lakini Rais alitengewa nafasi hizi 10 kwenye KATIBA yetu ya JMT ili azitumie vizuri kupata WATANZANIA waadilifu, wachapakazi, thinktanks watakaomsaidia yeye na TAIFA hili ili tusonge mbele. Watu ambao wanaweza kutoa majibu mazuri katika maswali magumu yanayolikabili Taifa hili. Watu ambao hata wakiteuliwa Watanzania wawakubali. Mbatia ni mmoja wao kweli?
  Tunao Watanzania wanaostahili teuzi kama hizi. Akina Jenerali, Prof Issa Shivji, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta, Mzee Mwanakijiji,... Nahisi Rais wetu hazitumii vizuri fursa hizi za kuteua na ndio maana haishi kuunda na kuteua kila wiki kama sio kila siku.
   
 11. S

  Stoudemire JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 840
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Naomba rekodi ya huyo bwana aliwahi kufanya kazi wapi na alipata mafanikio gani?

  Au unataka apewe cheo kwa uhodari wake wa kuleta hoja hapa JF?

  Ni nini kinakufanya uamini Shivji na Jenerali wanaweza kuwa viongozi wazuri?
   
 12. Vato

  Vato JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Feb 15, 2009
  Messages: 230
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 33
  Mtu kama Mwanakijiji au Shivji kumpa uwaziri katika serikali ya JK ni kama kumharibu/ku under utilise uwezo wake wa kufikiria...ni vizuri wakafanywa kuwa wakuu wa THINK TANKS flani katika organs za serikalli badala ya wasimamizi wa utendaji katika wizara..haha
   
 13. M

  Mgongo wa paka JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 486
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Acheni udaku vitu visivyo na fact
   
Loading...