Katiba ya warioba haingeongelea mambo hayo kwa sababu kwenye mfumo wa serikali tatu, hayo siyo mambo ya muungano! Hayo mambo yote yangetajwa kwenye katiba ya Tanganyika na katiba ya Zanzibar. CCM wamewatupia changa la macho tena wananchi kama wewe kwa kuwaambia eti mzisome rasimu zote mbili mzilinganishe wakati siyo sahihi kufanya hivyo! Ya warioba ilijikita kwenye yale mambo ya muungano tu! Mambo ya ardhi, vijana, wakulima, wavuvi na kadhalika yote yangetajwa kwenye katiba za nchi washirika. Sijui umeelewa?!
Umeniuliza swali moja tu nalo ni 'Kwahiyo hapa hoja ya UKAWA ni serikali 3, mambo mengine ya wananchi wao hayawahusu.' Naamini nimekujibu vilivyo!
Sio kifungu ni ibara vifungu vinaaply ktk acts eg Public service act no 8 of 2002 dk 2 nakuletea
Wewe inaelekea haujaelewa issue ya separation of powers (kutenga serikali na bunge) au 'trias politica', kwa lugha ya wanasheria. Kuwa na makamu wa rais watatu halafu bado mawaziri wanatokana na wabunge siyo separation of powers hata kidogo, na wala vitu hivi viwili havina uhusiano wowote! Kamdanganye mtu mwingine. Kweli nimeanza kuamini ile hoja kwamba wasomi wengi ndio wanaoipinga CCM na wasiosoma ndio mnaikubali! Serikali maanake ni rais na mawaziri wake kwenye nchi zenye presidential system (USA, kenya) au waziri mkuu na baraza lake la mawaziri kwenye nchi zenye parliamentary system (UK, France). Sisi hapa mfumo wetu haueleweki kwa vile unadalili za kuwa pande zote mbili. mawaziri kutokana na wabunge hiyo ni parliamentary system, na mawaziri kutotokana na wabunge ni presidential system. Sasa ili ujue mfumo wetu ni wa ovyo, na inasikitisha kwamba tumeamua kuendelea nao, kwenye parliamentary system lazima mkuu wa nchi awe tofauti na kiongozi wa serikali (Rais anakuwa mkuu wa nchi tu na waziri mkuu anakuwa mkuu wa serikali). Hapa kwetu tunampa Rais majukumu yote hayo (ambayo ni characteristic ya presidential system) lakini bado mawaziri wanateuliwa kutokana na wabunge (ambayo ni characteristic ya parliamentary system). Sijui umenielewa? Kwa mfano, ikiwai kutokea Rais anatoka CHADEMA halafu chama chenye wabunge wengi bungeni ni CCM, huyo rais atalazimika kuchagua mawaziri wa CCM, na kwa kifupi tu nchi itaingia kwenye political gridlock! Sasa hivi tumetulia kwa vile haijawahi kutokea hivyo.OK. Sasa wewe ulikuwa unataka Serikali tatu au moja au ya mkataba?
Ukotayari kujifunza mantiki ya serikali mbili?
Hebu soma vipengere vyote.
Halafu hebu niambie nitatizo gani kuwa na serikali mbili?
Kwasababu katika mantiki yako ya serikali tatu inatekelezwa kwa kuwa na makamu watatu wa rais
1. Makamu wa kwanza ndiye aliye na mamlaka kote
2. Makamu wa pili wa raisi ndiye Raisi wa zanzibar.
3 Makamu wa tatu wa rais ndiye mtendaji mkuu wa serikali kwa mantiki hiyo ndiye msimamizi wa mambo ya Muungano na mambo yote ya Tanzania bara.
Halafu ikumbukwe Makamu wa kwanza wa rais na makamu wa tatu wa rais wanasifa ya kuwa marais wa JMT ikitokea rais hayupo.
Serikali, Mahakama na Bunge vimetenganishwa.
Katika Rasimu ya pili Jaji na Spika walikuwa na uwezo wa kuwa Rais.
Huoni ingeleta mgongano wa maslahi. Maana Spika anaweza akashirikiana na wabinge au vyoyote kumuondoa rais.
Na ikubukwe kwenye Rasimu hii ya mwisho wabunge wanao uwezo wa kumuondoa rais madarakani.
Sijui umeelewa!!!!
-------------
Usilete ushabik kwa mfumo uliopo wa serikali mbili hayo mambo hayawez kutekelezeka labda arudi masia" kwa utitiri wa wabunge 360 na makamu wa raisi watatu kwa budget ipi watz ebu zindukeni kutoka ucngizini hizi sanaa tu
Pamoja na kujadili mambo ya muungano, ni lazima rasimu ya warioba ingeweka 'framework' au mwongozo kwa hizi katiba za washirika ili kuzuia migongano, na kulinda haki za binadamu ni moja ya miongozo hii. Ndio maana kuna kipengele kikasema 'sheria yoyote itakayotungwa na chombo cha dola cha nchi washirika inayotofautiana na katiba hii, basi sheria hiyo itakuwa ni batili'Kama ilijikita kwenye mambo ya muungano kwann iongelee haki za binadamu?
Kwa sababu upo Tanzania ndo maana tunatumia katiba ya Tanzania..... Na Wala Hakuna Uzuri Wowote Hapo, Uvundo Tu. Mfano, Ardhi Ni Suala La Muungano? Mbona Lipo Kwnye Katiba Ya Tanzania.
Vitu kama haki za binadam watoto na makundi mengine maalum tayari ipo kwenye sheria na mikataba ya kimataifa.kwa hiyo sisi wa Tz bado tunasisitiza kkuwa kuna mambo muhim wame yatupaSURA YA TANO
HAKI ZA BINADAMU, WAJIBU WA RAIA, JAMII NA MAMLAKA ZA NCHI
Code:Hii inazungumzia haki za Binadamu na Wajibu wa raia. Pia tena inatoa mipaka ya haki za binadamu hebu tujaribu kuisoma vizuri
Pamoja na kujadili mambo ya muungano, ni lazima rasimu ya warioba ingeweka 'framework' au mwongozo kwa hizi katiba za washirika ili kuzuia migongano, na kulinda haki za binadamu ni moja ya miongozo hii. Ndio maana kuna kipengele kikasema 'sheria yoyote itakayotungwa na chombo cha dola cha nchi washirika inayotofautiana na katiba hii, basi sheria hiyo itakuwa ni batili'
Vitu kama haki za binadam watoto na makundi mengine maalum tayari ipo kwenye sheria na mikataba ya kimataifa.kwa hiyo sisi wa Tz bado tunasisitiza kkuwa kuna mambo muhim wame yatupa
Pamoja na kujadili mambo ya muungano, ni lazima rasimu ya warioba ingeweka 'framework' au mwongozo kwa hizi katiba za washirika ili kuzuia migongano, na kulinda haki za binadamu ni moja ya miongozo hii. Ndio maana kuna kipengele kikasema 'sheria yoyote itakayotungwa na chombo cha dola cha nchi washirika inayotofautiana na katiba hii, basi sheria hiyo itakuwa ni batili'
Okay, tuweke hilo kando, ingawaje hujajibu hoja zangu hata kidogo! Naendelea kusisitiza idadi ya makamu wa rais siyo separation of powers. Hata spika akifuata kuwa rais ni temporary na siyo permanent, hutokea rais na makamu wake wakiwa hawawezi kutekeleza majukumu yao tu! Nchi nyingi hufanya hivyo kwa kuzingatia kuwa wao ni viongozi wa mihimili mitatu ya dola, hivyo basi ndio viongozi wakuu wa nchi (waziri mkuu, spika na jaji mkuu)Ndugu yangu mawaziri ndio watekelezaji wa sera za serikali iliyopo madarakani.
Halafu kwann unatolea mfano wa nchi za magharibi tu?
Spika yeye ni msimamizi wa chombo cha kutunga sheria na ni msimamizi wa chombo cha kuiwajibisha serikali. Sasa spika huyo huyo awe na madaraka ya kuwa rais atatasimamia kweli kuiwajibisha serikali?
Jaji mkuu yeye kazi yake ni justice. Kutafuta haki. Kuweza kuweza kutoa haki kulingana na sheria zilizotungwa na bunge na zinasimamiwa na serikali kupitia vyombo vyake vya kusimamia sheria.
Sasa jaji akiwa tena ni rais wapi na wapi.
Si kila kitu cha magharibi tuna fuata la hasha. mazuri tunafuata yanayotufaa yasiyotufaa tunaachana nayo.
Halafu umeongelea USA hivi unawajua viongozi wa kamati mbali mbali za seneti. asilimia kubwa wametoka chama tawala. jaribu kusoma uone.
Na ndio maana rasimu hiyo ilibidi ipitie kwenye bunge maalum la katiba, ili kui fine-tune na kuondoa makosa kama hayo, lakini siyo kubadilisha na ku overhaul rasimu nzima! ilibidi CA ifanyie kazi rasimu ya warioba kama ilivyoletwa!Vile vile nataka kuongezea. Rasimu ya pili ilikuwa na tatizo moja kubwa sana katika swala la ulinzi wa nchi.
Maana iliwaruhusu maraisi kuanzisha vyombo vya ulinzi. Hivi wewe unatetea tu hii kitu. Matokeo yake kungesababisha kugongana kwa amri.
Kwenye kipengere hiki tu. kilinifanya niimi kuwa kuna ajenda ya siri nyuma.
... Tanzania Kweli Wapumbavu Wengi Sana, Kaz Ipo
Mpaka hapo tumepata makosa mangapi yaliyo kwenye Rasimu ya pili?Na ndio maana rasimu hiyo ilibidi ipitie kwenye bunge maalum la katiba, ili kui fine-tune na kuondoa makosa kama hayo, lakini siyo kubadilisha na ku overhaul rasimu nzima! ilibidi CA ifanyie kazi rasimu ya warioba kama ilivyoletwa!
Unaonekana umesoma lakini huna uwezo wa kutumia elimu yako kusaidia jamii yako
Kama ardhi imewekwa kuwa ndiyo rasilimali muhimu itamilikiwaje na watu wenyekipato kidogo na hawana fursa kama yako?
Wanawake walikuwa na shangwe kuwa 50/50 na fursa ya kumiliki ardhi ipi katika familia au wapi mbona hata sasa wapo wanaomilki ardhi tena wegi tu ila wenye fedha lakini wenye hawana hata wanaume hawana fursa hiyo na waliobahatika kurithi za wazazi wananyang'anywa na wenye fedha.
Tumieni kalamu zenu kufanya mambo kwa maslahi ya wanyonge na si wenye nacho kama mnavyofanya sasa.