Katiba imekaa vizuri sana

Hii ndiyo ilikuwa rasimu ya ukweli. Soma kwa makini utagundua kuwa unaongozwa kwa ushabiki zaidi.
Japo kuwa umeandika kwa mwandiko mdogo sana hebu soma Ibara 28 kifungu cha 2

Angalia na hapa
 
... Mkuu, Huyo Jamaa Atakuwa Kada Wa Ccm, Anajaribu Aone Kama Takataka Yao Inakubarika Au La

Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!
 
Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!

Utaonaje ubaya wake na wewe ni gamba?
 
Ungetafuta wasaa ukatuliza akili na kuisoma hii rasimu iliyopendekezwa usingeandika hivi. Tatizo lenu ni wavivu wa kujisomea.

Mimi binafsi sijaona ubaya wake!

... Ni Kwavile Umevaa Miwani Ya Mbao, Ndo Maana..
 
Katiba imepitishwa kiujanja ujanja na magamba pale Dodoma, na wewe ni gamba mwenzao japokua hukwenda Dom. Utaionaje ubaya wake?
 
... Nasikia Huyu Annael Siyo Mtanzania, Ni Mganda Alikimbia Vita Ya Idd Amin
 
Japo kuwa umeandika kwa mwandiko mdogo sana hebu soma Ibara 28 kifungu cha 2


Angalia na hapa

Tofauti yake ni kwamba rasimu ya Warioba ilikuwa moja moja bila kumung´unya maneno; huu uchafu wa 6 unajikanyagakanyaga na kutupia mpira bunge ambalo pia wanajua kuwa kwa kuruhusu darasa la saba kama "Kibajaji" kuwa wabunge, hilo bunge halitatunga chochote cha maana.
 
Nashukuru sana ndugu yangu ila umesahau kimoja hebu soma hapa
 
Kaka hapo ndio unapo enda tofauti. Kumdharau mtu sio vyema hebu tu chambue kwa hoja.
Unajua kuna vitu vingine vinatakiwa viwekwe kwenye sheria maana vinabadilika kila wakati.

Hebu jaribu na kujisomea hapa
 
... Nasikia Huyu Annael Siyo Mtanzania, Ni Mganda Alikimbia Vita Ya Idd Amin
Mnyarwanda vipi tena. Umeanza kubabaika na kurukia kila tawi.
 
tume ya mipango
 
lengo la kijamii

 


Hizi ni porojo tu ambazo hazina tofauti sana na yaliyomo kwenye katiba ya sasa. Hii rasimu ya Sitta na Vijisenti imejaa unafiki na mambo yaleyale ya kale. Imekosa ujasiri wa kukataza maovu moja kwa moja. Kusema kwamba darasa la saba wasiruhusiwe kuwa wabunge sio ubaguzi, ni swala linalojibu mahitaji ya nyakati hizi za sasa; hivi mbunge wa darasa la saba atakuwa na kichwa cha kuchambua na kuhoji mkataba wa serikali na Statoil? darasa la saba anakichwa cha kuchambua hesabu za serikali? Matokeo yake ndiyo unakuwa na wabunge wenye hoja kama za John Komba (aka usingizi) kumuita Warioba shiiida.
 

Heshima kwako. Tatizo haujui kazi ya mbunge ni nini.
Hebu twende kipengere kwa kipengere kuhusu katiba ya iliyopo na rasimu hii.

Halafu useme kama ziko sawa.
 
cha msingi katiba haiwezi kumfanya kila mtanzania kuwa na maisha bora....! fanya kazi ndipo maisha bora yatakuja!
 
Heshima kwako. Tatizo haujui kazi ya mbunge ni nini.
Hebu twende kipengere kwa kipengere kuhusu katiba ya iliyopo na rasimu hii.

Halafu useme kama ziko sawa.

Haziko sawa, zingekuwa sawa wasingemwita Warioba shiida. Huitaji masters degree kulibaini hilo.
 
Haziko sawa, zingekuwa sawa wasingemwita Warioba shiida. Huitaji masters degree kulibaini hilo.
Mkuu wewe unapinga kitu gani? Hebu twende pointi kwa pointi. Maana nimekupa vipengere haujapinga kwa hoja. Naomba Labda unipe kipengere kwa kipengere tofauti ya Rasimu ya Tume na hii ya Bunge maalumu.

Maana tukiongea tuuu hatutamaliza.
Nawasilisha hoja.
 
Kwenye tatizo ni huko kwenye uongozi wa nchi. Kwa nini waliondoa vipengele muhimu kama wananchi kuwawajibisha wabunge na wanabunge kuwa watu wenye elimu ya form four? ndiyo maana bunge letu litaendelea kuwa substandard na lisilokuwa na viwango. Pia muundo huu wa muungano ni wa ovyo sana haijawai tokea. Kwa nini tusiwe na serikali moja au tatu ili muungano ueleweke? Sasa hivi Tanganyika inaminywa tu na wazanzibar wanadandia tu!
Hii katiba yetu huwezi kusimama hata kuilinganisha na katiba za nchi kama Kenya au SA au Ghana......haina viwango na ni ya kuundwa kimagendo kwa maslahi ya chama kimoja! Huu mpasuko wa kisiasa uliojitokeza lazima utaadhiri utekelezwaji wa katiba mpya pindi itakapokubaliwa na wananchi. Ila CCM kwa vile wanadhani watabaki madarakani milele, ndio maana wamepitisha katiba ya ovyo kama hii! Katiba inafaaa kuwa chama chochote kikishika dola kinaridhika na muundo wa serikali uliopo na si vinginevyo!
 
Ongelea katiba na pointi kwa point sio kuleta porojo hapa. Tao ibara ipi unaipinga kwanini. Sio kutoa bra bra tu.

Amir jeshi wa Tanzania ni nani? Je Rais wa Zanzibar anapigiwa mizinga kama nani? Sherehe za Mapinduzi nani anatangulia uwanjani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…