Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
Nimeipitia katiba kipengere kwa kipengere.
Hakika imekaa vizuri sana. nimekuwa nikijiuliza wale wanaoipinga wanapinga kwa hoja zipi!!?
Ailimia kubwa mambo yaliyopendekezwa na tume ya Warioba yamo.
Eti kwa sababu tu kwamba serikali tatu haipo.
Asilimia kubwa ya watu wanaisoma kwa mrengo wa kuipinga. Hawako na free mind.
Kuna mambo mazuri sana mengi. Mfano:
Na kuna mambo mengi sana nitaendelea kuya toa.

22.-(1) Ardhi ndiyo rasilimali kuu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi,
kijamii na ustawi wa nchi na watu wake wote. Serikali ya Jamhuri ya Muungano
itaweka mipango bora ya matumizi endelevu ya ardhi kwa faida ya kizazi
kilichopo na vizazi vijavyo.
(2) Ardhi yote itamilikiwa, itatumiwa na kusimamiwa kama
itakavyoainishwa na sheria itakayotungwa na Bunge kwa kuzingatia misingi
ifuatayo:
(a) raia wa Tanzania pekee ndiye atakayekuwa na haki ya kumiliki
ardhi ya Tanzania, na haki hiyo italindwa kwa mujibu wa Katiba hii;
(b) mtu ambaye siyo raia wa Tanzania atakuwa na fursa ya kutumia
ardhi kwa ajili ya uwekezaji na maendeleo mengine ya kiuchumi na
makaazi;
(c) haki ya kumiliki, kuendeleza na kuhifadhi ardhi kwa ajili ya
makundi mbalimbali ya jamii wakiwemo wakulima, wavuvi,
wafugaji na makundi madogo itatambuliwa na kulindwa kwa mujibu
wa Ibara hii; na
(d) kila mwanamke atakuwa na haki ya kupata, kumiliki, kutumia,
kuendeleza na kusimamia ardhi kwa masharti yaleyale kama ilivyo
kwa mwanaume.
Na kuna mambo mengi sana nitaendelea kuya toa.