Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Kwa maana leo hii ukimuuliza Mbongo kwa nini nchi yake masikini unapata jibu haraka Katiba mbovu, kwanini watoto hawasomi jibu Katiba mbovu, kwa nini mafisadi wanaitafuna nchi jibu Katiba mbovu, kwa nini UKIMWI unamaliza watu jibu Katiba mbovu, kwa nini ajali zinamaliza watu jibu Katiba mbovu yaani kila kitu jibu lake ni Katiba mbovu!
Sasa swali langu mkipata hiyo katiba mnayoitaka, mtakuja na singo gani nyingine ya kusingizia?
Najua lazima mtaipata kwa maana historia yetu inatuonyesha hivyo kwamba kila wkt tulikuwa tunatafuta kisingizio cha kushindwa kwetu kuendelea kama jamii nyingine Duniani.
Tulianza na utumwa kwamba watu wetu wenye nguvu waliuzwa utumwani hivyo tukakosa watu wa kufanya kazi ndiyo maana tukawa masikini, ikaja Ukoloni Wazungu walitunyonya wakatuibia kwa kutusainisha mikataba ya kilaghai ndiyo maana tukawa masikini, tukapata Uhuru ikaja Wazungu wanatuibia kwa kutumia Ukoloni mamboleo ndiyo maana tumebakia kuwa masikini, ikaja Globalization wakulima wetu wanashindwa kushindana kwa sababu Wazungu wanasubsidies Wakulima wao ndiyo maana tumebakia masikini!
Sasa hiyo singo imeisha na tumepata nyingine ya Katiba kwamba tuna Katiba mbovu ndiyo maana tumebakia masikini ikumbukwe kwamba hii Katiba inayoitwa mbovu inatumika jamii nyingi Duniani kama Uchina, Singapore, Vietnam, ilitumika kujenga Korea Kusini, ikajenga Taiwan, ikaendeleza Ujerumani, Japan, Uingereza, Chile, Afrika Kusini lkn kwetu imeshindwa,
Sasa swali langu Je hiyo mpya italeta miujiza gani kama kwa miaka zaidi ya 200 ingawaje tuliyoyapitia wengine wameyapitia pia kama Ukoloni, Utumwa, Katiba mbovu lkn leo hii wako mbele sana kiuchumi!