HEKIMA KWANZA
JF-Expert Member
- Mar 31, 2015
- 2,942
- 3,937
Vyombo vya habari Tanzania wakuwa wanalia kila kukicha kuwa serikali inaminya uhuru wa habari. Lakini kuna jambo linanitatiza na ningeomba 'Great thinkers' mnisaidie.
Jukumu la msingi la vyombo vya habari ni kutoa habari za kweli kwa umma ama waandishi wanazipenda au hawazipendi taarifa au hata chanzo cha taarifa. Tafsri yake ni kwambwa waandishi wa habari wanatakiwa kufanya kazi zao bila kuongozwa na hisia, itikidi au imani zao.
Mfano, kwa wale wanaofuatilia siasa za Marekani, Rais Trump amekuwa anatoleana maneno na vyombo vya habari na kuviita 'fake news' lakini waandishi wameendelea kuwapa habari wananchi bila kujali wanachukizwa na kauli za Trump.
Lakini hapa Tanzania naona shida, ikitokea kiongozi anakosana na waandishi wa habari, ghafla waandishi wanatangaza kususia kuandika taarifa zozote zinazomhusu kiongozi huyo. Kitendo hiki kinaonesha kuwa waandishi wa habari wa Tanzania wanatoa habari wanazozipenda wao, wanawachagulia wananchi ni habari gani wanatakiwa kuisoma kutokana na hisia, itikidi au 'maelewano' wa wahusika.
Sasa, kwanini waandishi habari wa Tanzania wanawaamulia Watanzania ni habari gani wasome? dhana ya 'impartiality' iko wapi? na kuendelea KUCHUJA habari kutokana na ugomvi binafsi na watu, waandishi wanatofauti gani ni kile wanachodai kuwa serikali inaminya uhuru wa habari?