Kati ya sentensi zifuatazo, ipi sahihi?

mwachisabwe kibona

Senior Member
Aug 5, 2014
116
27
1:mtu yeyote atakayemwona mtoto HUYO atoe taarifa polisi
2:mtu yeyote atakaemuona mtoto HUYU atoe taarifa polisi
nawasilisha
 
tafasiri hizi sentensi mbili kwa mtazamo wa "hapa na pale".
inategemea na mazingira na wakati ambapo mtoa taarifa ana habarisha. kwangu mimi zote ni sahihi
 
tafasiri hizi sentensi mbili kwa mtazamo wa "hapa na pale".
inategemea na mazingira na wakati ambapo mtoa taarifa ana habarisha. kwangu mimi zote ni sahihi

on second note, nadhani ya pili ni sahihi zaidi. "mwona" si sahihi, "muona" ni kiswahili sanifu
 
sentensi ya pili ni sahihi zaidi. neno "atakayemuona" ni kiswahili sanifu zaidi ya atakayemwona sio neno sahihi
 
1: "mwona" "HUYO"

2: "emuona"
nadhani makosa ni hayo
 
1:mtu yeyote atakayemwona mtoto HUYO atoe taarifa polisi
2:mtu yeyote atakaemuona mtoto HUYU atoe taarifa polisi
nawasilisha

Zote ni sahihi, ila zimeandikwa katika maumbo tofautitofauti. Ya kwanza, neno mwona limeandikwa katika umbo la ndani, na neno muona limeandikwa katika umbo la nje
 
1:mtu yeyote atakayemwona mtoto HUYO atoe taarifa polisi
2:mtu yeyote atakaemuona mtoto HUYU atoe taarifa polisi
nawasilisha

kimatamshi sentens zote zipo sahihi..kwa kuwa moja inarahisisha matamshi.
katiks kisw..irabu " U" ikifuatiwa na irabu yoyote isipokuwa U" bas umbo ubadilika na kuwa " W" na hiyo kitaalamu s badiliko la kimofolojia wala kifonolojia ni badiliko la kimofofonolojia. mf hiyo mu-ona imekuwa mwona
u-embe inakuwa wembe
mu-ana inakuwa mwana
mu- imbaji inakuwa mwimbaji
u-imbo inakuwa wimbo nk
katika uandishi wa lugha ya kiswahili sentesi ya pili ipo sahihi yenye neno "muona" kwa sababu kila kipashio(element) inayojenga neno lazima ionyeshe kazi yake kama mofimo. hivyo katka uandishi sentens ya kwanza haipo sahihi kwa sababu utashindwa kuchanganua kazi ya kila mofimo ktk neno "mwona"
nafikir utakuwa umeelewa vizuri.
 
Huyo.. mbali
huyu.. karibu au unaelezea kwa kuishika picha yake au jina lake mana obviously km ujamwona basi ayupo karibu
 
Zote zipo sawa ila kwa kiswahili sanifu kabisa hiyo sentensi namba 1 inakiswahili sanifu hapa: yeyote >atakaye>hizo ye zinasimama kwa nafsi ya mtu. Hicho kitenzi mwona badala ya muona haiko sawa sana.
 
on second note, nadhani ya pili ni sahihi zaidi. "mwona" si sahihi, "muona" ni kiswahili sanifu

vp kuhusu mantink ya sentensi kwa ujumla ,ivi unaweza tafuta mtu uliye nae karib (Huyu) au unatafuta mtu uliye nae mbali (huyo) ufafanuzi tafadhari ,,,
 
Back
Top Bottom