mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
Kwa sasa Kuna mjadala wa kipi kianze Kati ya katiba ya wananchi na Tume huru ya Uchaguzi.
Mvutano mkubwa unaonekana katika vyama viwili vya ACT Wazalendo na Chadema.
ACT Wazalendo wanataka ianze Tume huru ya Uchaguzi katika kuiendea katiba mpya na Chadema wanataka katiba mpya kwenye kuiendea Tume huru.
Mawazo yao yamewaingiza katika uadui mkubwa huku upande wa ACT Wazalendo ukijenga hoja ya kwanini ni muhimu kuanza na Tume huru na Chadema wakiwangooshea vidole na kuwatukana wakati mwingine kuwa wanatumiwa na serikali kuihujumu
Katika hatua hii Kuna makundi ya watu wenye ushawishi wametoa maoni yao.
Miongoni mwao ni Maria Sarungi kupitia bunge la Space anayetaka katiba mpya kwa kuungana na Chadema
Lakini wote hao hawasemi wataifikia vipi katiba mpya kutoka katika kura za wananchi hadi tume ya Sasa yenye jukumu la kuhesabu kura za maoni zitakazopigwa.
Kwa upande wa ACT Wazalendo,mawazo yao yanaungwa mkono na wanasheria nguli wa Chadema, Peter Kibatala na Tundu Lissu kuwa ni muhimu kuanza na Tume huru kabla ya Katiba mpya huku wakielezea sababu zao.
Kibatala amesema katika moja ya mahojiano na Clouds Tv kuwa sheria ya mabadiliko ya katiba ya Jaji warioba inataja tume ya uchaguzi ya Taifa NEC na ZEC kuwa ndiyo watakaosimamia kura za maoni kwenye kuipata katiba mpya.
Anasema hiyo tume isipokuwa huru hata wananchi asilimia 98 wakiwa wamepigwa kura ya kuidhinisha katiba mpya tume hizo zinaweza kupindisha ukweli na wananchi wakapoteza haki zao.
Pia Tundu Lissu kwa mlango wa Nyuma amesema mchakato wa Katiba uanze na ikiwa itafikia Uchaguzi wa 2024-25 katiba ikiwa haijaakamilika basi iundwe Tume huru,itakayosimamia Uchaguzi huo.
Kauli yake hii ambayo kwa namna moja ama nyingine imebeba tahadhari zote za kuzuia ukosolewaji ndani ya chama inaashiria wazi tamanio lake ni kuanza na Tume huru kabla ya Katiba mpya.
Kwa hiyo utaona mitazamo ya ACT Wazalendo na hao wanasheria nguli kwa pamoja kwao muhimu ni TUME huru Kwanza kabla ya Katiba.
Na Kibatala amekuwa muwazi zaidi katika hili tofauti na Lissu,anayesema chaguo lake kwa kuzunguka