Katazo la Rais kuzuia mikutano ya siasa kweli limekuwa sheria katika nchi ya wasomi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,710
149,949
Mahakama huko nchini Marekani imefuta zuio la Rais wa nchi hiyo tena la "kimaandishi" la kuzua waislamu kutoka mataifa saba duniani kuingia nchini humo.

Kilichofanyija Marekani ndio kinaitwa utawala wa sheria na kinathibitisha kuwa katika nchi hiyo hakuna alie juu ya sheria tofauti na hapa kwetu.

Sasa sisi Katiba yetu inatambua uwepo wa mikutano ya siasa lakini serikali(sijui kama ni Raisi au Jeshi la Polisi) linajitojeza hadharani kupiga marufuku mikutano hiyo na kuiwekea masharitu mapya ya namna mikutano hiyo itakavyofanyika mashariti ambayo sijui yako katika sheria gani ya nchi hii.

Kuna wakati nilisikia CHADEMA wamefungua kesi Mahakanani(sina uhakika sana) kupinga amri hii ya serikali ila nashangaa mpaka leo sioni dalili yoyote kuwa kuna kesi kama hii Mahakamani na wala sijui itatajwa lini kama kweli ipo.

Nachojiuluza kama kweli kesi hii ipo kwanini hawakuipa uzito kwa kuifungua chini ya hati ya dharura?

Je,kesi hii ikichukua miaka 3 na zaidi nani atakuwa na hasara?

Kama kweli kesi hii ipo haiwezakani kuifungua upya kwa hati ya dharura Mahakama Kuu/ Mahakama Kuu Kitengo cha Katiba?

Chama cha wanasheria cha nchii na chenyewe kimechukua hatu gani?

Jukwaa la Katiba nao wamechukua hatua gani?

Kama hakuna kabisa kesi ya kupinga amri hiyo ya serikali,kweli sisi tuko serious au sisi ni wapiga kelele tu?

Kesho wakija na amri nyingine tutashangaa?

Kila mtu ni mtu lakini si kila mtu ni binadamu (anae-fit definition ya human being)

Sisi sijui tuko wapi hapo.

Mod 3 , Mod 4 naomba mbadilishe hiyo heading isomeke katazo la serikali.
 
Mkuu
Vyama tawala Afrika haviwezi kukupa haki ya mikutano hadi udai kwa nguvu
Kenya mwana mapinduzi Martin Shikuku na wenzake walikuwa wanatiwa mahabusu kila siku
Malawi Mzee Chakufya Chihana na John Tembo kila siku Kamuzu Banda akawa anawatia jela
Zambia akina Chiluba na Mwanawasa walionja joto kwa Kaunda
Zazibar hapa akina Maalim walikuwa wanawekwa kizuizini kwa miaka lkn sasa Maalim yupo huru hadi kujitangazia matokeo na hawezi kamatwa sababu CCM inaogopa watu waliopo nyuma yake ZNZ

Huku Bara hawa ndimi mbili akina Lissu waoga kweli kweli!Wanafikiri kuwa Magufuli atawaruhusu kukutana bila kulazimisha!Wala hawajui kuwa Rais kuruhusu wao kukutana ni kuanika madudu yake na kujipunguzia yeye kura 2020 na idadi ya wabunge wake

Wana CHADEMA walikuwa tayari kuandamana kudai UKUTA lkn Lowassa anasema kuandamana ni siasa za kizamani!CHADEMA imeisha kufa na Rais atafanya apendalo na 2020 CUF kitakuwa chama kikubwa cha upinzani
 
Mr mahakama za wenzetu majaji wanajiamini,ukiwa na majaji ambao wengi wao ni makada wa ccm unategemea nini,Kama jeshi letu ndio walinzi wetu wote raia wa nchi hii,Leo wanachaguliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya,Leo ikitokea mtifuano wa upinzani na ccm nani anaweza kusimama katikati wakati wanajeshi wetu wengi ni makada wa ccm na pia ni wakuu wa wilaya na mkoa na ambao ni wajumbe wa halmashauri wa chama mkoa na wilaya.wewe Kama kesi ya Lema ina dhamana na hakim anakubali kutoa dhamana dakika chache anaitwa chemba baadaye a anarudi Anabadilisha mawazo unategemea maagizo alitoa wapi.nchi hii katiba haizingatiwi Bali matakwa ya ccm ndio katiba yetu.lile li katiba ni boya tu la katiba
 
Marekani majaji hawateuliwi na rais
Na wanasheria wa serikali hawateuliwi na rais.

Sasa hapa tz kuna mtu ambaye atake Thubutu kumkoromea boss wake?

Suala la kuzuiliwa mikutano sio suala la chadema, mwanasheria mkuu alipaswa yeye mwenyewe kupinga kauli za rais ambazo zinavunja katiba, lakini ni kinyume chake, haina haja ya kuwa na mwanasheria ambae alie shindwa kuilinda katiba kwa kulinda mboga yake
 
Mr mahakama za wenzetu majaji wanajiamini,ukiwa na majaji ambao wengi wao ni makada wa ccm unategemea nini,Kama jeshi letu ndio walinzi wetu wote raia wa nchi hii,Leo wanachaguliwa kuwa wakuu wa mikoa na wilaya,Leo ikitokea mtifuano wa upinzani na ccm nani anaweza kusimama katikati wakati wanajeshi wetu wengi ni makada wa ccm na pia ni wakuu wa wilaya na mkoa na ambao ni wajumbe wa halmashauri wa chama mkoa na wilaya.wewe Kama kesi ya Lema ina dhamana na hakim anakubali kutoa dhamana dakika chache anaitwa chemba baadaye a anarudi Anabadilisha mawazo unategemea maagizo alitoa wapi.nchi hii katiba haizingatiwi Bali matakwa ya ccm ndio katiba yetu.lile li katiba ni boya tu la katiba
Huu ndio udhaifu mbaya kuliko wote.Tukiendelea hivi kuacha kuthubutu tutaona maatokeo yake siku si nyingi.
 
Mahakama huko nchini Marekani imefuta zuio la Raisi wa nchi hiyo tena la "kimaandishi" la kuzua waislamu kutoka mataifa saba duniani kuingia nchini Marekani.

Kilichofanyija Marekani ndio kinaitwa utawala wa sheria na kinathibitisha kuwa katika nchi hiyo hakuna alie juu ya sheria tofauti na hapa kwetu.

Sasa sisi Katiba yetu inatambua uwepo wa mikutano ya siasa lakini serikali(sijui kama ni Raisi au Jeshi la Polisi) linajitojeza hadharani kupiga marufuku mikutano hiyo na kuiwekea masharitu mapya ya namna mikutano hiyo itakavyofanyika mashariti ambayo sijui yako katika sheria gani ya nchi hii.

Kuna wakati nilisikia CHADEMA wamefungua kesi Mahakanani(sina uhakika sana) kupinga amri hii ya serikali ila nashangaa mpaka leo sio dalili yoyote kuwa kuna kesi kama hii mahakamani na wala sijui itatajwa lini kama kweli ipo.

Nachojiuluza kama kweli kesi hii ipo kwanini hawakuipa uzito kwa kuifungua chini ya hati ya dharura?

Je,kesi hii ikichukua miaka 3 na zaidi nani atakuwa na hasara?

Kama kweli kesi hii ipo haiwezakani kuifungua upya kwa hati ya dharura Mahakama Kuuu au katika Mahakama ya Katiba?

Chama cha wanasheria cha nchii na chenyewe kimechukua hatu gani?

Jukwaa la Katiba nao wamechukua hatua gani?

Kama hakuna kabisa kesi ya kupinga amri hiyo ya serikali,kweli sisi tuko serious au sisi ni wapiga kelele tu?

Kesho wakija na amri nyingine tutashangaa?

Kila mtu ni mtu lakini si kila mtu ni binadamu (anae-fit definition ya human being)

Sisi sijui tuko wapi hapo.
we endelea kuamini viongozi wako wasanii wa chadema.
Wanachotaka ni cheap popularity tu.Wanaita waandishi wanasema watkwenda mahakamani au watafanya hiki,nyumbu wanashangilia wao wanjifungia wanakunywa bia.
Mfano Lissu alijigamba,Jumatatu fulani atakata rufaa ya lijua kali,mpaka leo kimya.
Lissu alijigamba,wanaongeza nguvu kesi ya lema hadi leo kimya labda kaongeza nguvu za giza hatuzioni.
Usitegemee nchi hii itasogea kwa presha ya upinzani huu wa kisanii
 
Mkuu
Vyama tawala Afrika haviwezi kukupa haki ya mikutano hadi udai kwa nguvu
Kenya mwana mapinduzi Martin Shikuku na wenzake walikuwa wanatiwa mahabusu kila siku
Malawi Mzee Chakufya Chihana na John Tembo kila siku Kamuzu Banda akawa anawatia jela
Zambia akina Chiluba na Mwanawasa walionja joto kwa Kaunda
Zazibar hapa akina Maalim walikuwa wanawekwa kizuizini kwa miaka lkn sasa Maalim yupo huru hadi kujitangazia matokeo na hawezi kamatwa sababu CCM inaogopa watu waliopo nyuma yake ZNZ

Huku Bara hawa ndimi mbili akina Lissu waoga kweli kweli!Wanafikiri kuwa Magufuli atawaruhusu kukutana bila kulazimisha!Wala hawajui kuwa Rais kuruhusu wao kukutana ni kuanika madudu yake na kujipunguzia yeye kura 2020 na idadi ya wabunge wake

Wana CHADEMA walikuwa tayari kuandamana kudai UKUTA lkn Lowassa anasema kuandamana ni siasa za kizamani!CHADEMA imeisha kufa na Rais atafanya apendalo na 2020 CUF kitakuwa chama kikubwa cha upinzani
Katiba ndio tatizo wala rais hana kosa, tatizo katiba ambayo haijawahi pata mzalendo wa kuifanya iwe na maslahi kwa taifa
 
we endelea kuamini viongozi wako wasanii wa chadema.
Wanachotaka ni cheap popularity tu.Wanaita waandishi wanasema watkwenda mahakamani au watafanya hiki,nyumbu wanashangilia wao wanjifungia wanakunywa bia.
Mfano Lissu alijigamba,Jumatatu fulani atakata rufaa ya lijua kali,mpaka leo kimya.
Lissu alijigamba,wanaongeza nguvu kesi ya lema hadi leo kimya labda kaongeza nguvu za giza hatuzioni.
Usitegemee nchi hii itasogea kwa presha ya upinzani huu wa kisanii
Pamoja na madhaifu haya ya upinzani,wewe huna uhalali wa kuwanyooshea kidole kina Lissu kwasababu siku zote umekuwa ukiinga mkono maamuzi ya hii serikali.Ulipaswa kwanza kukataa mambo haya kabla ya kuponda upinzani vinginevyo wewe ni mnafiki wa kiwango cha juu.
 
Tuliwaamini sana wapinzani wametuangusha,hawaaminiki tena kamanda.Ni heri tu kuungana na serikali kuliko kugeuzwa geuzwa kama chapati.Labda waje wapinzani wa kweli watakaosimamia mambo ya msingi yanayowagusa wananchi.
Angalia vipaumbele vya wapinzani wa Tanzania.:-Bunge live,mikutano ya hadhara,safari za nje.Hapo mwananchi wa kawaida umemgusa vipi?
 
Bora kuliko Makelele ya kinafiki
Wapinzani hawana hoja zaidi ya unafiki
Leo hili baya
Kesho lile lile zuri!!
 
Sio lazima uanzishe uzi hata hiyo buku 7 unaweza kuipata bila kutoa povu hapa.
 
Kwa upinzani huu wa kutaka kupinga kila jambo ni vigumu sana kupata sympathy ya watu wanaojitambua...Makonda kawaita wanaoshukiwa kama wanahusika na matumizi au uuzaji wa madawa ya kulevya kuwahoji badala ya mtu kuja kutoa njia mbadala au kutaja anaowafahamu yy ndio kwanza analeta porojo zisizo na maana..huu upinzani ni ngumu kuaminiwa kama unaweza kuleta mabadiliko tunayoyahitaji

Tundu Lissu unajiaibisha mkuu
 
Tatizo si chama tawala wala wapinzani bali ni umaskini wa kipato, kufungwa kwa kisingizio cha uchochezi, kabambikiziwa kodi kwenye biashara, kufukuzwa kazi bila mpangilio nk.
 
Vyama vya siasa vyenye wanasheria na vinavyopewa ruzuku vinashindwaje kufungua kesi Mahakamu Kuu kuhoji uhalali wa amri/katazo hili?

Mfano.Mbona CUF wamefungua kesi Mahakamani kupinga namna ruzuku ya chama hicho ilivyotolewa?

Unajua kuna tofauti kubwa sana ya kujaribu kwenda Mahakamani kupinga amri hii na kutokwenda kabisa licha ya watu fulani kuonekana wao wako juu ya sheria?

Niwambie tu.Siku tukilalamika,hawa jamaa watatubeza/watatuhoji mbele ya wananchi mbona hamkwenda Mahakamani kama mliona amri hiyo sio sahihi?

Tena hawataishia hapo tu bali watatubeza mbona mlienda Mahakamani kupinga zuio la kukaa mita 200 wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015?Wataongeza na mfano mwingiene wa CUF kufungua kesi kuhusu maswla ya ruzuku,n.k.

Sasa jiulize hapo mwananchi wa kawaida wa kule kijijini kwenu na hata baadhi ya wananchi wa mijini wasiofuatulia siasa za nchi hii, watamuamini nani hapo?
 
Back
Top Bottom