Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?

Sawa nimekulewa, pia katiba nimeisoma.

Msimamo upo palepale, raisi ana mamlaka ya kudhibiti matumizi ya fedha zinazokusanywa kupitia kodi na vyanzo vingine.

Je nawe ni mmoja wa wale wanaolilia sana hizi safari?

Hakuna anaekuzuia kung'ang'ania msimamo ambao unasimama kwenye hoja, ili mradi unaungwa mkono na katiba/sheria lakini sio mipasho.
 
acheni unywanywa. hivi unavokurupuka kuongea shudu na mapovu mengi yamekutokoka kuwa JPM dictator una akili au we ni ku***ma. kama rais anaongoza muhimili mmoja tu basi tungekuwa tunapiga kura mojamoja ya kumchagua kiongozi wa,muhimili mmoja kwanza. acha kufikiri kwa kutumia nyuma wewe. haya amekataza na amri imetolewa. kama kuna anaejiona kaonewa basi akalalamike anapoona patatengua amri ya rais.
Huyu nae kachangia!!! CCM imeliua taifa...Sasa wewe mijadala ya kawaida tu unaporomosha mitusi hovyo, itakuwaje kwa mjadala unaohitaji kutumia akili za ziada?
 
Mimi nimeshangaa kwamba hadi wabunge waombe ruksa?
na waseme safari zao zina manufaa gani kwa taifa?

ina maana hata safari binafsi now sio ruksa?

Ningependa kuwepo na utaratibu..na sio ruksa
mtu akitaka safari yake binafsi aambiwe utaratibu ukoje hasa kama hatumii pesa ya serikali
aufuate.....otherwise tupo China ya Mao.....
Hivi Zenji wanaendelea kupasua anga?
 
Wanabodi,

Naomba kuanza na angalizo: Ukosoaji wowote, utaofanywa kwa kinachofanywa na serikali yetu, kama unatolewa in good faith, kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, huu ni ukosoaji mzuri na ni very heathy kwa serikali yoyote yenye nia ya dhati ya kufuata katiba na kuheshimu utawala wa sheria!, kinyume cha hapo ni udikiteta!.

Kitendo cha Mkuu mmoja wa mihimili ya dola, kuingilia haki, uhuru na mamlaka za mihimili mingine, sio kukiuka ile kanuni ya Checks and Balances and The Separation of Powers?!.

Nimehamasika Kuanzisha uzi huu, kufuatia mjadala wa ami ya rais kuzuia safari za nje, pia imewakumba watumishi wa bunge na watumishi wa mahakama!.


Mkuu Mahesabu hapa umeongea jambo la maana sana!, angalia nilivyowajibu hawa watu!.







Sio kila anayelipwa na fedha za umma ni mtumishi wa serikali!, hata vyama, watumishi wote wa vyama vya siasa, kikiwemo Chadema, wanalipwa kwa fedha za umma kupitia ruzuku, hawa sio watumishi wa umma!.

Kuna kanuni za uendeshaji wa serikali zote dunia nzima, ambapo kuna mihimili mitatu, seikali bunge na mahakama!, rais wa nchi ni mkuu wa mhimili mmoja tuu wa serikali, mkuu wa bunge ni spika na mkuu wa mahakama ni Jaji Mkuu!. Kitendo cha rais wa nchi kutoa amri ya kutosafiri kwa watumishi wa bunge na mahakama bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi ni rais kuingilia uhuu na madaraka ya vyombo hivi, huku ni kwenda kinyume cha utawala bora!, mimi nakuita ni sehemu tuu ya udikiteta wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli!, kitendo cha watu wanaojua the principle of separation of powers, hawakupaswa kulinyamazia hili!.

Kwa vile katazo la rais kuzui safari za nje bila kibali, limetolewa kwa nia njema ili kuzuia safari za nje zisizo na manufaa kwa taifa, rais alipaswa kuwaita Spika na Jaji Mkuu, ili spika na yeye atoe amri kama hiyo kwa wabunge na watumishi wa bunge kuomba kibali kwa Spika kupitia kwa Katibu wa Bunge, na watumishi wa mahakama, kuomba kibali kwa Jaji Mkuu kupitia kwa Msajili wa Mahakama ili ami ya rais iwahusu watumishi wa serikali tuu ikiwa ni seikali kuu na serikali za mitaa. Wabunge wapate vibali ofisi ya bunge na watumishi wa mahakama wapate vibali vya mahakama ili kuepusha kuingilia majukumu kati ya mihimili hii!.

Naomba kuwasilisha.

Heri ya Mwaka Mpya.
Pasco

Kuheshimu separation of power ni muhimu but at whose expense? Kama wabunge wakitaka kusafiri kwa gharama zao kisha serikali ikawaingilia kati, hapo tutawatetea. Lakini kama wanataka separation of power, yet hawataki separation of responsibilities, then acha serikali iwakalie kooni. By the way, when was the last time tumepewa taarifa za ufanisi wa ziara za wabunge huko nje?
 
Tuwekeeni hilo katazo, naona wengi wanachangia bila kufahamu agizo lile lilisema nini. Tusijadili kwa kukisia tujadili na facts.

BTW JPM haendi kokte kule atawanyoosha tu hawa wezi wa kisasa ambao walifikiri Tanzania ni shamba la bibi.
 
Kuheshimu separation of power ni muhimu but at whose expense? Kama wabunge wakitaka kusafiri kwa gharama zao kisha serikali ikawaingilia kati, hapo tutawatetea. Lakini kama wanataka separation of power, yet hawataki separation of responsibilities, then acha serikali iwakalie kooni. By the way, when was the last time tumepewa taarifa za ufanisi wa ziara za wabunge huko nje?


Mlalahoi upo, long time sijaona michango yako. Naona tunapishana tu humu JF
 
Taarifa yenyewe hii hapa:

12227836_899791443445832_1545951304086428184_n.jpg

Rais Magufuli akifanya kikao na makatibu wakuu

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli leo asubuhi katika Ikulu ya Dar es Salaam amefanya kikao na Makatibu wakuu, Manaibu Makatibu wakuu, Gavana wa Benki Kuu Prof. Benno Ndulu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ili kutoa uelekeo wa Serikali anayoitaka mara baada ya kuapishwa.

“Nataka Serikali iendelee kwa nguvu zote na katika kutekeleza dhana ya ‘HAPA KAZI TU’ na viongozi kuzingatia na kukumbuka ahadi nilizotoa ili zianze kuonekana na kufanyiwa kazi mara moja” Rais Magufuli amesema.

Katika Kikao chake, Rais ametoa mwongozo na kusisitizia kuwa ni lazima kila mtendaji Serikalini kuuzingatia, kufuata sheria na taratibu ili taifa lisonge mbele kwa ufanisi zaidi.

Katika kikao hicho Rais ameelekeza mambo kadhaa ambayo watendaji hao wanapaswa kuyasimamia, kuyawekea mikakati na kuyapanga vizuri ili atakapo teua Baraza lake la Mawaziri mambo hayo yawe tayari ili Mawaziri watakaoteuliwa waweze kuyasimamia bila kukosa.

Mambo hayo muhimu ni kama ifuatavyo:

Kuanzia mwezi Januari mwaka 2016, wanafunzi wote wanaoanza shule watasoma bure bila kulipa ada, Katika jambo hili, Rais amewataka watendaji kuanza kuliwekea mikakati tayari kwa utekelezaji
Suala la mikopo ya wanafunzi nalo lifanyiwe kazi na mipango yake ikamilike kwa ajili ya utekelezaji mzuri Zaidi

Amefuta safari zote za nje ya nchi kuanzia leo hadi hapo atakapolitolea suala hilo maamuzi mengine na kueleza kuwa shughuli zote zinazotakiwa kufanywa nje ya nchi zifanywe na kusimamiwa na mabalozi wa Tanzania wanaowakilisha nchi huko nje.

Pengine patokee jambo la dharura sana na hata hilo lazima kibali kitolewe na Rais au Katibu Mkuu Kiongozi. Badala yake Rais amewataka watendaji hao kufanya zaidi ziara za kwenda vijijini ili kuzijua na kutatua kero za wananchi wa Tanzania.

Katika Kikao hicho, Rais amemtaka Kamishna wa TRA, Ndugu Rished Bade kusimamia kwa makini zoezi la ukusanyaji wa mapato nchini na kuhakikisha kero ndogo ndogo kwa wananchi lianze kutekelezwa kama alivyo ahidi kwa kufanyiwa kazi mapema zaidi.

Rais ameitaka TRA kukusanya mapato hayo kutoka kwa wafanya biashara wakubwa zaidi na wale wanaokwepa kodi bila kuogopa mtu wala taasisi yoyote hapa Tanzania na kusisitiza kuwa katika Serikali hii wa kutoa maamuzi vinginevyo zaidi ya haya ni yeye Rais ama Makamu wake.
Rais Magufuli pia ameagiza usimamizi katika suala la manunuzi ambalo limekuwa likitumika vibaya na kuwa mwanya wa kuibia Serikali kwa watu kuongeza bei ya vitu hata kama ni vya bei ndogo kabisa katika jamii.

“Ikitokea suala hilo likagundulika kwa watu kuongeza bei ya vitu, watendaji watawajibishwa mara moja”. Rais amesema, na kuwataka watendaji hao kufanya kazi zao kwa kuzingatia Sheria na taratibu zilizopo na kuzingatia maadili mema ya kazi.

………………………MWISHO……………………
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
7 Novemba, 2015
 
Kasome Katiba acha kuweka Hisia. Wajua kuwa Bunge laweza kumng'oa Rais? We umeona uwezo wa Rais kulivunja Bunge ila hujaona Kuwa Bunge lina Uwezo wa Kumu impeach Rais. Not every Tom Harry n Dick will understand this. Hizi ni taaluma za watu. Kukusaidia tu, tafuta,soma kuhusu Parliamentary Supremacy, Separation of Powers, Checks n Balance kisha urudi (though it'll take you some months to be deep on those areas).
Serikali katika Dola ina majukumu yake na Mipaka yake, sawa na Bunge katika Dola na Mahakama katika Dola. Ni jukumu la Serikali kukusanya na kusimamia matumizi ya Kodi za Wananchi, je wajua juu yake nani anamsimamia Serikali? Mbona hili mashabiki wa Magufuli mnalikwepa? Hamuoni mnapotosha maana halisi ya Dola? Mnajenga utamaduni wa kila mtu kudhani kuwa muhimili fulani ni Superior kuliko mingine, that is totally wrong. Mihimili yote ni SAWA na INATEGEMEANA. Ndio maana Rais anamteua Jaji, ila Rais naye huapishwa kuwa Rais na Jaji,tofauti na hivyo hakuna kitu. Rais anaweza kulivunja Bunge, na Bunge laweza Kumuondoa Rais. Bunge linatunga Sheria, anayetafsiri ni Mahakama. So punguzeni Ushabiki, leteni Hoja zenye backup ya Authorities.

Hatuzungumzii nani ni zaidi ya mwenzake. Nilichosema ni kuwa ibara ya 34(3) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa mamlaka rais kufanya jambo lolote kwa maslahi ya taifa na hakuna chombo kingine chochote kilicho juu yake. Kwa hiyo akisimamia rasilmali zetu pamoja na mapato na matumizi ya serikali pamoja na kuthibiti nidhamu tusilalamike kwa kuwa wote tunakubaliana kuwa nchi ilikuwa inakwenda hovyo.
 
".....mambo yote ya muungano na ya tanzania bara yatakua chini ya rais.."
Hivi unaijua separationa of power na malengo yake.
Unaijua historia ya separationa of power??

Ukitaka vitu vyote viwe chini ya rais
Kwa maana ya serikali bunge na mahakama hii sidhan km imekaa sawa

Imekaa sawa ni wewe tu hutaki. Rais ndiye anayemteua jaji mkuu na rais ndiye anayeweka sahihi muswada wowote wa sheria ndiyo uwe halali na sheria iweze kutumika, na rais ndiye anayeidhinisha matumizi yote ya bunge na mahakama pamoja na maslahi yao na hakuna aliye juu yake. Bado huelewi?
 
Katazo la Rais Kusafiri Nje ya Nchi bila Vibali: Je, Halikiuki 'Separation of Powers'?
Pasco

Kiongozi wa umma umepewa madaraka na jukumu la kuhudumia wenye nchi, hivi kweli kuwahudimia vyema ni lazima uende nje ya nchi?! Haya yalikuwa ni mazoea tu, watu kupiga hela, kufanya ufuska na kubadilisha magari na kujenga mahekalu kukicha, sasa JPM kabana, watu wanalilia hata kuthubuti kuuliza haya maswali... inashangaza kusikia kwenye vyombo vya habari eti kiongozi kupeleka maombi ya kusafiri nje ya nchi MARA TANO?!
Tulikuwa tunamalizwa na hawa walafi..
 
Imekaa sawa ni wewe tu hutaki. Rais ndiye anayemteua jaji mkuu na rais ndiye anayeweka sahihi muswada wowote wa sheria ndiyo uwe halali na sheria iweze kutumika, na rais ndiye anayeidhinisha matumizi yote ya bunge na mahakama pamoja na maslahi yao na hakuna aliye juu yake. Bado huelewi?
MKUu hujui kitu its better ukae kimya hivi vitu hujui better uulize
 
udikteta wake si ndo tunaupenda..yaani kama vp wabunge awatimue watoke mjn warudi kwenye ofisi zao za mikoani..na wasaini daftari la mahudhurio ili washughulikie shida za wananchi...maana wakiupata ubunge wanakimbilia dar ...huo ni utoro ....
 
Back
Top Bottom