Katanga kama Zanzibar tu kule DRC

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Katanga ni Provence kutoka DRC ambalo lina area ya 497000 km2, Population ya milioni 7, capital city Lubumbashi, lugha yao Kiswahili na Kifaransa.

Hii katanga ndo kumetokea viongozi wengi wa DRC kama Lorent Kabila, Joseph Kabila na kwasasa Moise Katumbi anataka kugombea.

Jimbo hili limekuwa na matatizo ya kutaka kujiondoa kwenye umoja wao na DRC kwa kudai ya kwamba raia Wakongo wamekuwa na tabia ya kuwabagua na kubagua viongozi wao.

Eti walianza na Lorent Kabila wakasema sio Mkongo ni Mtanzania, Kabila akatoka akaja mtoto wake Joseph Kabila wakadai sio Mkongo ni Mnyarwanda.

Sasa hivi ni Moise Katumbi wanadai sio Mkongomani, mama yake ni raia wa Zambia na baba yake ni Muisrael. Wao wakatange wanadai katumbi ni mtoto wao na chimbuko lake ni Katanga mama yake Katumbi ni mtoto Wakatanga.

Kwa hiyo wanaomba serekali ya Kongo kama watakataa candidacy ya Moise Katumbi wao watajitenga na Kongo na kudai haki yao ya kuwa nchi huru maana Wakongomani wamekuwa na tabia ya kubagua watu wao na kuwa na mashaka na uraia wawatu wao wamechoka mateso.

Hivi unafikiri ni nini kinacho sababisha ugomvi au kutoelewana pale unapounganisha nchi mbili, hasa hasa Afrika?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lorent Kabila ni Mongomani na Joseph Kabila ni mtoto wake wa kulea (Adopt baada ya baba yake kufia katika mapambano ya kumtoa Mobutu).
Baba yake Joseph nick name joseph Kabila aliitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na joseph jina lake halisi ni Hypolite baba yake alikua aliitwa Christopher kanembe kazemberembe Mnyarwanda na allikua dereva wa Kanali wakati huo James Kabarebe wakiwa RPF msituni alinyukwa na kuacha watoto wawili Jenny na Hippolite baada ya Mobutu kuondolewa ikabdi Desire kabila amuoe mama yake Hippolite Kanambe aliitwa Marecelline ,wengine wanataja kwa jina mama SIFA ambae ndugu yake alikua james kabarebe ,akamlea na kumbadilisha jina mtoto Hippolite kuwa joseph badala la Hippolite Kanambe aka Joseph Kabila so ni pure Mnyarwanda
 
Attachments

  • kanambe.jpg
    kanambe.jpg
    15.4 KB · Views: 13
Nchi ya Katanga itaundwa na Mikoa ya Fungurume, Kolwezi, Kasai, Kasumbalesa na Mukambo.

Makao Makuu ya Nchi yatakuwa Lubumbashi.

Rais wa kwanza wa Nchi hiyo atakuwa Moise Katumbi.

Ifahamike, migodi yote mikubwa ya Congo ipo Jimbo la Katanga.

Mimi nitaishi pale pa Village Kasumbalesa karibu na Wisk ili la mgambo likilia mbio nahamia upande wa Zambia.
 
Katanga ni Provence kutoka DRC ambalo lina area ya 497000 km2, Population ya milioni 7, capital city Lubumbashi, lugha yao Kiswahili na Kifaransa.

Hii katanga ndo kumetokea viongozi wengi wa DRC kama Lorent Kabila, Joseph Kabila na kwasasa Moise Katumbi anataka kugombea.

Jimbo hili limekuwa na matatizo ya kutaka kujiondoa kwenye umoja wao na DRC kwa kudai ya kwamba raia Wakongo wamekuwa na tabia ya kuwabagua na kubagua viongozi wao.

Eti walianza na Lorent Kabila wakasema sio Mkongo ni Mtanzania, Kabila akatoka akaja mtoto wake Joseph Kabila wakadai sio Mkongo ni Mnyarwanda.

Sasa hivi ni Moise Katumbi wanadai sio Mkongomani, mama yake ni raia wa Zambia na baba yake ni Muisrael. Wao wakatange wanadai katumbi ni mtoto wao na chimbuko lake ni Katanga mama yake Katumbi ni mtoto Wakatanga.

Kwa hiyo wanaomba serekali ya Kongo kama watakataa candidacy ya Moise Katumbi wao watajitenga na Kongo na kudai haki yao ya kuwa nchi huru maana Wakongomani wamekuwa na tabia ya kubagua watu wao na kuwa na mashaka na uraia wawatu wao wamechoka mateso.

Hivi unafikiri ni nini kinacho sababisha ugomvi au kutoelewana pale unapounganisha nchi mbili, hasa hasa Afrika?

Sent using Jamii Forums mobile app
Moisemusajiografii
 
hilo linchi likubwa sana....ni sawa tu kama baadhi ya province zikijitenga na kuunda nchi kamili.
 
Back
Top Bottom