Katambi: Nchi jirani zinachochea machafuko ili tushuke kiuchumi

Katambi: Nchi jirani zinachochea machafuko ili tushuke kiuchumi

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,061
Reaction score
7,006
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema baadhi ya nchi jirani zinachochea machafuko nchini kwa lengo la kudhoofisha uchumi wa Tanzania

Vita ya kiuchumi ni kuchocheana nyie wenyewe mpigane bwana wakubwa waje kuchukua rasilimali."

"Mimi msingi wangu uko sehemu moja nasimamia ulinzi na usalama na amani ya taifa ulinzi wa raia mmoja... ulinzi wa raia na mali zao

Tumetoka kwenye corona hatukushuka kiuchumi. Tumetoka kwenye kufiwa na rais akiwa madarakani hatukushuka kiuchumi... bado tumeendelea kutoa ruzuku kwenye mbolea tumetoa ruzuku kwenye pembejeo za kilimo."


Soma Pia: Katambi: Nipo radhi kupoteza nafasi yangu lakini sitakuwa tayari kuona amani ya Taifa hili inavunjika

Kwa mfano ndugu yangu unajua kuna ndege sasa hivi... waliponda sana hizi ndege lakini ndio wa kwanza wamo mle ndani na wanalala usingizi

 
Yani ukiangàlia CV ya mawaziri wa Kenya na huyu wa kwetu na hoja zake utadhani darasa la Saba wa kijiweni vs prof wa university Yani sisi ni weupe mno ila ndio viongozi wanaotoka kwenye JAMII zetu CV zao kubwa ni kuipinga chadema tayari unapewa uwaziri.
 
Mda unavyozidi kwenda mdomo wake watu watajua mpaka koromeo lake
 
Katambi amekuwa boya kweli, yaani ccm imeahindwa kazi wewe unasingizia nchi jirani. By the way, mbona wanajeshi wa kiganda wanajivuna sana kwamba mliwaleta wakauwa watanzania via kutisha. Useless. Mtakosana na Kenya si muda mrefu, na Kenya ni mafundi wa kuharibu. TV zao zitaungana na watu wenu wa ndani. Naiona East African Community ikiwa imevunjika kwa kauli za akina "Kitambi" ambao ni maafsa Vipenyo ambao hawajui diplomasia. Wanaropoka tu
 
😂😂😂😂
😂😂😂😂
😂😂😂😂
😂😂😂😂
 
Yaani watu kama hawa wanalitia aibu na kulifedhehesha sana Taifa. Imekuwa ni Serikali ya majungu na unbeya wa ajabu.

Kama ana uhakika na ana ushahidi wa anachokizungumza, azitaje hizo nchi, na aseme hizo nchi zimefanya nini dhidi ya Tanzania. La sivyo afunge domo lake baya, asituharibie mahusiano na nchi majirani.
 
Back
Top Bottom