Katambi amepotoka, anahitaji toba

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,499
86,037
Naibu Waziri anayehusika na mambo ya Ajira sijui na Nini vile, amejitokeza na kuwalaumu vijana wenzake kuwa ni walalamishi na wanachagua Ajira! Sina tatizo na Hilo ila tatizo langu ni wapi zilipo Ajira ambazo vijana walipewa wakazigomea?

Ni ujinga na kujilisha upepo kuona au kuwadharau vijana ambao Leo hii yeye akiondoshwa hapo hatakua na Cha kufanya.

Kuna PhD holder alikua RC Morogoro, alivyotumbuliwa akaanza kulalamika kuwa family nzima inategemea yeye! Sasa huyo ni PhD holder, je hali ikoje kwa vijana? Ni kweli tuna vijana wavivu?

Kuna vijana walikua wanashinda ONLINE wanafanya kazi mbalimbali ONLINE na walikua wanalipwa vizuri tu, akatokea Mpuuzi huko huko CCM akasema hakuna kufanya malipo kwa PayPal sijui na Nini Ile. Vijana wengi Ajira zikafa.

Hawajapona vizuri akatokea kichaa mwingine akaongeza Bei ya bundle kwa 50%. Yaani wakati ulimwengu unapunguza gharama za bundle Tanzania wanaongeza gharama Kisha anatokea mwendawazimu mmoja anawalaumu vijana. Dah!

 
Siasa kwa Tanzania ni ajira sio. Siku akikosa ajira yake akili zitarudi.

Vijana wanapambana pamoja na vikwazo wanavyopata, Yeye angelenga kuwatia moyo vijana wapambanaji na kuboresha mazingira ya kuwapa support sio kuja na kauli mbofu mbofu.
 
Back
Top Bottom