Chama cha Demokrasia na maendeleo(CHADEMA) Mkoani Njombe kimeanza mikutano yake ya kata kwa kata kwa lengo la kujenga chama ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wake.
Chama hicho ambacho kimeanza shughuli zake rasmi wiki iliyopita pia kupitia mikutano hiyo ina elimisha wananchi hao namna ya kuipata katiba mpya ambayo itazingatia matakwa na mahitaji yao na si matakwa ya wachache wenye nia ya kulihujumu Taifa.
Hatua hii imekuwa ni msumari mkali sana kwa chama cha Mapinduzi(CCM) ambao wamekuwa wakihaha huku na huko ili kuzuia watu wasihudhurie mikutano hiyo kwa kuhofia wananchi kukihama chama chao hivyo kuwahonga vijicent kidogo huku wengine wakitishiwa kufukuzwa kwenye vibanda vyao vya biashara.
Wakitoa kero zao wanawake wa kata hiyo kwa mgeni rasmi ambaye pia ni katibu CHADEMA wa wilaya ya Njombe Bwana Alatanga Nyagawa, wanawake hao walisema ni miaka mingi sasa wanahangaika na suala la maji japo swala hilo lilikuwa ni sehemu ya ahadi ya Mbunge wao Mh Deo Sanga ali maarufu kama JAH PEOPLE.
Wananchi hawa ambao pia wapo kwenye mchakato wa kupeleka mawazo yao kwenye mabaraza ya katiba wanausubiri kwa hamu ujio wa Mwenyekiti wa chama Mhe MBOWE akiambatana na Mhe John Mnyika pamoja na Mhe Tundu Lissu ambao wanatarajia kuhutubia mjini hapo tare 22/08 siku ya alhamis wiki ijao
Jana Jumamosi CHADEMA walikuwa katika kata ya UBENA katika mji wa makambako.
Hii mbegu inayopandwa itakuja kuzaa matunda 100,1,000, 10,000 na 100,000. Natamani na kanda ya kusini wangeanza kazi hii. kwani huko watu wamelala fofofo
Mbona kama huo mkutano umeuzuliwa na viongozi wa CHADEMA wa hayo maeneo (kwangu naona kama semina elekezi kwa viongozi wa CHADEMA).
hammy D
nadhani hujanielewa vizuri, hiyo picha ya mwisho ni sehemu tu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo..
watu walikaa kwa kutawanyika sana kwa sababu ya jua na pia ukumbuke huu ni mkutano wa kata tu...
Fanya zoezi hili.
Hebu itisha mkutano wako eneo hili hili halafu tupime nguvu ya CDM na CCM ila msibebe watu kwenye makarandinga na pia msifunge biashara zao kwa sababu ya mikutano hii utapata majibu.
lakini pia usikose kushuhudia umati utakaofurika mkpokea Kamanda wa anga alhamisi wiki hii
Acha kuchanganyikiwa diwani, huu ni mkutano wa kata na hao watu unaowaona wamekuja kukiri wenyewe kuwa wametishiwa kufungiwa vibanda vyao kama watafika eneo la mkutano na hiyo ni sehemu tu ya waliohudhuria wengi wao walitawanyika kwa sababu ya jua...CCM wanaubavu wa kupata watu kama hawa bila vitisho? kuna wakati ukifika mtu mwenye busara hukubali matokeo na kurudi nyuma kujipanga
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.