Kasumba ya Usultani tuachane nayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasumba ya Usultani tuachane nayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by habi alex, Mar 29, 2012.

 1. habi alex

  habi alex Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 1, 2011
  Messages: 90
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Kwa muda mrefu nimekuwa sifurahishwi kabisa na tabia ya viongozi wa Tanzznia kuwarisisha uana siasa watoto wao. Mfano wa wanasiasa waliorithi uana siasa wa baba zao ni pamoja na Amani Abeid Karume, Husein Mwinyi, Vita Kawawa, Adamu Malima, January Makamba,....

  Napenda kutoa rai kwa Watanzania wenzangu tusikubali kuendeleza usultani wa hawa wanasiasa uchwara, wapo hapo kulinda maslahi yao binafsi na ya baba zao na ndugu zao wengine. Naamini kuwa nchi hii inao watu wengi wenye akili na uwezo wa kuongoza, na iwe mwisho na mwiko mwanasiasa kumwambukiza mtoto wake uana siasa.

  Kwa kuanzia uchaguzi wa mwaka 2015 tuwapige chini watoto wote wa vigogo wanaozani ni wao tu ndio wanaweza kuongoza.

  Aidha, wabunge wote waliokwisha tumikia wananchi kwa vipindi viwili nao iwe mwisho wao kugombea. Na tuwape fursa na wengine wakajaribu umaskini wa bingeni kama alivyosema spika Makinda. Hili litasidia kuondoa usultani katika nchi hii na kuwafanya viongozi wawe na hofu ya wananchi na hofu ya Mungu pia.

  Naomba kutoa hoja.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Naunga Mkono
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Ubovu wa mfumo huu ni kwamba mtu anapanda ngazi si kwa ujuzi na kazi yake, bali kwa jina. Hatuwezi kuendelea kwa minajili hii.

  Leo William "Le Mutuz @NYC" naye anataka kuwa mbunge wa Tanzania EAC.Huyu ngumbaru atachangia nini kule?

  Then tunashangaa nchi inagubikwa na mikataba mibovu!
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu hili la usultani litakuwa gumu kidogo hebu rejea na vyama vingine, huko ndiko kumeoza ile mbaya, tangu waasisi wa vyama hadi wajukuu watakaozaliwa wameshapangiwa nafasi zao zinawasubiri. Hakika kwa hili tusiongee manake hata majukwaani hakuna anaeligusia kwa vile ni donda ndugu kwa vyama vyote.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu nakuunga mkono asilimia 100 hii imekuwa ni tabia mbovu sana hata wakati mwingine watoto wanajitwisha madaraka ya baba zao kufanya mambo fulani tumeyaona hata kwa mtoto wa mkuu. mitoto inapelekwa marekani kwa hela za walipa kodi inarudi na kiingereza watu wanaiogopa wanaona ni misomi kama ilivyo kawaida ya nchi hii. jamani kama mtoa mada alivyosema tuitolee hi mitoto mbavuni
   
 6. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hii kitu sio ya kuijadili juu juu. Tunachotakiwa kujadili ni je hawa watoto wanaingia kwa ushawishi wao wenyewe au kwa mgongo wa baba zao? Je wanaweza kukabiliana na changamoto zinazotukabili? Hawajaingizwa kwa rushwa? Wananchi tunawakubali? Ukiangalia maisha ya kawaida ndivyo ilivyo. Mara nyingi mtoto wa dr/nurse atakuwa daktari au nurse, mtoto wa mwalimu naye. Mtoto wa enginere yuko hivo hivo. Ndo maneno aliyokua na kuyasikia ndani ya familia, obviously atakuwa influenced. Nchi nyingi maisha yako hivyo ila ugomvi unakuja pale mzazi anapolazimisha mumkubali mwanaye asiyekubalika na hana uwezo wa kuongoza. Angalia familia za kina bush, kuffor, shinawatra, odinga, bemba,khama, muluzi, rawlings,bhuto,gandhi nk. Wote ni wale wale. Utofauti ni namna mtoto anavyoingia kwenye hizo siasa. Huwa nnachukia baba au mtoto anapolazimishia kuwa kwenye uongozi na hekima za uongozi hana. Haya ndo ya kina wade, mwinyi, bongo,jk et al.
   
 7. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii kwa kweli inasikitisha sana, Hawa watoto wa viongozi hawawezi kutetea taifa hili, hawajasoma Tanzania, hawaishi na watanzania, mawazo yao sio ya kitanzania. Taifa linaangamia kupitia CCM!!
   
 8. K

  KABUKANOGE Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 20, 2012
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watanzania tumeingiwa na uvivu wa kufikiri, ukimwambia mtu tatizo, yeye anakimbilia, kusema he! mbona na kwafulani tatizo hili lipo, jamani hii maada ni muhimu sana ukisema eti wanakubalika, kwani nani hajui jinsi rushwa inavyotawala chaguzi zetu, na kutangazwa ambaye hajashinda?, jana nilichangia kuhusu huyu mtoto wa Maliccera, ila nikafokewa,

  Naomba tuwe makini sana na hii tabia ambayo sisi tunaona kuwa ni dili, wakati waarabu sasa wanapigana kwa sababu ya michezo kama hii, walianza eti wanapendwa na wananchi wakaongoza miaka zaidi ya 30, na hapohapo wakawa wanawaandaa watoto wao, may take, mchovya asali hachovyi mara maoja na tukiendelea kushabikia mambo kama haya, itakuwa mabya kwani watoto wa Kayumba, hakika hatakama watasoma hawataweza kupata nafasi hizo.

  Kuna hoja eti wanaopiga kura si babazao tu, kwani kamati za vyama vyetu siwite marafiki tu, NASISITIZA TENA NA TENA, WATANZANIA WENGI HUCHAGUA KWA KUPELEKESHWA NA NJAA NAWALA SI UTASHI WAO, na mara watakapo stuka hakika mimi naanza kuona kama giza mbele kwa Tanzania endapo tukiendelea kushangilia mambo kama haya
   
 9. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Njia pekee ya kuondokana na huu usultani ni kuipiga CCM chini! maana wao usultani ni moja ya sera zao!
   
 10. s

  sangija Senior Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli kabisa!!! hatuwez kuendelea kwa kasumba hizi za kurithishana madaraka/uongozi.Hao wanao fanya vile wanakuwa na hofu ya baadae ndo maana wanasimika watoto wao ili kuwalinda na kujiongezea maslahi wala hakuna wa kuwagusa make ni wao kwa wao,ila kama akiwa mtu tofaut lazima kama kuna sintofaham ihojiwe ama maelezo ya kina yatolewe.
   
 11. s

  sangija Senior Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sijakuelewa kabisa,unapomkataza asiliongelee hilo una maana gani?? mtu usha spot tatizo,so kinachofuata ni kukabiliana nalo ama kutafuta namna ya kulidhibiti ndo kitu alichofanya mwenzetu,so ni mchango wa mawazo kwamba tulimalizeje?? Hatuwez kuendelea hiv hiv mwisho utakuwa mbaya sana.Kwa nn iwe wao tu?? na lazima tuanze na chama tawala ili iwe mfano wa kuigwa.je ni wao tu ndo wenye uwezo wa kuongoza?? its too much!!!!!
   
 12. s

  sangija Senior Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yes,hapo umesema kweli hao ndo waanzilishi na wanaendekeza usultan wa hali ya juu,haiwezekani kabisa lazima tufanye maamuz wakt huu!!
   
Loading...