Kasoro hizi zinadhihirisha Nec haikujiandaa vizuri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kasoro hizi zinadhihirisha Nec haikujiandaa vizuri

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Nov 3, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Watanzania wengi jana walijitokeza kupigakura kuwachagua rais, wabunge na madiwani kwa amani na utulivu.
  Tunawapongeza sana wananchi kwa kujitokeza kwa wingi na kupiga kura katika mazingira ya amani na utulivu, kinyume na hali ya wasiwasi ambayo ilikuwa imejengeka kuwa

  zingetokea vurugu na uchaguzi kuvurugika.
  Pamoja na mchakato wa upigaji kura kutawaliwa na amani, zimeripotiwa kasoro nyingi ambazo zimesababisha wananchi kadhaa kushindwa kutimiza haki yao ya kikatiba ya

  kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka.
  Katika maeneo kadhaa baadhi ya wananchi walishindwa kupigakura kutokana na sababu kadhaa kubwa ikiwa ni ya kukosekana majina yao.

  Kasoro ya watu kukosa majina iliikumba karibu mikoa yote nchini na kuwalazimisha wananchi wengi kushindwa kupiga kura licha ya kuwa na shahada za kupigia kura.
  Mbali na baadhi ya wapigakura kutoona majina yao katika orodha iliyobandikwa, lakini pia

  wapo waliokuta majina yao yamebandikwa lakini bila kuwepo katika daftari ndani ya vituo.
  Aidha, zimeripotiwa habari kuwa baadhi ya vitabu vyenye orodha ya wapigakura vilipelekwa maeneo tofauti kwa mfano, mmoja wa wasimamizi wa kituo cha Kibondemaji C1, Mbagala Kizuiani, Dar es Salaam, alisema katika kituo chake walipewa kitabu cha

  Kizuiani C badala ya Kibondemaji, kitu ambacho kilisababisha malalamiko kutoka kwa wananchi.
  Hali hiyo ilisababisha malalamiko mengi kutoka kwa wananchi, ambao waliilalamikia Nec kushindwa kuitatua kasoro hiyo kabla ya uchaguzi.
  Tangu awali, Nec iliahidi kuwa wale wote wenye vitambulisho watakaoshindwa kuona majina yao wangepiga kura.

  Mkurugenzi wa Nec, Rajabu Kiravu, amekuwa akisisitiza kuwa watakaokosa majina yao, wasimamizi watawasaidia kuhakikisha wanapiga kura.
  Kasoro nyingine kubwa iliyobainika jana katika baadhi ya maeneo nchini, ni kukosekana

  kwa karatasi za kura za madiwani na kuwalazimisha baadhi ya wapiga kura majina yao kuhamishiwa katika kata nyingine na hivyo kukosa fursa ya kuwachagua madiwani badala yake wakapiga kura za urais na ubunge.

  Aidha, kuna baadhi ya masanduku yamekosewa kwa kupelekwa sehemu zisizohusika.
  Matokeo yake ni kwamba Nec imejikuta ikilazimika kuahirisha uchaguzi katika baadhi ya kata na majimbo ili uchaguzi ufanyike upya katika tarehe itakayopangwa baadaye.
  Kwa mfano, wananchi wa kata tatu mkoani Tabora walishindwa kupiga kura za madiwani

  kutokana na kutowasili kwa katarasi.
  Wapiga kura hao wa kata za Kingwa na Ibelamilundi kwa upande wa wilaya ya Uyui na Kisanga kwa wilaya ya Sikonge watapangiwa tarehe nyingine ya kupiga kura.
  Mratibu wa Uchaguzi mkoani Tabora, Liana Hasani, alisema wapiga kura hao wa kata hizo

  walishindwa kupiga kura kutokana na kutowasili kwa karatasi za wagombea udiwani kutoka nje ya nchi zilikochapishiwa.
  Majibu kama hayo sio rahisi kuaminiwa na wapigakura kwa sababu yanatolewa katuika muda usio mwafaka. Tunasema hivyo kwa kuwa suala la vifaa vya uchaguzi hususani

  karatasi tulielezwa kuwa ziliingizwa nchini muda mrefu kutoka Uingereza.
  Tunaelewa kuwa uchaguzi ni mchakato mgumu kiasi kwamba sio rahisi kutekeleza hatua zote kwa ufanisi wa asilimia mia moja. Hii ni kwa sababu sisi kama binadamu lazima ziwepo kasoro.

  Pamoja na ukweli huo, lakini kasoro nyingi zilizojitokeza jana zilikuwa kubwa na zingeweza kuepukika kama Nec ingekuwa makini zaidi wakati wa maandalizi hayo.
  Sababu kubwa ya kuanzishwa kwa Daftari la Kudumu la Wapigakura ilikuwa ni kuhakikisha kwamba mfumo wetu wa uchaguzi unaboreshwa tofauti na zamani.

  Kuwepo kwa daftari hilo kulikuwa na lengo la kuhakikisha kila mwananchi aliyejiandikisha jina lake linakuwa la kudumu katika daftari hilo na si vinginevyo.
  Kwa kuwa tayari uchaguzi umefanyika na watu kadhaa wamekosa haki yao ya kikatiba kutokana na kasoro tulizozitaja, tunaishauri Nec kuzichukulia kwa umakini mkubwa kasoro za jana ili zisijirudie katika chaguzi zijazo.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...