Kasi ya Rais Magufuli yafuta likizo TRA

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Kasi ya Rais John Magufuli kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewalazimu kufuta likizo kwa wafanyakazi wake wote ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha juu.

Wakati uongozi wa mamlaka hiyo ukifuta likizo hizo, tayari Rais Magufuli ameipongeza kwa kukusanya mapato ya zaidi ya Sh1.3 trilioni mwezi huu. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo alisema lengo ni kuhakikisha kuwa mapato zaidi yanakusanywa.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa kufutwa kwa likizo hizo kutokana na mtikisiko ulioikumba mamlaka hiyo ukiwamo wa kuibuliwa kwa ufisadi katika ukusanyaji wa mapato uliosababisha watumishi 35 kuchukuliwa hatua mbalimbali, wanane kati yao wakifikishwa mahakamani akiwamo Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki.

Wafanyakazi wa TRA wataungana na wenzao wa Tanesco ambao pia likizo zao zilifutwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa lengo la kushughulikia tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa nishati hiyo nchini.

Mkoani Kilimanjaro nako, mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla alipiga marufuku likizo za wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais Magufuli.

Msimamo wa Tucta

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Desemba 2, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Hezron Kaaya alitaka ieleweke kuwa likizo ni haki ya mfanyakazi na kama kuna mwajiri anataka kuzuia likizo hiyo, anapaswa kufanya majadiliano na mwajiriwa ili wakubaliane kulingana na taratibu za sheria zilizopo.

Chanzo:
Mwananchi
 
Poa tu ndo mpango mzima. Elimui bure haiwezi patikana kwa watu kwenda likizo wakiacha majukumu bila wa kuyashughulikia
 
Kasi ya Rais John Magufuli kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewalazimu kufuta likizo kwa wafanyakazi wake wote ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha juu.

Wakati uongozi wa mamlaka hiyo ukifuta likizo hizo, tayari Rais Magufuli ameipongeza kwa kukusanya mapato ya zaidi ya Sh1.3 trilioni mwezi huu. Mkurugenzi wa huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo alisema lengo ni kuhakikisha kuwa mapato zaidi yanakusanywa.


TRA kama wana competent HR Management, watakuwa wameamua kwa kudharau kitengo hicho. Hakuna HR professional anaweza kukubaliana na hicho kilichoamuliwa kwa kudhani kitainua ufanisi. Never on earth!. Subirini mjifunze kwa maumivu.
 
TRA kama wana competent HR Management, watakuwa wameamua kwa kudharau kitengo hicho. Hakuna HR professional anaweza kukubaliana na hicho kilichoamuliwa kwa kudhani kitainua ufanisi. Never on earth!. Subirini mjifunze kwa maumivu.


Na sidhani kuna mtu yeyeote anayetumia ufahamu wa kawaida anaweza kudhani kwamba kuwafutia likizo wafanyakazi kutaongeza ufanisi. Haya ni maajabu. Vinginevyo mtoa hoja hajaelewa kilichoamuliwa.
 
Likizo kama ni lazima isitishwe wanayohaki ya kulipwa mishahara miwili kila mwezi
 
Jamani mbona hamuelewi...likizo hazijafutwa ila wamesema wamelazimika kutokwenda likizo ili kufikia malengo ya kukusamya mapato...said hapo kuna shinda gani..wakimaliza malengo yao wataenda likizo..
 
Amri hiyo ni KUSOGEZWA MBELE TAREHE YA WAFANYAKAZI HUSIKA NA KWA SABABU MAALUM NA HAKI YA LIKIZO IKO PALEPALE KWA MFANYAKAZI YE YOTE.ILA BASI SIE TUNAONYUMBULISHA SANA HILO TAMKO TUNAONA KAMA NI DHULUMA.BALI KWA WAZALENDO WAKO TAYARI KUTEKELEZA YALE YOTE MAZURI KWA FAIDA YA NCHI HII.TUMEYATAKA MABADILIKO BASI TUWE TAYARI KIVITENDO NA SIYO BLABLA MDOMONI TU
 
Isije kuwa kama story za taifa stars eti "tutafia uwanjani' lakini sijawahi kuona wakipata matokeo mazuri wala kuchukua vikombe mbali na kuwaona 'wakifa' kweli!
Kurefresh minds ni kigezo muhimu katika kufanikisha ufanyaji wa kazi hasa za maofisini na ndio maana likizo zikawepo, sasa mtu akifanya kazi masaa yote si vichwa vitajam!?
 
sasa hizi ni kazi tu hakuna masihara hata kidogo hapa kazi tu.
 
Kwa mujibu wa sheria za kazi, likizo ni haki ya kila mfanyakazi. Kila mfanyakazi ana siku 28/yr (2.33 kila mwezi). Mwajiri atake asitake - kwenda likizo ni lazima.
 
Hajafuta likizo, mimi nadhani kuwa likizo zimesogezwa mbele.

Huu ukweli nimeupenda, huwezi ondoa haki yamtu kisheria bila fidia, kama amewafidia basi itakua sawa ila kama hakuna fidia basi wamekubaliana kuisogeza mbele kidogo wafikie lengo lao kwanza.
 
Kuna watu wana miss interprete hii kauli mbiu ya JPM, hasa watumishi wa juu wa sector za uma.
 
Ukweli na kwamba likizo hazijafutwa ila wamezisogeza mbele ili kufikia malengo yao waliyojiwekea. Likizo ni haki ya kila mwajiriwa na haiwezi ondolewa kwa kauli tu hivihivi, ila panapokua na melewana hakuna kinachoharibika.
 
Issue sio likizo kusogezwa mbele au kufutwa...issue ni lini walioshiriki upotevu wa containers2000 na zaidi watashughulikiwa?

Naibu wangu waziri wa fedha na CG Mpango tunaomba utufilisie walioshiriki upotevu wa containers2000 tafadhali, kwa sababu naona kama hili suwala linapotezewa vile
 
Back
Top Bottom