Kasi ya prof Mhongo TANESCO: Mameneja waagizwa kushughulikia luku zenye matatizo haraka

kumusoma

JF-Expert Member
Feb 3, 2014
566
889
TANESCO - MAOMBI YA SIKU ZA NYUMA YA KUFUNGIWA UMEME NA YALE YA KUBADILISHIWA LUKU ZENYE MATATIZO:

Jana Jumanne (15 Desemba 2015), Mameneja wa Kanda wa TANESCO wameagizwa na Prof Muhongo kuhakikisha kwamba ifikapo tarehe 15 Januari 2016 kazi ya kuwapatia waombaji wa umeme wa muda mrefu iwe imekamilika.

"Maombi yakubadilishiwa luku zenye matatizo yawe yameshughulikiwa ifikapo tarehe hiyo (15 Jan 2016). TANESCO lazima ibadilike au itabadilishwa," alisema Muhongo
 
Kipindi cha muhongo tanesco ilibadilika sana kiutendaji, waliopata huduma kipindi chake ni mashahidi, luku zilikuwa za kutosha na wale wa service line walifungiwa umeme ndani ya siku 14
 
Inabidi tujenge Taasisi na mashirika yanayofanya kazi kwa ufanisi wakati wote bila kujali waziri aliyeko. Waziri asiwe polisi ye asimamie utekelezaji wa sera tu..
 
Muhongo ni kiongozi mzuri sana tatizo anafanya kazi na wana siasa wanaopenda kutoa maneno yenye matumaini hata pasipo na tumaini
 
Muhongo hata kama ungekuwa ni wewe lazima ujitutumue tu kwa sasa, maana anajua anytime wenye nchi watalianzisha upya ESCROW.
 
Back
Top Bottom