Kasi ya kugufurika awamu ya 5

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
19,609
2,000
Kasi ya Kugufurika Awamu ya 5 mwaka 2016 ♂


1...Aliyeibia TRA mil 7 kwa dk 5 kwanini hajashtakiwa?

Hiyo ni sawa na Bil.6.048 Tshs kwa mwezi 1 tu sawa na Bil.72.536 kwa mwaka zinapelekwa wapi kama serikali imeshindwa kuwapa mikopo wanafunzi wanaohitaji mikopo ya Elimu ya Juu, kujenga madarasa na kuweka Madawati?


2...Tulianza na watumishi hewa, je wameisha? Waliosababisha hilo tatizo wako wapi ni akina nani? Je, ni Majina ya Watumishi hewa yako wapi? Kwanini yawe siri?


3.. Kutumbua, kumeleta tija kwa taifa au kumejenga woga na nidhamu ya kuigiza?


4... Sakata la sukari kufichwa na kuwa itakayopatikana ingegawiwa bure kwa watanzania,

Je, Ilipatikana? Iligawiwa bure? Lini wapi na walionufaika na sukari ya bure ni akina nani?


5..Bei elekezi ya sukari ya serikali ni 1800, je hapo ulipo wanauza kiasi gani leo?


6... Mbwembwe za Mawaziri kuwahi ofisini hadi kufunga geti ili kubaini wanaochelewa zimeisha lini? Je, hayakuwa maigizo?


7..Waandishi walipataje taarifa kuwa waziri atawahi kufunga geti ili wampige picha?? Au Rais atafanya ziara ya kushtukiza?


8..Ziara za kushtukiza za Mawaziri, na viongozi wengine zilizokuwa zinasheheni waandishi zimeisha kwanini? Mwakani zitajirudia? Zimekuwa na tija yoyote kwa sisi Wananchi?


9...Fedha zilizokuwa zimefichwa na wafanyabishara zimetolewa? Hatua gani imechukuliwa?


10.. Kukatika umeme ilielezwa itakuwa ndoto, hali ikoje sasa?


11..M?Mbwembwe za mahakama ya mafisadi zimeishia wapi? DK Mwakyembe amesema watuhumiwa wa ufisadi hakuna.


12.Sakata la Faru John litaishaje, na kwanini lilipewa umuhimu kuliko miili 7 ya mto ruvu na kupotea Ben Saanane?


13 Wapiga dili tulioambiwa watachukuliwa hatua kuwa walitaka kutugombanisha na Dangote wamechukuliwa hatua gani, ni akina nani?


14. Rais Magufuri alikuwa na maana gani kusema atashugulikia wapiga dili, majibu na Mafisadi wa awamu 4 na awamu zilizopita huku akijiondoa yeye na kueleza kuwa hakuna atakayemgusa mtangulizi wake Jakaya Kikwete.....alimaanisha wao hawakuwa katika awamu hizo?


15..Makonda ametatua kero ngapi katika Jiji la Dar? Bajeti ya kurusha matangazo alilipa nani kama serikali inabana matumizi?


16.Kuwa huru kwa Vyombo vya habari ni halali kwa CCM, Makonda, MAGUFURI, na serikali ila ni haramu kwa vyama vingine vya siasa.


17.Kauli yaM/Kiti wa CCM na Rais MAGUFURI akiwa katika sherehe za miaka 39 ya CCM kule Singida kuwa vyama vingine vya siasa visiwe na ndoto na katu visiwaze kushinda Uchaguzi na kushika dola sio kauli kidikteta.


18. Kuhoji maovu ya serikali na kukosoa ni haramu na uchochezi, ila kuisifu serikali kwa kila jambo ni uzalendo.


19...Mafisadi hawatungiwi sheria Kali, na faini yao ni kiduchu, na wanaokuwa kwenye system wapo wengi wanaongezewavyeo...... .eg.Muhongo in Escrow, yule aliyetumbuia TCU amepewa cheo kingine.....n.k

Ila vyombo vya habari vinavyosidia kufichua ufisadi na Mafisadi vimetungiwa sheria Kali sana kupindukia kuviziba midomo na kuvishika mikono ili visiwe vinachimbua maovu ya Mafisadi na kuwajulisha wananchi....

Kisha watawala wanajinasibu kuwa awamu ya 5 ni serikali ya wajibikaji, uzalendo, ukweli na yenye kuzingatia maadili.


20..Watanzania fyatueni watoto wengi mpendavyo, maana sasa elimu ni bure, mikopo ya elimu ipo, gharama za zimeshuka serikali Mpya inawajli Watu wake.

21. S?Serikali imejenga viwanda 3800 kwa mwaka 1 hivyo janga LA ajira linakaribia kuwa historia.


22. Mashine za kupimia magonjwa MRI na CT-Scan sio tatizo nchini maana Mh. kufanya ziara ya kushitukiza na kuahidi kushufuta kero hiyo.....akasema Tanzania ni nchi tajiri haitakiwei kukosa vitendea kazi hivyo.....Leo hata MoI hakuna hata kimoja.


23..Serikali inajali wananchi, imewajali sana wahanga wa Tetemeko la Ardhi, imekusanya rambi rambi ikazitumia kwa niaba yao.....wananchi wakaambulia kusubili hadi leo, wanafunzi wamepewa mikopo, kero Maji, umeme na afya sio taabu tena.


24...Sakata za ufisadi wa Lugumi, IPTL, Escrow na mengine mengi sio majipu ndio maana baba Jesca ameyapa kisogo.


25. Uwanja wa ndege wa Chato ni kipaumbele cha TAIFA.....mikopo ya elimu, ajira za walimu, wauguzi, Mishahara kupanda isubili ila uwanja wa ndege wa Chato ujengwe kwanza.

Kutemea mabadiriko kupitia CCM ni sawa na kutegemea bata amzae punda, Mto Msimbazi umwage Maji yake Ziwa Victoria.


Endeleeni kuisoma....CCM mbele kwa mbele....mmeipenda wenyewe.

Na;

Solomon KAMBARANGWE

01/01/2017
 

Mkoroshokigoli

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
14,605
2,000
Sukari imenikera sana,toka 1800/- had 2300/- kwa makusidi,maana price ilishatulia wamei desturb na haijashuka
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,812
2,000
Kweli mtu akiandika inabidi awe anayajua anayoyaandika.

Nimeishia namba moja, napita.

Kichekesho kwangu kwa mwandishi
 

Ihoyelo

JF-Expert Member
Apr 28, 2016
288
250
Hofu yangu ya viwanda vinavyopigiwa debe kwa sasa vitakuja kuwa mazizi ya kufugia mbuzi kama ya Morogoro
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom