Kashfa ya UDA sasa Ukaguzi kufanywa na KPMG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya UDA sasa Ukaguzi kufanywa na KPMG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 31, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 31, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Sunday, 30 October 2011 20:48 0digg

  [​IMG]Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh

  Raymond Kaminyoge
  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ameamua kukabidhi uchunguzi wa kashfa ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa Kampuni ya Kimataifa ya KPMG kutokana na ofisi yake kuwa na majukumu mengi.

  Uamuzi huo wa CAG umekuja miezi mitatu tangu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika, kumtaka afanye kazi hiyo haraka.Mkuchika alimwandikia CAG barua hiyo Agosti 13, mwaka huu akimpa kipindi cha mwezi mmoja kufanya kazi hiyo.

  Lakini, jana CAG aliliambia gazeti hili kwamba ameamua kukabidhi jukumu hilo kwa KPMG kutokana na ofisi yake kutingwa na mambo mengi na kuongeza kwamba, kampuni hiyo binafsi ilianza kazi hiyo tangu Ijumaa iliyopita na imepewa mwezi mmoja kuikamilisha.“Hiki ni kipindi cha ukaguzi, hivyo hatutakuwa na uwezo kufanya ukaguzi maalumu wa UDA na kuacha majukumu mengine,” alisema Utouh na kuongeza:

  “Tukisema tuifanye kazi hiyo wenyewe, tutaichelewesha, ndiyo maana, tumeamua tuipe kampuni ya KPMG iifanye.”

  Utouh alisema kampuni hiyo imepewa hadidu za rejea za kufanya ukaguzi huo na kuongeza kwamba, ilishaandikiwa barua za utambulisho za kufanya ukaguzi UDA.

  Bungeni

  Sakata la UDA liliibuka katika Mkutano wa Nne wa Bunge uliomalizika Agosti, mwaka huu baada ya wabunge kupinga kubinafsishwa kwa shirika hilo kwenda kwa Kampuni ya Simon Group.Baadhi ya wabunge waliwataja baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika na kutaka wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, akiwamo waziri wa zamani, Iddi Simba.

  Sakata hilo pia ndilo liliibua mvutano kati ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi na baadhi ya wabunge wa mkoa huo akidaiwa kuwashambulia kwa maneno makali.

  KUTOKA MWANANCHI
   
 2. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu jamaa amemwogopa masburi ndo maana kagawa kazi wengine wanasema nae anakajikampuni humo ndani ya uda
   
 3. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]CAG alemewa kashfa ya UDA [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Sunday, 30 October 2011 20:48 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg


  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ameamua kukabidhi uchunguzi wa kashfa ya Shirika la Usafiri Dar es Salaam (UDA) kwa Kampuni ya Kimataifa ya KPMG kutokana na ofisi yake kuwa na majukumu mengi.

  Uamuzi huo wa CAG umekuja miezi mitatu tangu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), George Mkuchika, kumtaka afanye kazi hiyo haraka.Mkuchika alimwandikia CAG barua hiyo Agosti 13, mwaka huu akimpa kipindi cha mwezi mmoja kufanya kazi hiyo.

  Lakini, jana CAG aliliambia gazeti hili kwamba ameamua kukabidhi jukumu hilo kwa KPMG kutokana na ofisi yake kutingwa na mambo mengi na kuongeza kwamba, kampuni hiyo binafsi ilianza kazi hiyo tangu Ijumaa iliyopita na imepewa mwezi mmoja kuikamilisha."Hiki ni kipindi cha ukaguzi, hivyo hatutakuwa na uwezo kufanya ukaguzi maalumu wa UDA na kuacha majukumu mengine," alisema Utouh na kuongeza:

  "Tukisema tuifanye kazi hiyo wenyewe, tutaichelewesha, ndiyo maana, tumeamua tuipe kampuni ya KPMG iifanye."

  Utouh alisema kampuni hiyo imepewa hadidu za rejea za kufanya ukaguzi huo na kuongeza kwamba, ilishaandikiwa barua za utambulisho za kufanya ukaguzi UDA.

  Bungeni

  Sakata la UDA liliibuka katika Mkutano wa Nne wa Bunge uliomalizika Agosti, mwaka huu baada ya wabunge kupinga kubinafsishwa kwa shirika hilo kwenda kwa Kampuni ya Simon Group.Baadhi ya wabunge waliwataja baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika na kutaka wawajibishwe kwa mujibu wa sheria, akiwamo waziri wa zamani, Iddi Simba.

  Sakata hilo pia ndilo liliibua mvutano kati ya Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi na baadhi ya wabunge wa mkoa huo akidaiwa kuwashambulia kwa maneno makali.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 4. k

  kayumba JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 654
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Amejifunza kwa Jairo!
   
 5. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,182
  Likes Received: 1,183
  Trophy Points: 280
  Angekodi ile iliyo ibua ya BOT
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Tenda ya kupata wakaguzi (binafsi) kutoka nje ilitolewa lini... au KPMG ni by default auditors tunaposhindwa?!
   
 7. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Mpaka wageni watukague! Wenyewe kwa wenyewe aibu
   
 8. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Stewart issue nyingine hiyo subirini invoice ndiyo mtashika vichwa
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Salam Mkuu Mwanakijiji zikufikie popote ulipo, nakutakia afya njema na uimara zaidi katika vita hivi vilivyopo mbele yetu.

  Mkuu unadhani tunaweza kupata hadidu za rejea za CAG, nadhani hii itatusaidia hasa katika kubaini uzito wa uchunguzi/ukaguzi unaotegewa kufanyika.
   
 10. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Tanzania ni nchi ya ajabu sana, watu wanafanya madudu kwa ajili ya manufaa yao binafsi badala ya kuchukuliwa hatua zifaazo, wanaundiwa tume ambazo zinatumia mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuwachunguza.

  Ifike mahali mtu akituhumiwa kwa jambo lolote awekwe pembeni ili aache wengine waendelee na kazi. Leo Tanzania ina uhaba mkubwa wa waalimu kuanzia ngazi ya shule za msingi hadi vyuo vya elimu ya juu lakini waalimu waliohitimu vyuoni tangu mwezi Juni hadi leo hawajaajiriwa kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha.

  Rais wa nchi anasafiri na halaiki ya wafanyabishara kwa fedha za walipakodi kwenda kufanya utalii nje ya nchi lakini vijana wananyimwa fedha za mikopo kwa ajili ya kulipia ada kwenye vyuo vya elimu ya juu kwa kisingizio kuwa serikali haina fedha.

  Hizo fedha za kuwalipa KPMG kuchunguza madudu yaliyofanywa na walafi fulani na kugharamia safari zisizokuwa na tija zinatoka wapi? Watanzania tuamke vinginevyo tutazikwa tukiwa hai na viongozi wanaotudanganya kila uchao.
   
 11. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Tanzania ni nchi ya wakulima na wafanyakazi, maana yake ni Tanzania ni nchi nchi ya wajanja wachache na wajinga wengi! Huu ndio urithi wa Chama chashika hatamu! Hivi jiulize kwa nini UTOH kampatia kazi nyeti kama hiyo mkaguzi kutoka nje wakati kazi hiyo ipo ndani ya uwezo wake? Huyu Utoh anaonesha hana kitu kiitwacho PERSONAL INTEGRITY(au kibiblia tunaita honest).

  Halafu hizo kashfa hata kama zikiibuliwa nje, nanai atachukuliwa hatua? Ona tume ya kumchunguza Jairo, imeishia wapi? Huyu huyu Utoh alimtetea Jairo na kumkosha hadhalani bila ya uwoga. Kweli kama serikali ikiwa na mkaguzi na mdhibiti wa mahesabu kama huyu, basi ni hatari kwa dinali na talanta zetu kutumiwa vibaya.

  Jamani , china wana adhabu ya kifo ndio wamefika pale walipo na dinali zao zinaogopwa sana kutumiwa vibaya na wansiasa, sasa sisi tunangoja nini kuweka adhabu ya kifo kwa wahujumu uchumi? KPMG haingepewa tenda na utoh kwa kuogopa adhabu ya kifo, maana huko ni kutumia tena dinali na talanta zetu vibaya!
  Kweli kufa kwa sokoine lilikuwa pigo kubwa sana kwa nchi kama Tanzania. Maana huyo mtu alikuwa na shepu ya kuwabana sana hawa watu kama kina utoh!
   
 12. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Nahisi tulishaacha kuwa wakulima na wafanyakazi. Tumekuwa wezi na wapiga madili.What the hell is this UDA Scandal?? In nut shell ni wizi mtupu!
   
Loading...