Kashfa ya Romania: Funzo kwa Rais Magufuli

X-bar

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2019
Posts
1,006
Reaction score
1,156
Kuna tatizo kubwa katika uongozi wa rais wa awamu hii. Rais anatumia vibaya madaraka yake kupuuza na "ku-dismiss" tuhuma na malalamiko ya wananchi dhidi ya watu anaowapenda na kuwateua kuwa wasaidizi wake.

Kiongozi anayepingana, kupuuza na kudharau maoni au malalamiko ya wanachi wake hudhihirisha kiburi, majivuno na ubinafsi alionao.

Kujiwekea msimamo kuwa wananchi wote ni "wajinga", bali ni yeye peke yake kama kiongozi mkuu wa nchi ndiye anayejua usahihi wa "mambo ya nchi" ni kujidanganya. Hii ndo tabia ya rais wetu.

Rais wetu mara nyingi amekuwa akifanya maamuzi yanayosigana na matakwa, maoni na mitazamo ya wananchi. Anafanya hivi si kwa bahati mbaya, bali anakusudia mambo yafuatayo;

1. Kuonesha kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi na hapangiwi la kufanya kupitia maoni na mitazamo ya watu. Alipomtumbua Nape na Mwigulu kutokana na kujaribu kuwachukulia hatua watu aliowateuwa yeye ilikuwa ni kuonesha "ukuu" wake yeye kama rais na kuwalinda wapendwa wake.

2. Kusafisha tuhuma za mtu anayempenda na kuonesha kuwa mtu huyo hana "madudu" ila tu watu "wanamchafua" kwa nia mbaya dhidi yake. Kwa mfano alipompandisha cheo Mnyeti kutoka DC na kuwa RC ilikuwa ni kuonesha kitendo chake cha kuwashawishi madiwani wa CDM wajiunge CCM kwa ahadi ya vyeo haikuwa rushwa. Mwenyekiti mpya wa Bodi ya VETA, Mtendaji Mkuu wa TPDC na Lugola wote aliwateuwa wakiwa wanakabiliwa na tuhuma za kifisadi katika katika utendaji wao.

3. Ikiwa anayelalamikiwa au kutuhumiwa ni mtu aliyemteuwa yeye, hapendi ionekane kuwa "rais alikosea" katika uteuzi wa mtu huyo. Mfano hai ni kuacha kumtumbua RC Makonda kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi kwa kujaribu kukwepa kodi ya kontena zake bandarini.

4. "Kuwaumiza roho" watu "fulani" kwavile anatambua watu hao wanachukizwa na maamuzi yake kutokana na sababu mbalimbali. Mathalani kuwateuwa wapinzani katika nafasi ambazo walistahili kupewa wana CCM, wapo wana ccm wasiofurahishwa na teuzi hizo kwa wapinzani.

Alipuuzia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola na kumteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na leo anamtumbua kwa tuhuma ya rushwa ya Romania. Wananchi hatuna zaidi ya kusema Rais ajifunze kuzingatia maoni, matakwa au malalamiko yetu katika maamuzi mbalimbali anayoyafanya. Bali katika jamii ya watu zaidj ya 50 milioni haiwezekani yeye peke yake ndo mwenye akili ya kujua jema na batili eti kwavile tu ni rais.
 
Wewe ni nani hadi Raisi wa JMTZ asikilize ushauri wako? Huo ubinafsi unaomsingizia Raisi wa JMTZ unao wewe mwenyewe, unafanya projection kwa wengine. Ulitaka Raisi afwate ushauri wa watu zaidi ya milioni 45 sasa kuna haja gani ya kuchagua wawakilishi?
 
Wewe ni nani hadi Raisi wa JMZT asikilize ushauri wako? Huo ubinafsi unaomsingizia Raisi wa JMTZ unao wewe mwenyewe, unafanya projection kwa wengine. Ulitaka Raisi afwate ushauri wa watu zaidi ya milioni 45 sasa kuna haja gani ya kuchagua wawakilishi?
Mimi si lolote bali ni mwananchi wa kawaida. Kwa maoni yangu endapo rais angezingatia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola, hasingemteua kuwa waziri na kwahiyo hasingepata usumbufu wa kufanya mabafiko madigo kwenye baraza lake la mawaziri na kusingekuwa na kashfa hii.
 
Tuhuma ziko nyingi maadamu hajashitakiwa popote na Mahakama hana kosa lolote.
 
Mimi si lolote bali ni mwananchi wa kawaida. Kwa maoni yangu endapo rais angezingatia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola, hasingemteua kuwa waziri na kwahiyo hasingepata usumbufu wa kufanya mabafiko madigo kwenye baraza lake la mawaziri na kusingekuwa na kashfa hii.
Unapoteza muda wako bure kujaribu kuwa 'rational' na mtu kama huyo unaymjibu; unless kama hujui/hujawahi kusoma anayoweka humu jamvini.
 
Mm naona aendelee kuwateua wale wenye kashfa then anawatumbua kwani mnafikiri wakiwa wasafi wapo na wanadumu atamtumbua nani? Ilkhali kwake anatafuta wananchi wamsikie amefanya nn?

Nitoe tahadhari isijekuwa kupunguza makali ya NIDA-TCRA midomoni mwa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa ufupi ni kwamba ukweli na Nondo uljlomwaga hapa.Magufuli au wasaidizi wake wakipita hapa mwambieni au ajiambie au ajitafakari kama ana thamani ana uwezo wa kuendelea kutumikia nembo ya rais?
Magu nchi imemshinda kuongoza hii kwa sababu ya chuki zake binasfi.Kangi alikuwa na kesi mahakamani,Kwa nguvu akamteuwa kuwa waziri,kisha akaamrisha DPP kufuta kesi.Sasaivi tunataka kama kangi atafikishwa kwa korti basi ahesabiwe makosa yake tangia rushwa za uchaguzi wa ccm wa ndani hadi wa nje hadi huu wa nje ya nchi.Watu kama hawa ndio hawawezi kuacha chama kingine kiingie madarakani maana lazima wakaishi uhamishoni au jela inawahusu.Kwa hiyo wako tayari hata kuua ili wasalie madarakani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi si lolote bali ni mwananchi wa kawaida. Kwa maoni yangu endapo rais angezingatia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola, hasingemteua kuwa waziri na kwahiyo hasingepata usumbufu wa kufanya mabafiko madigo kwenye baraza lake la mawaziri na kusingekuwa na kashfa hii.
Ndugu, ushauri unabaki kuwa ushauri..sio lazima auchukue..usilazimishe, sawa????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tatizo kubwa katika uongozi wa rais wa awamu hii. Rais anatumia vibaya madaraka yake kupuuza na "ku-dismiss" tuhuma na malalamiko ya wananchi dhidi ya watu anaowapenda na kuwateua kuwa wasaidizi wake.

Kiongozi anayepingana, kupuuza na kudharau maoni au malalamiko ya wanachi wake hudhihirisha kiburi, majivuno na ubinafsi alionao.

Kujiwekea msimamo kuwa wananchi wote ni "wajinga", bali ni yeye peke yake kama kiongozi mkuu wa nchi ndiye anayejua usahihi wa "mambo ya nchi" ni kujidanganya. Hii ndo tabia ya rais wetu.

Rais wetu mara nyingi amekuwa akifanya maamuzi yanayosigana na matakwa, maoni na mitazamo ya wananchi. Anafanya hivi si kwa bahati mbaya, bali anakusudia mambo yafuatayo;

1. Kuonesha kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi na hapangiwi la kufanya kupitia maoni na mitazamo ya watu. Alipomtumbua Nape na Mwigulu kutokana na kujaribu kuwachukulia hatua watu aliowateuwa yeye ilikuwa ni kuonesha "ukuu" wake yeye kama rais na kuwalinda wapendwa wake.

2. Kusafisha tuhuma za mtu anayempenda na kuonesha kuwa mtu huyo hana "madudu" ila tu watu "wanamchafua" kwa nia mbaya dhidi yake. Kwa mfano alipompandisha cheo Mnyeti kutoka DC na kuwa RC ilikuwa ni kuonesha kitendo chake cha kuwashawishi madiwani wa CDM wajiunge CCM kwa ahadi ya vyeo haikuwa rushwa. Mwenyekiti mpya wa Bodi ya VETA, Mtendaji Mkuu wa TPDC na Lugola wote aliwateuwa wakiwa wanakabiliwa na tuhuma za kifisadi katika katika utendaji wao.

3. Ikiwa anayelalamikiwa au kutuhumiwa ni mtu aliyemteuwa yeye, hapendi ionekane kuwa "rais alikosea" katika uteuzi wa mtu huyo. Mfano hai ni kuacha kumtumbua RC Makonda kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi kwa kujaribu kukwepa kodi ya kontena zake bandarini.

4. "Kuwaumiza roho" watu "fulani" kwavile anatambua watu hao wanachukizwa na maamuzi yake kutokana na sababu mbalimbali. Mathalani kuwateuwa wapinzani katika nafasi ambazo walistahili kupewa wana CCM, wapo wana ccm wasiofurahishwa na teuzi hizo kwa wapinzani.

Alipuuzia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola na kumteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na leo anamtumbua kwa tuhuma ya rushwa ya Romania. Wananchi hatuna zaidi ya kusema Rais ajifunze kuzingatia maoni, matakwa au malalamiko yetu katika maamuzi mbalimbali anayoyafanya. Bali katika jamii ya watu zaidj ya 50 milioni haiwezekani yeye peke yake ndo mwenye akili ya kujua jema na batili eti kwavile tu ni rais.
Pia kuna shida kubwa sana Wilayani Hai, Dc ana lalamikiwa kwa rushwa, kumdharau RC, na kudhalilisha wananchi. Juzi kadanganya Taifa kwamba kuna hujuma kwrnye reli, polisi wamekanusha ila kwa Mh Rais yeye anaona hizo sio shutuma..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni nani hadi Raisi wa JMTZ asikilize ushauri wako? Huo ubinafsi unaomsingizia Raisi wa JMTZ unao wewe mwenyewe, unafanya projection kwa wengine. Ulitaka Raisi afwate ushauri wa watu zaidi ya milioni 45 sasa kuna haja gani ya kuchagua wawakilishi?
Nina Hakika hujaelewa uzi huu , na kama umeelewa halafu ukajibu kijinga namna hii basi wewe bila shaka yoyote huwezi kuwa mzima
 
Kuna tatizo kubwa katika uongozi wa rais wa awamu hii. Rais anatumia vibaya madaraka yake kupuuza na "ku-dismiss" tuhuma na malalamiko ya wananchi dhidi ya watu anaowapenda na kuwateua kuwa wasaidizi wake.

Kiongozi anayepingana, kupuuza na kudharau maoni au malalamiko ya wanachi wake hudhihirisha kiburi, majivuno na ubinafsi alionao.

Kujiwekea msimamo kuwa wananchi wote ni "wajinga", bali ni yeye peke yake kama kiongozi mkuu wa nchi ndiye anayejua usahihi wa "mambo ya nchi" ni kujidanganya. Hii ndo tabia ya rais wetu.

Rais wetu mara nyingi amekuwa akifanya maamuzi yanayosigana na matakwa, maoni na mitazamo ya wananchi. Anafanya hivi si kwa bahati mbaya, bali anakusudia mambo yafuatayo;

1. Kuonesha kuwa yeye ndiye mkuu wa nchi na hapangiwi la kufanya kupitia maoni na mitazamo ya watu. Alipomtumbua Nape na Mwigulu kutokana na kujaribu kuwachukulia hatua watu aliowateuwa yeye ilikuwa ni kuonesha "ukuu" wake yeye kama rais na kuwalinda wapendwa wake.

2. Kusafisha tuhuma za mtu anayempenda na kuonesha kuwa mtu huyo hana "madudu" ila tu watu "wanamchafua" kwa nia mbaya dhidi yake. Kwa mfano alipompandisha cheo Mnyeti kutoka DC na kuwa RC ilikuwa ni kuonesha kitendo chake cha kuwashawishi madiwani wa CDM wajiunge CCM kwa ahadi ya vyeo haikuwa rushwa. Mwenyekiti mpya wa Bodi ya VETA, Mtendaji Mkuu wa TPDC na Lugola wote aliwateuwa wakiwa wanakabiliwa na tuhuma za kifisadi katika katika utendaji wao.

3. Ikiwa anayelalamikiwa au kutuhumiwa ni mtu aliyemteuwa yeye, hapendi ionekane kuwa "rais alikosea" katika uteuzi wa mtu huyo. Mfano hai ni kuacha kumtumbua RC Makonda kutokana na tuhuma za kuhujumu uchumi kwa kujaribu kukwepa kodi ya kontena zake bandarini.

4. "Kuwaumiza roho" watu "fulani" kwavile anatambua watu hao wanachukizwa na maamuzi yake kutokana na sababu mbalimbali. Mathalani kuwateuwa wapinzani katika nafasi ambazo walistahili kupewa wana CCM, wapo wana ccm wasiofurahishwa na teuzi hizo kwa wapinzani.

Alipuuzia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola na kumteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na leo anamtumbua kwa tuhuma ya rushwa ya Romania. Wananchi hatuna zaidi ya kusema Rais ajifunze kuzingatia maoni, matakwa au malalamiko yetu katika maamuzi mbalimbali anayoyafanya. Bali katika jamii ya watu zaidj ya 50 milioni haiwezekani yeye peke yake ndo mwenye akili ya kujua jema na batili eti kwavile tu ni rais.
Good thinking ''uongozi ni dhamana tu haina maana waliochini yako uwezo wao wa kufikiri ni mdogo
 
Mimi si lolote bali ni mwananchi wa kawaida. Kwa maoni yangu endapo rais angezingatia tuhuma za rushwa dhidi ya Lugola, hasingemteua kuwa waziri na kwahiyo hasingepata usumbufu wa kufanya mabafiko madigo kwenye baraza lake la mawaziri na kusingekuwa na kashfa hii.
Nakuhakikishia hiyo avatar ya mbwa hipo hapo kwa bahati mbaya.
 
Wewe ni nani hadi Raisi wa JMTZ asikilize ushauri wako? Huo ubinafsi unaomsingizia Raisi wa JMTZ unao wewe mwenyewe, unafanya projection kwa wengine. Ulitaka Raisi afwate ushauri wa watu zaidi ya milioni 45 sasa kuna haja gani ya kuchagua wawakilishi?
Aisee wewe ni mmoja Kati ya watu wajinga kupindukia hapa Duniani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom