Kashfa ya marekebisho ya mishahara zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya marekebisho ya mishahara zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizibao, Jan 7, 2012.

 1. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 740
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Hivi karibuni tu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kama ilivyoahidi chini ya serikali ya umoja kwa kitaifa,ilifanya marekebisho ya mishahara ya wafanyakazi wake likiwa lengo kuu ni kurekebisha mishahara ya wafanyakazi wa afya ili kuwavutia Madaktari(MDs) na wataalamu wengine wa kizanizbari kuwa na moyo wa kurudi ZNZ na siyo kufanya kazi T.Bara na nchi nyengine duniani.
  Na kama aliyoahidi Muheshimiwa J.Duni marekebisho hayo yalitoka karibuni tu lakini la kuchekesha na kusikitisha sana zoezi hilo liligubikwa na udanganyifu mwingi sana,kwa mfano watu waliweza kuforge vyeti vya masomo ili kuwaengezea elimu na walijitahidi kufanya hivyo kabla ya zoezi la upandishaji wa mishahara haujafanyika na zoezi hilo lilipelekea watu kuwa na mishahara mikumbwa huku elimu yao hairuhusu insuch away mfanyakazi wa kawaida tu wa hospital(mfagizi) anapokea mshara mkubwa sana kuliko mfamasia mwenye diploma huku muda wa kuingia kazini haujapishana.
  na kichekesho kingine kikubwa zaidi ni kama vile Daktari(MDs) alikuwa anapokea 400,000 kabla ya marekebisho hayo na baada ya marekebisho wakaongezewa mpaka 601,000 huku mafao yao yote yakiwa yameondoshwa.lakini kitu cha kushangaza zaidi wahasibu ambao wana certificate,diploma wanapokea mpaka 1.5Milion TSH pamoja na mafao mengine na katika SMZ kuna wahasibu zaidi ya 100 lakini bahati mbaya Madaktari (MDs) hawafiki hata 20 zanzibar nzima na miongoni wao hao basi ni ma administrators.
  Kitu cha kushangaza SUK kwa nini ilirusuhusu kitu kama hichi kitokee na nina uhakika kilichofanyika kama kimetokea kwa bahati mbaya tu bali kilifanywa kwa kukusudiwa hasa ikizingatiwa walishiriki katika zoezi hilo ni wafanyakazi wa wizara ya Fedha.Je SMZ kama ilikuwa na nia ya kweli kwa nini iliamuwa kuwadhalilisha madaktari pamoja na wafanyakazi wengine wa kada ya afya wenye degree kwa kuwapa kiwango kidogo sana cha mishahara bila ya kuzingatia elimu yao na ugumu wa kada zao huku Muhasibu mwenye diploma au hata degree anachukua karibu mara tatu ya mshahara wa Daktari.
  Na udhalilishaji huo pia umewakuta ma eng.
  Mwisho kama una mtoto wako au jamaa yako yuko secondary ZNZ basi mshauri asome masomo ya arts,na asisome ya science kwani mishahara ya waliosoma arts in everage wana mishahara mikubwa zaidi kuliko science na utamuepusha kudharauliwa na wenzake waliosoma arts kwa kusoma vitu vigumu lakini ni maskini.
   
 2. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli usemacho na una vilelezo kama gazeti la serikali kuhusu hilo bandiko lako, jibu ni kwamba hayo huwa ni matokeo ya kuhusisha kazi za taaluma na siasa.
  Kwani kwa kawaida zoezi lolote linalohusu maslahi ya watu huwa halihitaji kukurupuka bali maandalizi makini yaani (kawia ufike) ukiwa mkamilifu angalau kwa zaidi ya 65%.
   
 3. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 740
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Niliyoaandika hapo juu yote ni ya ukweli mtupu na hivi sasa ZNZ malalamiko ni hayo tu.Na usimayo ni kweli hili zoezi lilifanywa kwa kukurupuka na wajanja waka take advantage.In general ni suala la kusikitisha sana.

  kweli usemacho na una vilelezo kama gazeti la serikali kuhusu hilo bandiko lako, jibu ni kwamba hayo huwa ni matokeo ya kuhusisha kazi za taaluma na siasa.
  Kwani kwa kawaida zoezi lolote linalohusu maslahi ya watu huwa halihitaji kukurupuka bali maandalizi makini yaani (kawia ufike) ukiwa mkamilifu angalau kwa zaidi ya 65%.[/QUOTE]
   
Loading...