Kashfa ya makontena TRA tena: Ni ya Silent Ocean

Cazben

New Member
Oct 10, 2012
4
15
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi kubaini kashfa ya kontena tisa zenye namba za kulipia kodi TZDL 16-10-25830 zilizoingizwa nchini na Kampuni ya Silent Ocean Ltd ambazo zilinaswa na kitengo cha "Fast Team" cha TRA zikiwa na bidhaa mbalimbali za vipuri vya magari, viatu vya ngozi na nguo za kifahari...

Hivi bado watu wanaendelea na hii michezo?? Hawaoni juhudi za Rais wetu na namna alivyo serious na mapato hasa bandarini?

Ipo kila sababu ya kumuunga mkono Rais wetu katika kuyakabili mambo kama haya.. Waliohusika waadhibiwe tu..maana hakuna namna!
 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza uchunguzi kubaini kashfa ya kontena tisa zenye namba za kulipia kodi TZDL 16-10-25830 zilizoingizwa nchini na na Kampuni ya Silent Ocean Ltd ambazo zilinaswa na kitengo cha Fast Team TRA zikiwa na bidhaa mbalimbali za vipuri vya magari, viatu vya ngozi na nguo za kifahari...

Hivi bado watu wanaendelea na hii michezo?? Hawaoni juhudi za Rais wetu na namna alivyo serious na mapato hasa bandarini?? Ipo kila sababu ya kumuunga mkono Rais wetu katika kuyakabili mambo kama haya.. Waliohusika waadhibiwe tu..maana hakuna namna!
Nakubaliana na wewe tumuunge mkono raisi katika mambo mazuri kama kupambana na ufisadi lakini tumkosoe pia anapochezea katiba na sheria za nchi
 
Pole sana kama ulidhani ufisadi umeishia!!!

Rushwa.png


Some other large African countries have failed to improve their scores on the index. These include South Africa, Nigeria, Tanzania and Kenya.

Hapo juu ni trailer tu, sasa subiri Ripoti ya CAG!! Ndo vile tena CAG hatumbuliki kirahisi rahisi... utakuja kushangaa!!!
 
Nadhani awamu hii ccm wamejipanga kupiga pesa nyingi,maana hawaulizwi zaidi ya kubebwa ufisadi hautaisha nchi hii
 
Huwezi kupambana na ufisadi kama Nchi haiendeshwi kwa Uwazi (Transparency).

Vyombo vya kukusaidia kupambana na ufisadi cha kwanza ni BUNGE halafu kuna vyombo vya Habari.

Bunge la Tanzania lipo kwenye giza totoro. Halina meno tena. Hata Viongozi wa mhimili wa Bunge wameufyata.

Vyombo vya habari vimewekewa sheria mbovu kabisa za kuvibana.

Subiri report ya CAG itakavyo tuumbua.
 
Tuache bla bla tuseme ukweli, Tanzania ni nchi ya wapiga dili, ujanja ujanja mwiingi, hakuna uzalendo au mnaleta proganda eti Hakuna Transparency, eti hakuna Bunge LIVE, Pamoja na Bunge Live mbona nchi ilikuwa inapigwa sana.
 
Nasikia wachezaji wakuu wa huu mchezo ni hao hao waliokuwa wanatwa homshopingi senta
 
Ok kumbe hili kampuni la tajiri mtata kama......................(Refer Dume Suruali ya Mwana Fa) Litapita tu hilo tena mbele ya macho yetu
 
Back
Top Bottom