Kashfa ya Jairo: Mamilioni yarejeshwa nishati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya Jairo: Mamilioni yarejeshwa nishati

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jul 25, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Mamilioni yarejeshwa kashfa nishati
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 25 July 2011 09:10
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]

  Waandishi Wetu
  Mwananchi

  SIKU chache baada ya Ikulu kumpa kazi Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kufanya ukaguzi wa hesabu za taasisi za Wizara ya Nishati na Madini, imebainika kuwa Sh100 milioni (Tunaomba majina ya Wabunge wala rushwa waliorudisha peza hizi) kati ya 460 zilizochangwa katika kashfa ya kuwahonga wabunge ili wapitishe bajeti ya wizara hiyo, zimeanza kurejeshwa.

  Wiki iliyopita, Ikulu kupitia kwa Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo ilitangaza uamuzi huo wa kumpa kazi CAG baada ya kuibuka tuhuma hizo bungeni ambazo zilimtaja Katibu Mkuu, David Jairo kwamba alitoa dokezo kwa taasisi hizo kila moja kutoa Sh50 milioni, ili kufanikisha mpango huo.

  Katika kile kinachoonekana ni hofu, uchunguzi uliofanywa na Mwananchi umebaini hadi kufikia Jumatano, Julai 21, 2011, fedha ambazo zilikuwa zimerejeshwa kwenye akaunti ni zaidi ya Sh99 milioni, kati ya zaidi ya Sh460 zilizokuwa zimeingizwa kwenye akaunti ya Wakala wa Madini Tanzania (GST).

  Kiasi cha fedha kilichoingizwa katika akaunti hiyo ya GST namba 5051000068 kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma ni Sh460 milioni na siyo bilioni moja kama ilivyodaiwa awali. Hesabu kwamba fedha hizo zinaweza kufikia Sh1 bilioni ilitokana na barua iliyosomwa bungeni na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambayo ilikuwa ikibainisha fedha zilizoombwa ni Sh50 milioni ambazo zikizidishwa kwa idadi ya idara na taasisi 21 zilizopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini.

  "Jumatano wiki hii (iliyopita) kama Sh99 milioni zilirudishwa kwenye akaunti hiyo ya NMB," kilieleza chanzo chetu na kuongeza: "Jumamosi (Julai 16, 2011) na Jumatatu (Julai 18, 2011) akaunti inaonyesha kwamba zilitolewa fedha nyingi na hii inaleta shaka kwamba kwa nini hawa watu walichukua fedha nyingi kiasi hiki?"

  Wizara ya Nishati na Madini iliwasilisha bajeti yake bungeni Ijumaa, Julai 15, 2011 na mwelekeo wa wabunge wengi waliopata nafasi ya kuchangia hotuba hiyo ya Waziri wake, William Ngeleja walieleza wazi kwamba hawako tayari kuunga mkono bajeti hiyo kutokana na sababu mbalimbali zilizokuwa zikigusa sekta za madini na nishati na umeme.

  Mjadala huo uliendelea Jumatatu, Julai 18 na karibu wabunge wote wa CCM na upinzani walikataa kuunga mkono bajeti hiyo kiasi cha kuilazimisha Serikali kuiondoa ili kwenda kujipanga upya na sasa itarejeshwa bungeni Agosti 13, mwaka huu kwa ajili ya kupata kibali cha Bunge.

  "Kwa nini fedha hizi nyingi zilichukuliwa Jumamosi baada ya mambo ya wizara kuonekana kuwa siyo mazuri siku iliyotangulia (Ijumaa)?" Kilihoji chanzo chetu na kuongeza: "Hata haya mapesa mengine yaliyochukuliwa Jumatatu nayo yana walakini."

  Taasisi zilizotoa fedha

  Habari zaidi zilizolifikia Mwananchi zilifafanua kwamba, hadi sasa ni taasisi tatu tu ambazo zimebainika ziliingiza fedha katika akaunti hiyo ya GST kama zilivyoelekezwa kwa barua ya Katibu Mkuu, Jairo ya Juni 21, 2011.

  Hata hivyo, vyanzo hivyo, havikuwa tayari kuzitaja taasisi hizo kwa sasa kwa maelezo kwamba si wakati mwafaka kufanya hivyo, kwani uchunguzi unaweza kuvurugika.

  Matumizi ya fedha

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopo, shughuli za kibajeti ni pamoja na posho za vikao (sitting allowance), posho za kujikimu (per diem), ununuzi wa vyakula na vinywaji na gharama za mafuta kwa magari ya watumishi hao.

  Mmoja wa watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini alisema mjini Dodoma kwamba baadhi ya watumishi wenzake wamehojiwa na Takukuru na kwamba hicho ndicho chanzo cha baadhi ya fedha kurejeshwa kwenye akaunti kwani wengi wameingiwa na hofu baada ya kusimamishwa kwa Jairo.

  Mtumishi huyo pia alidokeza kuwa wahasibu wawili wa Serikali ambao wanafahamu undani wa sakata hilo wametoweka ghafla na hadi sasa hawajulikani waliko na kwamba mara kadhaa maofisa wa Takukuru wamekuwa wakiwasaka bila mafanikio.

  "Hapa viti ni vya moto, watu hawakai wala hawatulii maana huwezi kujua nani ataitwa kuhojiwa leo au kesho."

  Alisema baadhi ya watumishi wa wizara hiyo walilipwa fedha nyingi kuliko ilivyo kawaida na kwamba baadhi walikuwa wakilipwa posho ya Sh150,000 kwa kila kikao walichokuwa wakikaa mbali na fedha za kujikimu walizolipwa na taasisi zao.

  Saidia bajeti ipite
  Kuanzia Julai 2008, kila mwaka Ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Nishati na Madini imekuwa ikiandika barua kwa wakuu wa taasisi, vitengo na idara zilizoko chini yake kutaka fedha ambazo kwa namna moja au nyingine zinahusishwa na shughuli za bajeti ya Wizara kusomwa bungeni au kugharamia sherehe ambazo hufanyika baada ya kupitishwa kwa bajeti husika.

  Fedha hizo kwa mujibu wa nyaraka husika zimekuwa zikitumika kugharamia tafrija mara baada ya bajeti kupitishwa na Bunge, posho za vikao (sitting allowance), posho za kujikimu (per diem), vyakula, vinywaji na mafuta ya magari.

  Hata hivyo, mmoja wa watumishi wa idara ambazo zimekuwa vinara wa kudaiwa fedha wakati wa bajeti alisema wakati wa vikao vyote vya Bunge kila taasisi huwagharamia watumishi wake wanaokwenda Dodoma na kwamba wao huambulia chakula na chai kama kuna vikao vya pamoja vinavyowajumuisha na watumishi wa idara nyingine.

  Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR - Mageuzi) David Kafulila, juzi amesema kwamba amemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete akitaka uchunguzi utakaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Wizara ya Nishati na Madini uanzie miaka ya mitano iliyopita.

  Kafulila katika barua yake ameweka wazi kuwa anakubaliana na hatua za awali za kumchunguza Jairo lakini akapendekeza ufanyike uchunguzi mpana akisema mtindo huo si kwa mwaka huu pekee, bali hata miaka iliyopita katika wizara hiyo na nyingine nchini.

  "Napenda kupendekeza kwako kuwa suala hili lifanyiwe uchunguzi mpana kwa kuwa upana wa kashfa hii ni zaidi ya mwaka mmoja wa fedha 2011/2012, ni zaidi ya Katibu Mkuu mmoja, David Jairo na pengine ni zaidi ya wizara moja ya Nishati na Madini katika hicho kinachoelezwa kuwa ni kusaidia uwasilishaji wa bajeti," inaeleza sehemu ya barua hiyo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwa mtaji huu si rahisi kwa tatizo la umeme kwisha kwani wahusika wanaonekana kufaidika na matatizo yetu ya umeme
  sasa nimesoma kwenye gazeti wameanza mpango wa dharura wa kukabiliana na tatizo la umeme sasa unajiuliza ni dharura gani
  wakati tatizo hili linafahamika for years. huu ni usalliti mkubwa kwa watanzania kwa maofisa kuendelea kujilipa bonus za nguvu kwa
  utendaji mbovu na kibaya zaidi ni kitendo cha RAIS KIKWETE kuwakingia kifua kwamba tatizo siyo wao bali ni Ukame.
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Hawapo serious maana wabunge ndio janga lenyewe
   
 4. F

  Froida JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  inajulikana kabisa wanaiba Kwa baraka za mkuu wa nchi Dr Jakaya Mrisho Kikwete kama alituingiza mkenge kwenye IPTL na Barrick Gold atashindwa nini kumuagiza rafiki yake kipenzi David Jairo kufanya aliyofanya kwa sababu Luhanjo kumsafisha maaana yake Raisi alibariki tendo hilo hii serikali ya sasa ni hovyo hovyo kuliko wakati wowote wa historia ya nchi tunaongozwa na majini wanaofyonza rasilimali zetu
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  Hawa ndio tulidhani kwamba ni wawakilishi wa Watanzania kule bungeni na pia watetezi wa maslahi ya Tanzania na Watanzania kumbe nao wametanguliza matumbo yao! Wakishapewa rushwa kutokana na pesa za walipa kodi basi wako radhi kupitisha madudu yoyote yale bila kujali athari yake kwa nchi yetu. Hili si Bunge tukufu tena bali ni Bunge haramu.
   
 6. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Hakuna haja ya kumchunguza Jairo, the guy should be fired forthwith and then prosecuted for sabotaging the economy; huu uchunguzi ni njia ya Kikwete kutaka kumsafisha na tuhuma zinazomkabili. It is no secret that the guy is his confidant hence his reluctance to fire him irrespective of glaring evidence against him.
   
 7. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Ndio maana mimi naamini katika uchunguzi juu ya tuhuma ya rushwa ili hata hawa wabunge wawajibishwe siyo kukwepesha mambo.
   
 8. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Majina ya wabunge waliokubali bahasha hizo yangewekwa wazi halafu iwe fresh kuwahoji nawao!!!
   
 9. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  "Sisi tumeingia madarakani tumelikuta tatizo hili la umeme"
   
 10. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mafia bosses say, Three people can keep secreat if two are dead. David Jairo inaonekana hata novel hasomi. Angekuwa anasomaga novel , asingekubali kirahisi kuihusisha siri hii kubwa ya rushwa na watu wasiopungua tisini. Sasa basi serikali tunaomba majina ya wabunge waliopokea rushwa jatajwe na wao wafikishwe mahakamni. Maana wamefanya usaliti kwa sisi na mbele ya vitabu vitakafu waliapa wakiwa ofisini. Uwezo wa kujua majina yao tunao, maana Takuru wanaweza kuwafuatilia. Jamani serikali tutajiani ajina ya wala rushwa!
   
 11. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mambo kama haya yanatendeka katika mti mbichi, itakuwaje katika mti mkavu?
   
 12. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Jamani ehee nyie hamuoni nchi ilivyo na double standard za sheria.

  Hi kazi ilitakiwa ifanywe na Polisi au TAKUKURUna sio CAG.

  BTN
  Je wizara nyingine zimetumia shilingi ngapi kufanya hayo hayo.
  ?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,533
  Likes Received: 81,947
  Trophy Points: 280
  ....lakini ukifuatilia utendaji wa Serikali ya kifisadi katika kashfa mbali mbali za nyuma sidhani kama hawa Wabunge wala rushwa kuna hata mmoja atakayewajibishwa, watajaribu kila wawezalo kuhakikisha kashfa hii inapotea kimya kimya.
   
 14. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,668
  Trophy Points: 280
  Mi nasikia hasira,hii sijui serikali inangoja nini kuwashtaki hawa watu!
   
 15. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Inasikitisha tunapokuwa na wabunge walarushwa kwani hawawezi kukemea rushwa hata kidogo ndio maana Jairao kwa kuelewa laliokula ni wao alisema wabunge wetu ni ze komedi
   
 16. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  "Sina uwezo wa kujibadili kuwa wingu!" JK, 2011.
   
 17. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  We’ve got a president who is committed to get rid of corruption. He has dealt with Mr. Lowasa, Chenge and RA diligently and soon Luhanjo will follow suit. God help the Empire of Fisadi papa and w a k w e r e to go to hell.
   
 18. B

  Balozi Chriss Senior Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 154
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hizi za ufisadi wa kodi za wananchi.Tunaomba wote waliojihusisha na sakata hili wanyang'anywe nyadhifa zao.
  Nafasi zao zitajazwa tu na wazalendo waliotayari .
   
Loading...