Kashfa ya DOWANS: Chadema yamuunga mkono Kafulila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa ya DOWANS: Chadema yamuunga mkono Kafulila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 25, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Chadema yamuunga mkono Kafulila


  *Ni kuhusu hoja ya Dowans kurejeshwa bungeni
  *Lissu asema lengo kupinga kuzawadia ufisadi


  Na Jumbe Ismailly, Singida

  HOJA Binafsi ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Bw. David Kafulila
  imeungwa mkono na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ili kupinga kile walichodai ni hatua ya 'kuzawadia ufisadi.'

  Hoja hiyo inayotarajiwa kuwasilishwa katika mkutano wa pili wa bunge la 10 utakaoanza Februari 8, mwaka huu, inahusu mgawo wa umeme ikilenga kuliomba bunge liazimie kumtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ajiuzulu na kupinga kuilipa kampuni tata ya Dowans sh bilioni 94 bila suala hilo kurejea bungeni.

  Lakini Bw. Kafulila, tayari ameonya kuwa iwapo serikali itafikia uamuzi wa kuilipa Dowans haraka, kabla ya mkutano wa bunge kama alivyonukuliwa Bw. Ngeleja akisema, wigo wa hoja yake utapanuka na ataliomba bunge, kadri litakavyoona, lipige kura ya kutokuwa na imani na serikali yote.

  Msimamo wa CHADEMA kumuunga mkono Bw. Kafulila umetolewa na Mnazimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Bw. Tundu Lissu, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Singida.

  Bw. Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (CHADEMA), alisema kuwa ni wazi kwamba Watanzania wengi hawakubali kuona nchi yao maskini ikilipa sh. bilioni 94 kwa kampuni ambayo wenyewe hawajulikani, iliyoingia mkataba kwa njia zinazonuka rushwa.

  Aliongeza kuwa kuilipa itakuwa ni sawa na kuamua kuuzawadia ufisadi badala ya kuuadhibu.

  "Kuhusiana na suala la Dowans ni wazi kabisa kwamba Watanzania hawakubali nchi hii maskini ilipe sh. bilioni 94 kwa kampuni ambayo wenyewe hawajulikani, iliingia kwa njia zinazonuka rushwa rushwa na kwa hiyo kuwalipa itakuwa ni kuzawadia ufisadi badala ya kuadhibu ufisadi," alisema Bw. Lissu, ambaye kitaaluma ni mwanasheria.

  "Sasa hili suala la Dowans lazima vile vile tukalizungumzie bungeni, nafahamu kwamba Mbunge wa Kigoma Kusini, mheshimiwa David Kafulila ametoa taarifa kwamba atapeleka hoja mahsusi bungeni kuhusu hili suala la Dowans," alisema Mbunge huyo wa CHADEMA.

  Kwa mujibu wa Lissu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa CHADEMA, yeye pamoja na wenzake siyo tu watamuunga mkono katika hoja hiyo, kwa sababu ina maslahi makubwa kwa wananchi wengi, bali pia watataka nyaraka zote zinazohusu Dowans, ilivyoingia, wamiliki wake na mkataba wake viletwe bungeni ili viweze kujadiliwa huko.

  "Tutataka nyaraka zote zinazohusu hiyo kesi ya Dowans dhidi ya TANESCO na serikali ya Tanzania ziletwe vile vile bungeni ili wabunge wajiridhishe kwamba kilichofanyika ni kisafi, tufahamu wenye Dowans ni akina nani, mawakala wao Tanzania ni kina nani...

  "...Ofisi zao ziko wapi, huo mkataba walioingia na Richmond na baadaye TANESCO una uhalali gani, kesi walioipeleka dhidi ya TANESCO serikali ya Tanzania ilikuwa inadai nini, majibu ya utetezi wa TANESCO na serikali yalisemaje, majibu yaliyotolewa mpaka tukashindwa kesi yakoje," alisema mbunge huyo.

  Hata hivyo, Bw. Lissu aliweka bayana kuwa baada ya kupokea taarifa zote hizo ndipo wataangalia kama hawauzawadii ufisadi na kuonya kuwa endapo bunge litaridhika kwamba kilichotokea ni 'uharamia', watalazimika kuchukua hatua za kuwaeleza Watanzania wasikubali malipo ya Dowans.

  "Kwa sababu kama ambavyo tumezungumza siku nyingi sisi viongozi wa CHADEMA, chama chetu hatuko tayari kunyamazia ufisadi katika nchi hii kwa hiyo Dowans hatutainyamazia," alisisitiza Bw. Lissu.

  Tangu kuibuka kwake 'upya' baada ya hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Biashara (ICC), mjadala wa Dowans umeshika kasi katika duru za siasa za Tanzania, ukichukua sura mpya karibu kila siku na kujiongezea wazungumzaji wengi waliogawanyika katika makundi mawili, yenye hoja mbalimbali.

  Kundi moja linaloonekana kupinga hukumu hiyo na hatua ya serikali kutaka kuwalipa Dowans sh. bilioni 94 kama ilivyoamuriwa na ICC limekuwa likihoji uharaka unaooneshwa na mamlaka husika kulipa tuzo hiyo. Pia limehoji sababu za serikali kutotaka kutumia 'mianya' iliyopo kuweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

  Kundi hilo linalowajumuisha wananchi wa kawaida, wanazuoni wa masuala mbalimbali kama vile utawala bora na sheria, viongozi waandamizi serikalini, wanaharakati, viongozi wastaafu na vyama vya siasa vya upinzani, wamekuwa wakihoji pia uhalali wa mkataba wa Dowans, uliorithiwa kutoka Richmond, ambayo tayari ilishaelezwa kuwa ni kampuni hewa.

  Lakini pia limekuwa likihitaji wale wote waliohusika kuifikisha nchi katika hali hiyo, kupitia katika mkataba wa Richmond na TANESCO, kisha Dowans na TANESCO wachukuliwe hatua stahili za kinidhamu na kisheria.

  Wengine wamekuwa wakihitaji hoja hiyo irudishwe bungeni, ili kama kuna ukweli ambao haujulikani mpaka sasa, ukaweze kuelezwa ikiwemo viongozi wa kisiasa kujiuzulu au serikali nzima kuangushwa. Tayari Bw. Kafulila ameshasema kuwa suala la Dowans litaipotezea serikali uhalali wa kisiasa kutawala machoni mwa wananchi.

  Kundi jingine likihusisha watu wenye sifa kama wa kundi la kwanza (kikiwemo Chama Cha Mapinduzi), limekuwa likiunga mkono serikali kuilipa Dowans, likisema kuwa suala hilo ni uamuzi wa kisheria.

  Wengine wamenukuliwa wakisema kuwa iwapo serikali itakiuka, itakuwa inajipalia 'mkaa', kuwa nchi inaweza kuwekewa vikwazo na hata mali zake nje ya nchi kukamatwa.

  Mbali ya kusema kuwa serikali haiwezi kukata rufaa kupinga uamuzi wa ICC, limekuwa likisema kuwa mamlaka zinazohusika kulipa tuzo hiyo hazina njia yoyote ya kukwepa malipo hayo, bali kukabiliana na hukumu hiyoo, kisha ijifunze kwa ajili ya siku za usoni.

  [​IMG]


  1 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... wote hamna akili huyo muha mtumwa wetu mnamuunga mkono basi wote wendawazinu
  January 24, 2011 9:11 PM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  kweli JK safari hii ataona kilichomtoa paka pangoni...........................................
   
 3. Michelle

  Michelle JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 7,364
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  Sasa naona nuru ya upinzani wenye maslahi kwa Taifa,mkishirikiana na kuungana mkono kwenye issues kama hizi mbona tutafika mbali??
  Excellent move....:)
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kweli nimeamini Chadema ni itikaadi (hisia) za ukombozi wa Mtanzania.Hata kama Kafulila alitaka leta wenge dhidi ya CDM kabla ya kushtukiwa ila kwa hoja ya DOWANS anagusa hisia zetu CDM imetutendea haki wanainchi kumuunga mkono bila shaka sasa hoja imepata wasemaji makini.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Tatizo CCM jana wamesema DOWANS kutokwenda bungeni...........hii inaashria Spika ataipiga kwanja kwa kudai suala hilo ilpo mahakamani na Bunge haliwezi kuingilia uhuru wa mahakama ingawaje kuna mengi ya kuyajadili ambayo wala siyo lazima yahusiane moja kwa moja na TUZO tajwa.................
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Chadema waangalie uwezekano wa kufanya kazi na NCCR-MAGEUZI........................ila wakae mbali na CCM-B............CUF na UDP ambao ni wababaishaji na watawayumbisha sana.............................
   
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,593
  Likes Received: 4,699
  Trophy Points: 280
  Safari hii lazima kieleweke. JK hafikishi 2015 lazima tumpige chini nyama huyu
   
 8. R

  Realist Member

  #8
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 11, 2006
  Messages: 90
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hongera CDM Huu ndio ukomavu wa kisiasa, kuunga mkono mambo yenye maslahi kwa taifa hata kama yanatolewa na mbunge wa chama kingine. . .
   
 9. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  hizi habari zinanikumbusha enzi zile wakati wa ligi kuu ya tanzania bara, kulikuwana pan africa, nyota nyekundu vijana wa mtaa wa kongo, pamba ya mwanza, rtc kagera, cda dodoma,majimaji songea, bila kusahau african sports,coastal union, achilia mbali yanga na simba. lakini sasa ushabiki umeamia kwenye siasa, sasa watanzania wanasubiri ligi inayoanza feb 8. wakati wazi bingwa amesha julikana. ccm 8 upinzani 0.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri wale wote wanaounga mkono DOWANS kulipwa wakaorodheshwa kwa ajili ya kumbukumbu za miaka ijayo
  1. William Ngeleja (MB) - Waziri wa Nishati
  2. Werema (MB) - Mwanasheria Mkuu wa Serikali
  3. Mizengo Pinda (MB) - Waziri Mkuu
  4. Mngeja - Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga
  5.Rex Attorneys - Wanasheria wa Tanesco/Wizara ya Nishari
  6. Kamati Kuu ya CCM Taifa chini ya Mh. Jakaya Kikwete (Raisi wa Tanzania) na Yusuph Makamba (Katibu Mkuu CCM Taifa)
  7.
  8,
  9.
   
 11. b

  babalinda Member

  #11
  Jan 25, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  u
   
 12. a

  arasululu Senior Member

  #12
  Jan 25, 2011
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bila kumsahau chatanda na lymo
   
 13. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  bila kumsahau rostam azizi
   
 14. mchonga

  mchonga JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,250
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  safi sana
   
 15. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
   
 16. S

  Sinamatata Member

  #16
  Jan 25, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Si kufanya kazi na NCCR-MAGEUZI, bali hata wapinzani wengine wenye mwelekeo wa Mh. Kafulila. Hata kama taratibu zinaruhusu kwa wabunge wa CUF wa bara na si visiwani!!!
   
Loading...