Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 137,707
- 272,600
- Thread starter
-
- #41
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba wafanyakazi wao ni wa kiwango cha chini sana , wengi ni wale wahitimu wa hizi Training college , kama Eagle Training college etc.hakuna mtandao/company hisiwe na mapungufu ila tigo wamezidi aisee,,niliwai lala na salio la elf2 kwenye simu nikaamka asbh nna mia7
Niliwahi kupata haya matatizo na huu mtandao na mawazo yangu kiukweli yalikua ni kama ya wengi waliochangia humu ila baada ya maelezo ya kina kutoka kwa mmoja wa mtu ndani niligundua yafuatayo....na kuanzia hapo nilipunguza kulalamika pindi napokosea kufanya muhamala kimakosa.Huu ni upuuzi sana, nilishawahi mtumia mtu fedha kwa bahati mbaya akaibiwa simu kabla ya kuitoa, na sehemu aliyokuwepo hakukuwa na huduma ya kurenew sim card, hivyo akaniambia niwapigie simu wairudishe ili nimtumie kwenye no nyingine..
Niliwapigia hao jamaa simu nikawaeleza lakini wakalazimisha hadi wawasiliane naye, mimi nikawaeleza hali halisi jinsi ilivyo but walisumbua sana na mtu mwenyewe alikuwa na shida sana na pia hata kiasi nlichotuma kilikuwa kikubwa kiasi,
Ikabidi yule mtu aende mjini na ilikuwa ni mbali akarenew tu ile line, but baada ya siku kama nne!
Hapa naona tu kuna ujanja ujanja wanafanya, ikitokea uliyemtumia hatopatikana hewani tena au umekosea kutuma kwenye no ambayo haipo ni maumivi, million 2 inaweza kuwa vapour hivi hivi...
Hapa pesa inakua imezuiliwa(pending),haiko kwa mtumaji wala mpokeaji...mwenye maelezo yenye ushahidi ndie atakaepata....,kwa kawaida muongo ni rahisi kumjua ,kama alietumiwa kimakosa yupo same eneo na mtumaji wanaweza kuombwa kukutana ofisi ya karibu lakini hata kama wapo mbali hua wanaunganishwa pamoja(conference call) hapo muongo utamjuaa tuu.sasa huyu mteja akipigiwa na akiongopa kuwa "tulikuwa na makubaliano ya kulipana kwa njia ya tigo pesa " nini watafanya?
Tatizo linakuja pale Tigo wanapoweka uongo kwamba aliyetumiwa hapatikani wakati yuko hewani .Niliwahi kupata haya matatizo na huu mtandao na mawazo yangu kiukweli yalikua ni kama ya wengi waliochangia humu ila baada ya maelezo ya kina kutoka kwa mmoja wa mtu ndani niligundua yafuatayo....na kuanzia hapo nilipunguza kulalamika pindi napokosea kufanya muhamala kimakosa.
1.Sababu ya kuchelewa kurudisha pesa uliyotuma kimakosa,au kutoa kimakosa.
-kuna tabia kati yetu watanzania kupata huduma then ukamlipa mhusika kwa tigo pesa then mtu huyo huyo akaenda kupiga simu tigo kuomba zirudishwe,hapa tigo wakiamua kurudisha pesa bila kukoconfirm na receiver kampuni yao lazima iwajibike.
Eg:Mtu kalipa nauli(tax,bus) kwa tigo pesa then akishuka anapiga simu tigo kwamba alikosea,hapa tigo wakirudisha pesa bila kumchek receiver wanakua hawako sahihi.
-pia inatia mashaka kukosea kutuma hela kimakosa kwani process husika inatoa muda kuverifyy jina na number husika
2.Kuhusu kucheleweshewa pesa ili ziibwe na wafanyakazi wa tigo,hii pia sio kweli kabisa....katika taratibu za utumaji na upokeaji pesa kuna wahusika wawili tuu....mtumaji na mpokeaji(sender n receiver),endapo kuna kosa kati ya mmoja wao... Tigo wanachoweza kufanya ni either kurudisha kwa mtumaji au kuziacha kwa mpokeaji....there is no way ukai-divert pesa ya mteja into other number or channel,ndo maana unaona kuna kitu kinaitwa kumbukumbu namba....zile zinatumika kufunga na kurudisha mhumala husika uliokosewa.
NB:kwenye hizi huduma kuna changamoto ya mitandao kudelay na kuleta hasira kwa watumiaji lakini kubwa zaidi ni tabia yetu watumiaji kutokua waaminifu......hizi ni changamoto ambazo zinasababisha kwa kiasi kikubwa delays na baadae mis-interpretation ya huduma za mobile money
Swali zuri sana !sasa huyu mteja akipigiwa na akiongopa kuwa "tulikuwa na makubaliano ya kulipana kwa njia ya tigo pesa " nini watafanya?
Hivi kwanini wanaangaliwa tu ?Tigo ni jipu. Ukiweka salio na kama hujajiunga na kifurushi chochote lazima huwa wanakukata tu
Hivi kwanini wanaangaliwa tu ?
Ushauri - Tigo ijitoe kwenye mambo ya pesa , itakuja kusababisha umwagaji wa damu .Voda sijui sa hv kuna siku nilimtumia mtu kimakosa 2.5 saa 11 jioni nilikosa amani sana mana siku hiyo vimeo viliongozana ila Mungu ni mwema nikapiga simu saa moja na nusu hela ikarudi, ila juzi kuna ya tigo nimekosea toka tar 20 mpka leo naambiw nisubir masaa 24 kila siku jibu ni hilo hilo yani
Wakuu Naomba hili tuliangalie kwa jicho la tatu .
Kuna malalamiko mengi sana kuhusiana na ucheleweshaji wa kurudisha fedha za wateja zinazotumwa kwa makosa kwa watu wasiohusika .
Ukiongea na customer care unaambiwa fedha zako ziko salama na utarudishiwa ndani ya masaa 24 lakini hawarudishi hata baada ya wiki , ukiwauliza unaambiwa utaratibu ni lazima wawasiliane na yule uliyemtumia hela , na kwamba kutokupatikana kwake ndio sababu ya kuchelewesha kurudisha hela , uongo mtupu ! Maana ni kwamba wateja wote hata kama wako hewani , hakuna ofisa yeyote wa Tigo anayejishughulisha kuwapigia simu kama wanavyodai , Tatizo liko wapi ? Ni kweli kwamba baadhi ya watu wa kitengo cha fedha si waaminifu kama nilivyodokezwa na mtu wa jikoni ? Na kwamba wanasubiri baadhi ya wateja wakate tamaa ili wazipige hela zao ?
Viongozi wa TIGOPESA tupeni majibu .
NB - UZI HUU NI WA UCHUNGUZI NA UTAENDELEA KUONGEZWA NYAMA KWA KADRI TAARIFA ZINAVYOTUFIKIA .