Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 141,293
- 283,240
Kwanini wanafanya hivyo , wanakopa hela za watu kinguvu ?mkuu unatakiwa uvute subira hasa mimi nilirudishiwa baada ya mwezi na wiki tatu nlifuatilia mpaka nkachoka kila ukiwauliza wanakwambia vuta subira
Wakuu Naomba hili tuliangalie kwa jicho la tatu .
Kuna malalamiko mengi sana kuhusiana na ucheleweshaji wa kurudisha fedha za wateja zinazotumwa kwa makosa kwa watu wasiohusika .
Ukiongea na customer care unaambiwa fedha zako ziko salama na utarudishiwa ndani ya masaa 24 lakini hawarudishi hata baada ya wiki , ukiwauliza unaambiwa utaratibu ni lazima wawasiliane na yule uliyemtumia hela , na kwamba kutokupatikana kwake ndio sababu ya kuchelewesha kurudisha hela , uongo mtupu ! Maana ni kwamba wateja wote hata kama wako hewani , hakuna ofisa yeyote wa Tigo anayejishughulisha kuwapigia simu kama wanavyodai , Tatizo liko wapi ? Ni kweli kwamba baadhi ya watu wa kitengo cha fedha si waaminifu kama nilivyodokezwa na mtu wa jikoni ? Na kwamba wanasubiri baadhi ya wateja wakate tamaa ili wazipige hela zao ?
Viongozi wa TIGOPESA tupeni majibu .
NB - UZI HUU NI WA UCHUNGUZI NA UTAENDELEA KUONGEZWA NYAMA KWA KADRI TAARIFA ZINAVYOTUFIKIA .
Kwa hali kama hii kwanini wasilaumiwe ?Wanaboa sana nilikosea
Nikawapa taarifa wakasema nisubili baada ya masa a 24 hakuna majibu na Leo ni mwezi na nusu
Asante mkuu kwa ushuhuda , hivi kwanini MAMLAKA ZINAZOHUSIKA ZINAWAANGALIA TU HAWA WAHUSIKA ?Huu ni upuuzi sana, nilishawahi mtumia mtu fedha kwa bahati mbaya akaibiwa simu kabla ya kuitoa, na sehemu aliyokuwepo hakukuwa na huduma ya kurenew sim card, hivyo akaniambia niwapigie simu wairudishe ili nimtumie kwenye no nyingine..
Niliwapigia hao jamaa simu nikawaeleza lakini wakalazimisha hadi wawasiliane naye, mimi nikawaeleza hali halisi jinsi ilivyo but walisumbua sana na mtu mwenyewe alikuwa na shida sana na pia hata kiasi nlichotuma kilikuwa kikubwa kiasi,
Ikabidi yule mtu aende mjini na ilikuwa ni mbali akarenew tu ile line, but baada ya siku kama nne!
Hapa naona tu kuna ujanja ujanja wanafanya, ikitokea uliyemtumia hatopatikana hewani tena au umekosea kutuma kwenye no ambayo haipo ni maumivi, million 2 inaweza kuwa vapour hivi hivi...
Naunga mkono hoja , lakini kabla ya hilo warudishe kwanza hela za watu .Huu mtandao ungepigwa ban miezi sita tu ili wajirekebishe maana ndio kampuni ya simu inayoongoza kwa huduma mbovu kwa sasa.