KASHFA Strabarg na ujenzi DSM

KASHFA Strabarg na ujenzi DSM

[h=1]Tanzania National Roads agency (TANROADS)[/h]





































[h=1]Ongoing Projects[/h]
ongoing%20projects-page-001.jpg
ongoing%20projects-page-002.jpg
ongoing%20projects-page-003.jpg

Kwa jinsi ujenzi wa barabara ya Kimara hadi Kivukoni unavyosababisha kero na karaha kubwa kwa wakazi wa Dar Es Salaam na vitongoji vyake, ni vyema TANROADS wangetuwekea maelezo yote yanayohusu mradi huo ikiwemo siku mkataba uliposainiwa na tarehe ya kumalizika kwake. Kwenye jedwali hapo juu lenye orodha ya miradi iliyo kwenye hatua za utekelezaji ambalo liko kwenye website ya TANROADS, mradi namba 11 ambao unahusu ujenzi wa barabara ya Kimara - Kivukoni hakuna taarifa taarifa za lini mradi huo ulisainiwa na lini utakamilika.

Ni vyema pia TANROADS wakaweka bayana sababu za ujenzi wa barabara hiyo kuishia Kimara ilhal idadi kubwa ya wakazi pamoja na magari mengi hayaishii Kimara pekee bali mengi huwa yanaenda/yanatoka mikoani na nchi jirani hali inayoonesha wazi kuwa ujenzi unaofanywa kwa sasa hautaleta ufumbuzi wa tatizo la msongamano/foleni kwa barabara hiyo zaidi ya kuongeza tatizo.

Kinachoonekana katika huo mradi ni sawa na kuongeza ukubwa wa chupa huku mdomo wa chupa hiyo ukibaki kama ulivyo.
 
Tukaye hapa tule miongo wote jamani, kauli za jk bwana, ndiyo hiyo misaada.
 
Back
Top Bottom