Kashfa nzito zaibuliwa dhidi ya Ubadhirifu Bodi ya Mikopo

Kashfa nzito zaibuliwa dhidi ya Ubadhirifu Bodi ya Mikopo

Hii ni hatari, nani anapaswa kufikisha habari hizi juu? Na je watawajibishwa? Naomba mungu itungwe sheria ya kuwafilisi na kuwa funga miaka 30 mafisadi wote ila kama ningekua rais adhabu ingekua kunyongwa
 
Asante alietoa source ya hii habari kwa uzalendo wake. Habari ina mashiko na ina ushihidi wa kina. Mi ni mhanga kwani nimemaliza chuo mwaka jana 2011 nimeshaanza kukatwa toka mwaka huu mwezi wa sita.

Wakati kuna watu wana miaka mingi tu toka wamalize wala hawajaanza kukatwa. Hii inaonesha hawana kumbukumbu ya wadeni wao. Na vile vile hao watu wa mikopo ndo chanzo cha vurugu zote vyuoni. Wanachuo kutoka vyuo mbalimbali wanateseka kwa kushinda njaa, mabinti wanajiingiza kwenye rushwa ya ngono bila kupenda kisa wao. Na Mungu wa mbinguni awashughulikie wastahilivyo. Na sipati picha watakaodahiriwa mwaka huu itakuwaje maana wengi watakosa mkopo kwa kisingizio cha vipaumbele vya wa sayansi na elimu. Kumbe hela zipo ila zinatumika vibaya.

Mungu itazame kwa jicho la huruma nchi yangu.
 
Mwandishi ni kanjanja! Tumb..f zake ndo maana anasema Fedha Boys na Girls, mara sijui BaoBao Sec. School. Yaani kukaa kote huko Dar jamaa hata shule hazijui? Mi-TZ ndivyo tulivyo! Sekta ya habari imesheheni Makanjanja, magazeti yenyewe ya waganga njaa tu na kujitengenezea mazingira ya kuchukua rushwa! Eti jina tunalo, jina limehifadhiwa! Wapi? Pumbavu!! MWANAHALISI tutakulilia mpaka ukamilifu wa dahali!! Mwandishi anatishia nyau!!?
 
Majungu matupu ,nasikia kuna kigogo mmoja (jina tunalo) amepigwa chini kwa ku "foji"vyeti ndio anawachafua wenzake kuandika makala hii ya uchochezi....tunasubiri majibu ya bodi maana hata ile tume iliyoundwa mwaka jana chini ya Prof Maboko ilibaini Bodi iko sawa,na inajitahidi sana kwa kasma waliokuwa wanapata kwa mbinde toka Wizara ya Elimu na si Wizara ya Fedha!!
Acha tusubiri majibu toka kwa Bodi husika ila wanasikitika sana maana huyo kigogo alietolewa bila kufikishwa mahakamani,yatampata asiyoyatarajia maana sheria ni msumeno!........

Nadhani si busara kusema kuwa ni "majungu" tu simply kwa sababu huyo kigogo kafukuzwa. Hapo zimetoelwa data ambazo zinaweza kuwa "verified" kama ni kweli au la. Toa data mbadala kuliko kuangukia common excuse ya watz wakiwa na makosa halafu wakatuhumiwa kwa makosa hayo.
 
Nchi Dhaifu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Hivi wapi kuna afadhali ndani ya nchi yetu leo hii?
 
Asante alietoa source ya hii habari kwa uzalendo wake. Habari ina mashiko na ina ushihidi wa kina. Mi ni mhanga kwani nimemaliza chuo mwaka jana 2011 nimeshaanza kukatwa toka mwaka huu mwezi wa sita.

Wakati kuna watu wana miaka mingi tu toka wamalize wala hawajaanza kukatwa. Hii inaonesha hawana kumbukumbu ya wadeni wao. Na vile vile hao watu wa mikopo ndo chanzo cha vurugu zote vyuoni. Wanachuo kutoka vyuo mbalimbali wanateseka kwa kushinda njaa, mabinti wanajiingiza kwenye rushwa ya ngono bila kupenda kisa wao. Na Mungu wa mbinguni awashughulikie wastahilivyo. Na sipati picha watakaodahiriwa mwaka huu itakuwaje maana wengi watakosa mkopo kwa kisingizio cha vipaumbele vya wa sayansi na elimu. Kumbe hela zipo ila zinatumika vibaya.

Mungu itazame kwa jicho la huruma nchi yangu.
Ubatili mtupu,ubatili mtupu mambo yote ni ubatili (Mhu 1:2 )
 
serikali chukueni hatua kunusuru hili
bodi nzima wasimamishwe fagia wote
ianze upya. wengi niwajuao wana majumba na mali za kutisha.mkitaka ushahidi ntafuteni
mshahara wake hauendani na thamani ya mali anazomiliki
 
Hii li serikali libovu mpaka linatia hasira. ningekuwa na uwezo ningepindua hili liserikali. haya yote yanatokea na mengine mengi tuu, mabilioni kule uswisi, pesa zinaliwa kwenye halimashauri, walimu hawalipwi vizuri, madaktari shida tupu, dawa hospitali za kubabaisha, vitabu mashuleni hakuna, hapo hapo tunasamehe kodi kwenye migodi, misaada kibao kutoka nje, pesa hazionekani zinafanya nini, viongozi hawajali, wabunge wanajiongezea mishahara utadhani wao ndo wafanyakazi bora kuliko daktari au mwalimu na wengineo, aaaaaaaaarrrrrrrrrrrrrrrggggggggggggggghhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. hii ni SERIKALI AU KUNDI LA MAJAMBAZI?????

Una kila sababu ya kukasilika!!
 
Wanaafisa habari wao mjibuji wa hoja hii... Aulizwe
 
mpaka lini lakini...kila wiki tunajadili ufisadi mpya:spy:
 
Hii nchi inanitia kichefuchefu yaani kila kukicha ufisadi mara huyu kafisadì hapa huyu pale!sasa mwaka ole wao tusikie mtu anasifa lakini ananyimwa mkopo eti bajeti haitoshi,lazima tuipindue hii bodi au vp wadau?
 
Hakika ni majungu ( na masufuria pia)

Hivi karibuni kuna KOGOGO kihiyo aliumbuka ikabidi aachie ngazi. Alisema ana Mastres ya India ila akashindwa kuonyesha Cheti. Akatimuliwa. Aitea Lubambula Machunda.

Pia kuna vijana ambao wameanza kazi ya kuwa mchwa kula hela za wanafunzi nao wametolewa na wana kesi kwa Pilato.

Haikosi hawa wamwchagia taarifa hii.

Kwa mazingira yaliyopo Bodi wanachapa kazi na ni mfano wa kuigwa. Ugumu ni kwamba ni vigumu kubaini haya bila kufanta kautafiti au kusoma taarifa. Sifa za kisiasa sio rahisi kwa taasisi inayotoa hela ambazo wala haziwatoshi wahitaji.

Nawasilisha
 
Hakika ni majungu ( na masufuria pia)

Hivi karibuni kuna KOGOGO kihiyo aliumbuka ikabidi aachie ngazi. Alisema ana Masters ya India ila akashindwa kuonyesha Cheti. Akatimuliwa. Aitwa Lubambula Machunda.

Pia kuna vijana ambao wameanza kazi ya kuwa mchwa kula hela za wanafunzi nao wametolewa na wana kesi kwa Pilato.

Haikosi hawa wamechagia taarifa hii.

Kwa mazingira yaliyopo Bodi wanachapa kazi na ni mfano wa kuigwa. Ugumu ni kwamba ni vigumu kubaini haya bila kufanta kautafiti au kusoma taarifa. Sifa za kisiasa sio rahisi kwa taasisi inayotoa hela ambazo wala haziwatoshi wahitaji.

Nawasilisha
 
Ndugu zangu,

Imenibidi niingie kwenye kwenye project research fasta, maudhui ni kuchunguza aina ya laana Tanzania iliyolaaniwa. Kwa sababu najua kuwa nchi hii imelaaniwa ila tu sijui ni laana ya aina gani.

So mnisadie vyanzo mbalimbali na materials (JF ni kisima) ili nikamilishe uchunguzi wangu fasta na kuwasilisha ripoti.
NB: Gharama za project ni zangu 100%.

Shukran kwa CCM na serikali zake/yake kwa kupelekea uwepo wa mazingira na hali ya kulazimisha project yangu kuwezekana.
 
Back
Top Bottom