Kashfa nzito zaibuliwa dhidi ya Ubadhirifu Bodi ya Mikopo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa nzito zaibuliwa dhidi ya Ubadhirifu Bodi ya Mikopo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ASSASSIN, Aug 26, 2012.

 1. A

  ASSASSIN Member

  #1
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vigogo wajilipa mishahara minono, ajira kinyemela

  [​IMG] Mikopo inayopaswa kurudishwa ni Sh. bil.300/-
  [​IMG] Hadi sasa fedha zilizokusanywa ni Sh. bil. 9/- tu  Vigogo Bodi ya Mikopo (HESLB), wanakabiliwa na tuhuma nzito za ubadhilifu wa fedha kwa kujilipa mishahara minono na matumizi mabaya ya madaraka huku mmoja wao akidaiwa kuajiri ndugu zake 11 wasiokuwa na sifa.

  Nusu ya vigogo walioajiriwa katika bodi hiyo wanadaiwa kutokuwa na sifa wala vyeti stahiki kama kibali na tangazo la kazi lilivyotangazwa gazetini.

  Vigogo hao pia wanadaiwa kulipwa mishahara minono ya mamilioni ya fedha huku Bodi hiyo ikiwa haizalishi chochote.

  Chanzo chetu cha habari ndani ya bodi hiyo kimedai kuwa kigogo wa ngazi ya juu analipwa Sh. 13,875,000 yakiwemo marupurupu na posho.

  Anayefuatia analipwa Sh. 12,950,000 kwa mwezi ikiwemo posho wakati mwingine mshahara wake pamoja na posho ni Sh. 12,025,000.

  “Watumishi wanaofuata baada ya menejimenti mishahara yao inaanza Sh. 3,000,000 kwenda chini bila posho yoyote,” kilisema chanzo hicho.

  Tangu Bodi hiyo ianzishwe mwaka 2005 mikopo iliyotolewa na kupaswa kurudishwa ni Sh. bilioni 300 lakini hadi sasa fedha zilizokusanywa ni Sh. bilioni 9 tu (sawa na asilimia 3).

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, licha ya utaratibu wa sasa wa serikali wa kutaka ajira zote zitangazwe kwenye vyombo vya habari ili kutoa fursa kwa Watanzania kushindania, lakini kigogo mmoja ametoa ajira za kudumu kwa watumishi kumi (majina tunayo) bila kutangaza wala wahusika kufanyiwa usaili.

  Chanzo hicho kimesema kuwa, miezi michache iliyopita bodi hiyo ilitangaza ajira za watumishi 21 wakati kibali cha ajira kilikuwa ni nafasi 24.

  “Cha kushangaza nafasi 11 zimejazwa na ndugu wa mmoja wa vigogo hao akiwemo mtoto wake (jina tunalo) ambaye alipewa nafasi ya mwanamke (jina tunalo) aliyekuwa amefaulu nafasi hiyo, nafasi nyingine tatu (majina tunayo) wamepewa wajomba zake,” kimesema chanzo hicho.

  Chanzo hicho kimedai watumishi wamekuwa wakipandishwa vyeo kiholela bila kufuata sifa na sheria zilizopo.

  “Kwa mfano zipo nafasi kadhaa (majina tunayo) ambazo wale waliopewa hawana sifa, moja inamtaka mtu aliye na sifa na uzoefu wa usiopungua miaka mitatu na nyingine ilikuwa inahitaji mtu mwenye Uzamili (masters), yupo aliyepandishwa cheo bila ya kuwa na CPA (T) kama miongozo inavyosema,” kimebainisha.

  Aidha, chanzo kimeendelea kufichua kuwa nusu ya wakurugenzi walioajiriwa hawana sifa wala vyeti stahiki na wanaajiriwa kiudugu.
  Baadhi ya vigogo walioajiriwa wanadaiwa kupewa ajira, wakiwa hawana kiwango cha elimu kilichokuwa imetangazwa na kwamba wengine walikuwa bado wanafunzi na wengine hawakuwa na taaluma ya kazi aliyoajiriwa.

  Pia chanzo hicho kimedai kigogo wa ngazi ya juu amekuwa na matumizi mabaya ya madaraka ambapo mwaka 2010 alitumia zaidi ya Sh. milioni 50 kwa ajili ya safari nchini Zambia akiambatana na vigogo wengine wawili.

  Chanzo hicho kimesema ubadhilifu mwingine ni posho za vikao vya bodi na safari.

  Kimebainisha kuwa, malipo ya fedha za wanafunzi vyuoni hutolewa kwa mfumo wa bajeti na kwamba katika mwaka mmoja wa masomo idadi ya vikao vya bajeti HESLB huwa ni 30 au 32.

  Chanzo hicho kimesema kwa mwaka posho za vikao hivyo kutengwa kiasi cha Sh. milioni 600 na wanaopitisha bajeti hizo huwa ni wajumbe wa bodi wa kamati ya utoaji wa urejeshwaji mikopo (LARC) na menejimenti ya bodi.

  “Kamati hii ina wajumbe wasiopungua watano na wakurugenzi kumi wa bodi yaani menejimenti, kwa kila kikao mjumbe wa bodi hulipwa posho Sh. 500,000 huku wakurugenzi kumi kila mmoja hulipwa Sh. 400,000,” kimesema chanzo na kuongeza:

  “Ukijumuisha gharama zilizosalia za posho za kujikimu kwa wajumbe wanaotoka nje ya Dar es Salaam, chai na gharama nyingine kikao kimoja hugharimu Sh. milioni 20, hivyo kwa vikao 30 ni Sh. milioni 600,” kimebainisha.

  Aidha, chanzo hicho kimesema kuwa, kiwango hicho kinachotumika kwa mwaka kwa ajili ya vikao hivyo ikizidishwa mara miaka saba ya bodi hiyo kukaa madarakani ni sawa na Sh. bilioni 4.2 kwa kamati moja ya bodi.

  “Hii ni sawa na kusomesha wanafunzi wa Shahada za Sayansi ya Jamii 1,400, ila kwa makusudi menejimenti imekuwa ikiagizwa iweke vikao vingi vya LARC wakati akijua kuwa wanafunzi wanateseka vyuoni na njaa kwa urasimu huu usio na tija,” kimefafanua chanzo hicho na kuongeza:

  “Bajeti ya mwaka kwa vikao vya bodi na menejimenti ni Sh. bilioni 3 ambapo fedha hizi kama utawakopesha wanafunzi kwa mwaka jumla yao ni 1000,” kimesema.

  Aidha, chanzo hicho kimesema kuwa, katika mwaka wa masomo 2011/12 Baraza la Mawaziri kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, chini ya Waziri Shukuru Kawambwa, lilitangaza kwenye vyombo vya habari vigezo vya utoaji mikopo.

  Chanzo hicho kimesema licha ya vigezo vya utoaji mikopo kutangazwa lakini ilikiuka kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi 600 wasiostahili.

  Kimefafanua nafasi hizo zilizotolewa ni wanafunzi 45 wa mwaka wa kwanza wanaosoma shahada ya ‘Law Enforcement’ Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambao ni waajiriwa wa Jeshi la Polisi nchini.

  “Tangazo lilitoa kipaumbele kwa kozi zote za afya ya binadamu na mifugo, ualimu wa Sayansi na Hesabu. Pia uhandisi, ualimu wa Art, na kozi za Sayansi ambazo zitazingatia uwezo wa muombaji kiuchumi na asiye na sifa linganishi yaani cheti na diploma,” kimesema na kuongeza:

  “Kozi ya sayansi ya jamii, hizi si kozi za kipaumbele kwa taifa hivyo watapata fedha itakayokuwa imesalia kwa uhitaji kwa kupima mtu hali yake ya kifedha na shule ya sekondari aliyosoma na kuchukua ile gharama ya juu zaidi , ufaulu haukuwa na kigezo, mikopo isitolewe kwa mtu mwenye sifa linganishi yaani cheti/diploma au aliyeajiriwa,” sehemu ya tangazo hilo imesema.

  Chanzo hicho kimesema, wanafunzi hao ambao wengi wao wakiwa na sifa linganishi za cheti/ diploma kinyume cha mwongozo kwa mwaka huo wa masomo awali walikosa wote mikopo.

  Aidha, kimesema kuwa baadaye wanafunzi hao kupitia uongozi waliwapatia mikopo kwa njia zisizoeleweka na suala hilo lilifikishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu ambaye hakuchukua hatua zozote.

  “Wapo wanafunzi zaidi ya 100 watoto wa vigogo wenye sifa linganishi cheti/diploma wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele vyuo mbalimbali ambao mwanzoni walinyimwa mikopo na sasa wamepata kinyume cha taratibu,” kimebainisha chanzo hicho.

  Chanzo hicho kimesema kuwa, wanafunzi hao wa vigogo walisoma shule za sekondari zenye ada kubwa kati ya Shilingi milioni tatu hadi saba na kwamba huko vyuoni hawasomi kozi za vipaumbele kama tangazo lilivyoainisha.

  “Waliosoma shule za Sekondari Fedha Boys na Girls ni wanafunzi 29, Marian Girls Bagamoyo wanafunzi 41, St. Marys wanafunzi 200, Laurentine International wanafunzi 20, Baobao Sekondari wanafunzi 40, St. Francis Mbeya wanafunzi 28, Loyola high school wanafunzi 60 na waliosoma nje ya nchi wanafunzi 10,” kimebainisha chanzo hicho.

  Chanzo hicho kimetoa ubadhilifu mwingine uliofanywa na vigogo hao kuwa ni matumizi ya Sh. milioni 300 kwa ajili ya kuhonga ili kuzima zoezi la kuiwajibisha Bodi hiyo baada ya kuundwa Tume ya Rais kuichunguza.

  Katika hatua nyingine, chanzo hicho kimesema kuwa katika mwaka wa masomo 2010/11, bodi ilitangaza tenda ya 'scan' fomu za wanafunzi na kampuni iliyokuwa imeshinda ni Digital Scap na kupewa barua ya kufanya tenda hiyo lakini uongozi ulitengua maamuzi hayo na kuipa kampuni ya Koseke.

  “Hili linafahamika mpaka PPRA lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa,” kimesema.

  Pia chanzo hicho kimesema ubadhilifu mwingine ni bodi hiyo kujilipa mishahara na mikopo mikubwa ya aina mbili yenye riba ya asilimia mbili tu isiyo na uwiano na watumishi wengine.

  Jumla ya mikopo iliyotolewa kwa watu hawa 16 ni Sh. 2,560,000,000, kiukweli fedha hizi ni sawa na kutoa mikopo kwa Watanzania 853,” kimebainisha.

  Pia chanzo hicho kimesema unyanyasaji wa wafanyakazi HESLB umesababisha wafanyakazi watatu waliofukuzwa na kushinda kesi hiyo iliyokuwa mahakamani Bodi kulazimika kuwalipa fidia ya Sh milioni 300.

  Katika hali isiyo ya kawaida, chanzo hicho kimesema, toka mwaka 2005 Bodi hiyo ianzishwe mikopo iliyotolewa na inapaswa kurudishwa ni Sh. Bilioni 300 lakini hadi sasa fedha zilizokusanywa ni Sh. Bilioni 9 tu sawa na asilimia 3.

  NIPASHE ilimtafuta Mkurugenzi Mkuu wa Bodi hiyo ili kupata ufafanuzi wa madai hayo lakini ilijibiwa na mtu wa mapokezi kuwa yuko nje ya mkoa kikazi.

  Licha ya kupigiwa simu yake ya mkononi na kutumiwa ujumbe mfupi, hakupokea wala kujibu ujumbe.

  Chanzo: Nipashe - Agosti 26, 2012
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  JK mpe Mwakyembe wizara mama ya bodi ya mikopo
   
 3. k

  king roja Senior Member

  #3
  Aug 26, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duh iyo hatari na ndio maana wanatupa asilimia 20 za mkopo
   
 4. ruhi

  ruhi JF-Expert Member

  #4
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 1,409
  Likes Received: 776
  Trophy Points: 280
  kwa sasa tufaneje? na hali inazidi kua mbaya?
   
 5. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #5
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Hii li serikali libovu mpaka linatia hasira. ningekuwa na uwezo ningepindua hili liserikali. haya yote yanatokea na mengine mengi tuu, mabilioni kule uswisi, pesa zinaliwa kwenye halimashauri, walimu hawalipwi vizuri, madaktari shida tupu, dawa hospitali za kubabaisha, vitabu mashuleni hakuna, hapo hapo tunasamehe kodi kwenye migodi, misaada kibao kutoka nje, pesa hazionekani zinafanya nini, viongozi hawajali, wabunge wanajiongezea mishahara utadhani wao ndo wafanyakazi bora kuliko daktari au mwalimu na wengineo, aaaaaaaaarrrrrrrrrrrrrrrggggggggggggggghhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. hii ni SERIKALI AU KUNDI LA MAJAMBAZI?????
   
 6. p_prezdaa

  p_prezdaa JF-Expert Member

  #6
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 415
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kiliooooooooooooo, kiliooooooooooooooooooo, kiloooooooooooooo, kilio cha samaki machozi kwenda na majiiiii
   
 7. a

  axel fowly Senior Member

  #7
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 109
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  dah!! watu watateketea sana kwa moto...hawana hata huruma mtoto wa masikini unampa asilimia sifuri wakati pesa za kujilipa mishahara mikubwa ipo..
   
 8. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #8
  Aug 26, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Kila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake, akiwa karibu na majani atakula majani kama ni marando/matembele yeye atakula tu! Na siku hizi mbuzi wa mjini wanakula hata maembe na ugali wa watoto, halafu sisi tunashangilia ... ooh ona mbuzi wa mjini.. wa kisasa hawa... hata ugali na maembe wanakula...!!!
   
 9. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #9
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kula na mimi nile
   
 10. NingaR

  NingaR JF-Expert Member

  #10
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 15, 2012
  Messages: 2,836
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mimi nina swali moja tu,
  First Year wa 2012 mkopo upo au haupo??
   
 11. July Fourth

  July Fourth JF-Expert Member

  #11
  Aug 26, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 2,288
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  ole wao watunyime mkopo wakati siri yao imefichuka....
   
 12. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #12
  Aug 26, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,955
  Likes Received: 37,495
  Trophy Points: 280
  Lakini tujiulize waziri mhusika nini atafanya baada ya kashifa hii kuibuliwa leo. Si ajabu kashifa hii ikapita hivi hivi kwasababu mawaziri wengi hawana ujasiri wa kuchukua maamuzi mazito. Kuna mawaziri kila baraza linapovunjwa na kuundwa upya wao wamo lakini utendaji wao hauridhishi kabisa.Kweli kupeana vyeo kama sadaka ni jambo baya sana na la kuisikitisha na kuathiri taifa kwa kiasi kikubwa.

  Ufisadi huu ni wa kutisha na wanaoteseka ni wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ambao kila wakati hupigwa mabomu.Wanafunzi wakiandama wanaambiwa wanatumika kisiasa kumbe ni kwasababu ya wazembe wachache tu.

  Uozo nchii umekuwa kama wimbo kwasababu raisi na mawaziri wake wamekuwa ni wazito kuchukua maamuzi magumu na kubaki kuwa watu wa maneno zaidi kuliko vitendo. Hivi kweli kama raisi na baraza lake la mawaziri wangekuwa wanachukua maamuzi magumu kama haya ya mh. Mwakyembe na mh. Kagasheki uozo huu kweli ungeendelea? Nani angekubali kuvuliwa madaraka na kufikishwa kwenye vyombo vyo dola? Rais asipotimuwa mawaziri wazembe na wasiowajibika nani tumlaumu?

  Tangu baraza jipya liundwe ni mawaziri wawili tu ndio wanaoonekana kuchukua hatua lakini wengine utadhani wizara zao hazina madudu haya au wako likizo. Hizi tuhuma za ufisadi zilizoibuka bodi ya mikopo zinatosha kabisa kuwaamsha hawa mawaziri wengine nao waanze kuchukua hatua vinginevyo maendeleo katika taifa hili itakuwa ni ndoto.

  Raisi kikwete ukiwa mkali kwa mawaziri wako utendaji wao utaonekana lakini mkienda kwa kubembelezana wewe ndio umma utakuja kukulaumu kwani wewe ndio mteuzi na mwenye mamlaka juu yao.
   
 13. MchunguZI

  MchunguZI JF-Expert Member

  #13
  Aug 26, 2012
  Joined: Jun 14, 2008
  Messages: 3,623
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Taarifa hii ya gazeti labda itawaamusha wa-TZ. Bodi hii ni kama tulivyosikia ajira za BoT. Kuna baadhi ya watu pale unamkuta baba yuko kwenye bodi, dada ni muajiliwa na kaka ni muajiliwa hapo hapo, siyo kwa sifa bali ni kwa sababu kuna pesa ya kuchezea.

  Bodi haijawahi kupata kiongozi. Mkurugenzi mkuu anayelipwa zaidi ya mil 13 siamini kama ni mtu mwenye akili timamu. Ukimuona si mtu wa kuhangaika kufikiri ili kuboresha hali ya utendaji.

  Hata ukiangalia background yake siyo mtu anayestahili kushika nafasi hiyo. Amekulia NBC enzi za ukiritimba na kama kawaida ya NBC yetu kazi muhimu ilikuwa ni kuchota pesa tu! Hajawahi kuwa kwenye taaisis ya elimu ya juu yoyote.

  Bodi haina sera! Kila mwka inaunda upya na ukiangalia sera zenyewe zinategemea matatizo ya mtu Fulani au mkubwa Fulani.

  Kuna mwaka walilipia wanafunzi kusoma Masters kwa sababu tu kulikuwa na ndugu yake na mwaka uliofuata wakaachana na sera hiyo.

  Sasa juu ya kuwanyoosha, hiyo tushau! Hakuna mtu ikulu! Rais wetu kila kitu ni majaliwa ya mwenyezi. Nimekuwa nikidhani labda mkuu wetu anafanya kwa makusudi lakini sasa naamini kabisa kwamba kuna tatizo la maumbile. Baada ya kuwapa miradi wanawe, kiongozi wetu anaamini nchi imeendelea!
   
 14. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Majungu tupu
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Aug 26, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Majungu matupu ,nasikia kuna kigogo mmoja (jina tunalo) amepigwa chini kwa ku "foji"vyeti ndio anawachafua wenzake kuandika makala hii ya uchochezi....tunasubiri majibu ya bodi maana hata ile tume iliyoundwa mwaka jana chini ya Prof Maboko ilibaini Bodi iko sawa,na inajitahidi sana kwa kasma waliokuwa wanapata kwa mbinde toka Wizara ya Elimu na si Wizara ya Fedha!!
  Acha tusubiri majibu toka kwa Bodi husika ila wanasikitika sana maana huyo kigogo alietolewa bila kufikishwa mahakamani,yatampata asiyoyatarajia maana sheria ni msumeno!
   
 16. S

  Safhat JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dah hi kasheshe.EWE MUNGU TUJALIE TUSINYIMWE MIKOPO.ameen.
   
 17. u

  usungilo JF-Expert Member

  #17
  Aug 26, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 499
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  hivi hakunaga member wa jf bodi ya mikopo? Haya mambo ya jina tunalo tumechoka nayo. Tunahitaji mtu atajwe tumzomee mtaani na kumpiga mawe. Au kwa sababu wanalipwa vizuri ndo maana hawaleti uozo wao huku?
   
 18. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #18
  Aug 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  tunataka majina ya wanaohujumu bodi tuwafuatilie zero distance
   
 19. m

  msafi Senior Member

  #19
  Aug 27, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hii ndio Tanzania!!!!!!!!
   
 20. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  I miss MWANAHALISI....Hii mambo ya "Jina Tunalo" "Majina Tunayo" huwa hakuna... wangeweka hapo majina na hata jina la kigogo Mwenyewe+ Namba za simu .....Kuhusu kujua kuwa bodi ya mikopo ina ubadhirifu kila mtu anajua issue ilikua nani anafanya ubadhirifu ambapo hata "chanzo cha hii makala" hakijamtaja....Same Old story za kulindana na kutengeneza mianya ya Rushwa katika tasnia ya Habari.... hapa ni huyo Kigogo au vigogo kusoma hii story na kumtafuta muandishi wampoze ili aipotezee hii issue......
   
Loading...