Jeshi la Polisi Mkoani Singida lipo katika kashfa nzito ya Wizi wa pesa za Watanzania. Jeshi la Polisi Mkoani humo limejenga Jengo la Ghorofa mbili, eneo la FFU kule Manguanjuki, na Jingine Jengo lililopo mjini karibu na ofisi za Usalama wa Taifa. Majengo mawili makubwa yamejengwa bila Zabuni kutangazwa, yanajengwa bila mkandarasi, yanajengwa na wafungwa, yamekaribia kukamilika, hatujui yana kiwango gani, yamekaguliwa na nani. Leo asubuhi wametangaza Zabuni. Makandarasi nendeni Singida mkashindanie majengo yaliyokamilika. Majengo haya yamejengwa kinyume cha taratibu za majengo ya Serikali, au majengo yanayojengwa mjini, yanayoonyesha Mkandarasi, Consultant, au Ruhusa ya Kujenga (Building Permit), na Kibali cha CRB. Kama polisi ni wezi vile wanakamata watu kwanini? ............... Kazi kwenu watanzania. Endeleeni kusubiri kuja kuunda kamati teule kwa mambo yanayoonekana yamefanywa kuwanufaisha vigogo. Waziri wa mambo ya ndani ulitembelea majengo haya umenyamazishwa. Tuambie kulikoni?. Zabuni imetangazwa leo wakati majengoyamejengwa yana miaka miwili. Ovyooooooooooooooooooooooo