Kashfa nyingine JK Nyerere Airport

vivian

JF-Expert Member
Nov 2, 2009
1,749
1,000
UWANJA wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere umekumbwa na kashfa nyingine, baada ya abiria, Mtanzania aliyekuwa tayari amegongewa muhuri wa uhamiaji kwenye hati yake ya kusafiria kwenda nje ya nchi, kutokomea kusikojulikana akiwa amewatapeli raia wa Poland, dhahabu na fedha vyenye thamani inayokadiriwa kufikia Sh80 milioni.

Tukio hilo limetokea huku kukiwa na kumbukumbu ya tukio la Desemba 2, mwaka jana pale abiria Zainabu Kaswaka alipokutwa na bastola kwenye ndege ya shirika la Emirates wakati akisafiri kwenda nchini Uingereza.

Wiki mbili baadaye, Desemba 17 mwaka jana, vyanzo vya habari za kiuchunguzi vimethibitisha kwamba raia wawili wa nchini Poland, Hery Jabloiw ambaye kitaaluma ni mhandisi na mwingine ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, walitapeliwa walipokuwa katika harakati za kusafiri kuelekea Warsaw kwa ndege ya saa 5:00 usiku ya Shirika la KLM.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, raia hao wawili wa kigeni, walikuwa nchini ambako siku zote walikuwa na urafiki na raia huyo wa Tanzania (jina tunalihifadhi kwa sasa) ambaye aliwasaidia kununua madhini ya dhahabu kwa mapatano kwamba wangemlipa kiasi fulani cha fedha.

Siku safari walifika naye uwanjani hapo kwa ajili ya kwenda naye Warsaw, Poland ambako wangemlipa malipo ya mwisho kwa mujibu wa makubaliano yao.

Vyanzo hivyo viliongeza kwamba katika mazingira ya kutatanisha, kabla ya kufanyiwa ukaguzi na kuingia uwanjani, raia huyo wa Tanzania aliwaambia Wapoland hao kwamba, madini wasingeweza kusafiri nayo kama mzigo wa mkononi na badala yake aliwashauri ufanyike utaratibu wa kusafirishwa kama kifurushi katika ndege ya mizigo.

Kufuati ushauri huo, Mtanzania huyo alikwenda kushughulikia suala hilo na baadaye kurejea na nyaraka bandia zilizothibitisha kwamba mzigo ulikabidhiwa kwenye ndege kwa ajili ya kusafirishwa.

Baada ya mchakato huo, tapeli huyo na raia hao wa kigeni walipita kwenye mashine za ukaguzi, kisha kwenda ofis za Idara ya Uhamiaji ambako waligongewa mihuri kwenye hati zao za kusafiria.

Taarifa hizo zinadai kuwa wakiwa tayari wamepita idara ya uhamiaji na kupata idhini ya kusafiri kwenda ng’ambo na baadaye kukaa katika chumba cha kusubiria ndege, ghafla Mtanzania huyo aliwaambia Wapoland hao kwamba kama wana fedha za Tanzania wampatie ili akazibadilishe kuwa dola za Marekani.

Katika mazingira ya kushangaza, Mtanzania huyo alitoka nje na fedha hizo Sh100,000, licha ya kwamba alishafanyiwa ukaguzi na kugongewa muhuri wa uhamiaji kwenye hati aya kusafiria.

Mwananchi lilibaini kwamba, raia huyo ambaye tayari alikuwa amelipwa ujira wa Sh1.7 milioni na Wapoland hao kama shukrani ya kuwasaidia katika utafutaji wa madini, alipotoka nje alipita sehemu zote za ukaguzi bila kuulizwa na akatokomea.

Vyanzo hivyo vilisema Wapoland hao walipanda ndege kwa matarajio kwamba rafiki yao angerejea, lakini haikuwa hivyo kwani ndege ilipokaribia kuruka, walitoa taarifa kwa vyombo vya usalama uwanjani hapo, hivyo wakaahirisha safari.

Walikaa usiku mzima uwanjani bila kumwona raia huyo, na hapo walibaini kwamba walikuwa wametapeliwa na hawakuwa na fedha za akiba kwani walimwambia Mtanzania huyo kwamba, kiasi kingine cha fedha za shukrani wangempatia baada ya kufika Warsaw.

"Wale Wapoland walikaa uwanjani pale hadi asubuhi wakawa hawana hata senti moja. Kuna askari mmoja aliwasaidia na kuwapa chai na chapati. Lakini, watu wanahoji iweje mtu aliyegongewa mhuri wa uhamiaji tayari kwa kusafiri, arejee tena nje na aruhusiwe?" kilohoji chanzo kimoja uwanjani hapo na kuongeza:,
"Kwa sababu, kiutaratibu mtu ukishagongewa mhuri wa uhamiaji maana yake tayari unatakiwa usafiri ng'ambo. Kama akipatwa na dharura, lazima aombe wahusika wakamsadie hawezi kutoka hivihivi, hili ni kosa lakini hapa inaonekana kuna mchezo."

Mkurugenzi
Alipoulizwa Mkurugenzi Mkuu wa Uwanja huo, Moses Mlaki alisema asingeweza kuongea suala hilo kwenye simu, na badala yake alitaka apewe maswali kwa maandishi.

Mkuu wa usalama wa uwanja huo, aliyejulikana kwa jina la Msangi alipoulizwa yeye alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwani eneo lake la kazi, linaishia kwenye ukaguzi wa mashine tu.

Baadhi ya vyanzo vyetu kinachochangia uhalifu ni baadhi ya vibanda vinavyotumiwa na askari kulinda uwanja huo kutokuwa na huduma za umeme na maji hali inayowafanya kufanyakazi katika mazingira magumu.
"Yaani hakuna maji, umeme wala nini, angalia tunalinda mitambo nyeti ya uwanja yenye thamani kubwa lakini maeneo yetu ya kazi hayana umeme wala maji. Tutafanyaje kazi katika hali hii?," kilihoji chanzo kimoja.
 
Hapa changamoto kuu ni kujiuliza ni kwa namna gani huyu mtu ambaye keshafanyiwa ukaguzi anaweza akaruhusiwa kutoka nje hivihivi, nahofu siku moja kwa uzembe huu usalama wa uwanja, ndege na abiria utakuwa compromised!!! Sasa naamini kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!
 
Hiyo inshu ni ndogo sana kwa Airport ile hata sishangai! ni suala dogo sana mtu anagongewa exit anazunguka anagongewa entry huyo mtaani. so M 1.7 aliyopewa ya asante plus total value ya kununua hayo madini ambayo ni kanyaboya jamaa ana mshiko wa nguvu tu! besides,,hivi angeenda huko Warsaw how sure was he kwamba wasingemgeuka na pengine kumchinjilia mbali?
 
Hapa changamoto kuu ni kujiuliza ni kwa namna gani huyu mtu ambaye keshafanyiwa ukaguzi anaweza akaruhusiwa kutoka nje hivihivi, nahofu siku moja kwa uzembe huu usalama wa uwanja, ndege na abiria utakuwa compromised!!! Sasa naamini kweli Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!
Hakuna tatizo la kufanyiwa ukaguzi na kutoka nje kwani ukirudi utafanya ukaguzi tena. Kikubwa hapa si kutoka nje unaweza ukatoka lakini ujue utapita na kukaguliwa tena na tena that's all it takes.
 
Hongera zake huyu Mzelendo halisi, Hivi ndio tunavyoibiwa dhahabu zetu. Mtu yoyote anayewaibiya Wageni waliokuwa na nia ya kutuibia rasilimali zetu huwa na msifu na namuona kama Mzalendo
 
Wanataka kupitisha dhahabu kwa mlango wanyuma bila ya kulipa ushuru, huu ni wizi tena hao wazungu walitakiwa kusekwa lupango kwa kutaka kutorosha rasilimali za taifa bila ya vibali. Na walitakiwa waulizwe wamekuja hapa nchini kwa mpango gani? Wengi wao wanajifanya wanakuja kufungua NGO kumbe wanakuja kutuibia Rasilimali zetu. Polisi walitakiwa wawe wanawahoji hao wazungu sio kuwapatia chai na Chapati za bure, na hao mapolisi ni washamba wa wazungu wanataka kujipendekeza. Huyo mtu aliyeondoka na hizo dhahabu alitakiwa kupewa zawadi. Je sasa tujuulize ni Wageni wangapi wanaopitisha dhahabu kwa njia hiyo bila ya kulipiwa ushuru?

Kweli Serikali yetu ni legelege
 
Back
Top Bottom