Kashfa mpya mradi umeme | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kashfa mpya mradi umeme

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Dec 29, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mwandishi Wetu


  [​IMG]


  Abhijeet Group


  Serikali yatuhumiwa kutetea wawekezaji wakwepa kodi
  Ni kampuni kubwa ya Kihindi, magazeti India yaifichua


  KAMPUNI kubwa na mashuhuri nchini India, Abhijeet Group, ambayo inalenga kuwekeza katika uzalishaji umeme pamoja na mradi wa makaa ya mawe nchini, inahusishwa na kashfa ya ukwepaji kodi India na kwa upande mwingine, taarifa kuhusu uwekezaji wake nchini Gabon zina utata,Raia Mwema, limebaini.

  Kashfa dhidi ya kampuni hiyo zimekuwa zikiripotiwa na magazeti kadhaa nchini India kwa muda sasa. Uchunguzi wa Raia Mwema, umebaini kuwa Gazeti la The Times of India la Januari 19, 2011, limeripoti kashfa ya ukwepaji kodi inayohusu kampuni hiyo.

  Lakini licha ya kashfa hizo, tayari uongozi wa kampuni hiyo umekaribishwa nchini na kuzungumza na baadhi ya viongozi serikalini, akiwamo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Gray Mwakalukwa, ambaye amedai kashfa dhidi ya kampuni hiyo ni uzushi.


  "Mimi nahusishwa vipi na mipango ya uwekekezaji wa kampuni hiyo? Masuala ya mgodi wa makaa ya mawe Kiwira yako serikalini chini ya Consolidated Holding Corporation"alisema Mwakalukwa na kuongeza:


  "Mgodi huo haujaletwa STAMICO, kampuni kadhaa zimekuwa zikifika STAMICO kuulizia juu ya mgodi wa Kiwira siyo Abhijeet peke yake," alisema Mwakalukwa.


  Lakini wakati Mwakalukwa akisema hayo alipoulizwa na Raia Mwema, zipo taarifa kuwa Ubalozi wa Tanzania nchini India, haujashirikishwa katika kuitafiti kampuni hiyo na tuhuma zake.


  Juhudi za gazeti hili kuzungumza na Balozi wa Tanzania nchini India, Dk. John Kijazi, hazikuzaa matunda baada ya simu iliyopigwa ubalozini hapo kujibiwa na Katibu Muhtasi kuwa, Balozi yuko kwenye likizo hadi mwanzoni mwa Januari, mwakani.


  Hata hivyo, zipo taarifa nyingine serikalini kwamba ubalozi haujashirikishwa katika kuipata kampuni hiyo kama ambavyo imewahi kutokea wakati ikitafutwa kampuni ya Richmond ya Marekani ambayo baadaye ilibainika kuzongwa na utata ikiwamo uwezo wa kazi ya kuwekeza katika kuzalisha umeme.


  Juhudi pia za kuupata uongozi wa Abhijeet Group kuzungumzia madai yanayoelekezwa kwao na magazeti mashuhuri nchini India zinaendelea, ingawa kwa wiki hii hazikufanikiwa.


  Abhijeet Group ni nani?

  Kampuni ya Abhijeet Group, si kampuni yenye rekodi safi ripoti kadhaa zinaonyesha hivyo hasa nchini India ambako ndiko kwenye makao makuu ya kampuni hiyo inayotaka kuwekeza nchini.

  Nchini India, kampuni hii inazongwa na kashfa ya ukwepaji kodi na suala hilo si la kificho kwa kuwa tayari limeripotiwa kwenye baadhi ya magazeti makubwa na mashuhuri nchini India.


  Kutokana na rekodi hiyo ya kutia shaka, swali muhimu miongoni mwa maofisa serikalini ni uhakika gani upo kwamba kampuni hiyo itaweza kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za Tanzania.


  Gazeti hili limeelezwa kuwa vyombo husika vya serikali vimeshindwa kufanya uchunguzi wake kwa njia huru, ikiaminika kuwa baadhi ya viongozi serikalini wana maslahi na ujio wa kampuni hiyo.


  Kampuni hii pia inadaiwa kuwa sugu katika kutoendeleza kwenye migodi inakowekeza na hili limeripotiwa na vyombo vya habari vya India, na hapa ndipo unazuka utata kwamba vipi wakiwekeza katika Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira, mgodi wenye rekodi ya kuwekezwa katika mikono ya wababaishaji.


  Ujio wao nchini

  Kampuni hiyo imekwishaanza hatua za awali za mchakato wa uwekezaji nchini na tayari imefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Madini (STAMICO), Gray Mwakalukwa.

  Uthibitisho wa mazungumzo kati ya Mwakalukwa na uongozi wa Abhijeet Group ni habari iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na gazeti la Serikali nchini la Daily News la Desemba 15 mwaka huu.


  Iliripotiwa katika Daily News ya kuwa Abhijeet Group, watawekeza katika uzalishaji wa megewati 600 za umeme, kiwango ambacho ni kikubwa mno ikilinganishwa kuwa mahitaji ya jumla ya umeme nchini ni takriban megawati 1,000.


  Habari hiyo inaeleza kuwa umeme huo utaingizwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya matumizi na hivyo kupunguza matatizo ya umeme nchini kama mradi huo utatekelezwa kwa ufanisi na si ubabaishaji.


  Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Abhijeet Jayaswal na mwenzake ambaye ni Mkurugenzi wa Oparesheni za kampuni hiyo katika miradi yake nje ya nchi (India), Abdulrahman Khan, wamenukuliwa wakieleza tayari wamekwishazungumza na Mwakalukwa, kuhusu masuala mbalimbali.


  Kwa upande wa suala la madini, kampuni hiyo inatajwa kulenga kuwekeza katika mradi wa makaa ya mawe, Kiwira, mwelekeo ambao umejitokeza katika mazungumzo yao na Mwakalukwa.


  Kutokana na miradi mingi ya umeme kugubikwa na kashfa mbalimbali, nyingine zikihusu udhaifu wa kampuni za kigeni zinazowekeza nchini, gazeti hili limefuatilia kwa undani kuhusu kampuni hiyo ya India, ikiwa ni pamoja na taarifa za kampuni hiyo nchini India.


  Kashfa ya ukwepaji kodi

  Gazeti la The Times of India, Januari, mwaka huu liliripoti madai kwamba kampuni hiyo imetumbukia katika kashfa ya ukwepaji kodi na imekuwa chini ya uchunguzi wa maofisa wa Idara ya Kodi.

  Wapelelezi hao wameripotiwa kuwa na wasiwasi kuhusu kampuni hiyo kuweka taarifa zisizo sahihi za mtaji wao kwa lengo la ukwepaji kodi.


  Abhijeet Group inayotajwa kuhusika zaidi katika miradi ya uwekezaji umeme, migodi, chuma, saruji na ujenzi wa barabara inatajwa kutokuwa na taswira nzuri kibiashara na hasa katika suala la kodi nchini India.


  Utata wa mtaji wake

  Mbali na kashfa hiyo ya ukwepaji kodi, madai mengi yanayoelekezwa kwa kampuni hiyo kwa mujibu wa gazeti la The Times of India ni utata wa upatikanaji wa mtaji wake.

  "Ukitazama nyaraka zake kwa juu juu utaweza kubaini hakuna kasoro yoyote, karibu kila kitu kipo sawa kisheria. Lakini hali halisi haiko hivyo, kampuni hii inakabiliwa na matatizo mengi ya kutiliwa shaka na hasa kwa upande wa kampuni zake tanzu," kinaeleza chanzo cha habari kilichokaririwa na gazeti la The Times of India.


  Gazeti liliripoti kuwa matokeo ya uchunguzi uliowahi kufanywa yamebaini kuwa kampuni tanzu takriban 24, zimetoa mtaji wake kwa Abhijeet Group, lakini hata hivyo, kampuni hizo zimebainika kutokuwa na uwezo wa kutoa kiwango hicho cha fedha kwa Abhijeet kama mtaji.


  Mbali na utata huo wa mtaji, kampuni hiyo inatajwa kuwa na mkopo mkubwa unaodaiwa kufikia takriban asilimia 80 ya gharama za miradi yake yote inayoendesha au kusimamia.


  Madai ya utata wake Gabon

  Zipo taarifa zinazoeleza kwamba kampuni hii imepata kuwekeza takriban fedha sarafu za Euro, bilioni mbili, nchini Gabon, katika mradi wa uzalishaji umeme na viwanda vya chuma pamoja na ujenzi wa bandari.

  Hata hivyo, magazeti ya nchini India yamepata kuripoti kuwa kilichofanyika ni kutia saini makubaliano ya awali tu na Serikali na si kweli kwamba kampuni imeweza kuendesha shughuli zake huko Gabon.


  Hizo ni taarifa zinazonukuliwa kutoka kwa wizara husika ya Gabon na kwamba, hakuna uwekezaji wowote uliokwishafanyika.
   
 2. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Kweli Jk mpaka aondoke madarakani watanzania watkuwa wanatembea uchi...JK sio mfano wa kuigwa
   
 3. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Hawa RAIA MWEMA vipi !! megawati 600 siyo "kiwango kikubwa mno". Hizo megawati 1000 ndizo zinazozalishwa na kutumika sasa hivi, ingawa siyo zote zinazotumika kutokana na matatizo lukuki. Mahitaji ya umeme ya nchii hii ni zaidi ya hizo 600 ili tuweze kuelekea uchumi wa kati ambayo ndiyo malengo ya mpango wa maendeleo wa sasa.
  Hata hivyo kampuni hii inabidi ichunguzwe vilivyo. 10% inatumaliza.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  kwanini kampuni za kihindi za kitapeli?
   
 5. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mh nchi hii bwana kwenye bajeti utasikia eti ''jamani kasungura kenyewe ni kadogo'' hivyo tukagawane kidogo kidogo. Eti hatuwezi kuwaletea maendeleo kwa haraka maana serikali haina hela
  Cha ajabu kila siku nchi inahujumiwa na kuibiwa mabilioni. kweli tuingie tu barabarani kama misri ila tukisema tusubiri mpaka 2015, mh tutaanza kuogea majani ya mipapai maana hatutakuwa na uwezo hata wa kununua sabuni.
  Aibu tupu
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nitafurahi sana kama watu watafuatilia pia ile kampuni ya Kichina itakayo chimba makaa ya mawe Mchuchua tujue records zake..
   
 7. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Nadhani wamesikia weakness za nchi yetu katika sekta ya uwekezaji wa umeme ndo maana wakakimbilia kwetu kuja kuvuna.Nina uhakika watafanikiwa tu kwani nchi yetu imejaa wachumia tumbo wengi.
   
 8. k

  kindafu JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Tulishakuwa "shamba la bibi" kila mmoja anakaribishwa! Usalama wa Taifa unafanya intelijensia ya kudhibiti chadema tu? Haya bwana!
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Ukiskia LAZY JOURNALISM ndio huku

  this says alot about OWNERS wa hili gazeti na bila kusahau EDITORS

  Lakini overall it also says alot about gutter journalism tulionayo Tanzania

  unfortunately GREAT THINKERS wa JAMII FORUMS nao watakuja humu na bandwagon zao kulalamika na kusema kila neno based on invisible writer ambaye anaitwa "MWANDISHI WETU"

  Pasco na Halisi watakuja hapa kutetea waandishi wa habari wa Tanzania kuwa wanafanya kazi kwenye mazingira magumu etc

  all in all how hard is it kwenda India na kufanya investigation za kila namna about this particular company badala ya ku copy na kupaste kila kitu from times of India na kisha kuja kudump humu?


  Kila kitu kwetu ni substandard!

  But then again tuna wanajeshi ambao wameshindwa kupanda mlima kilimanjaro na mwenye sembuse hili la waandishi na vyombo vya habari uchwara?


   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Dec 29, 2011
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Haya ndio mambo Usalama Wa Taifa wanatakiwa wafanyie due diligence badala ya kupoteza wakati na rasilimali za nchi kuwafuatilia wakina nani wanachangia huko Jamiiforums!!
   
 11. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #11
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tujaribu kupata wabia wa Western Europe au America tuone ubora wao kama unafaa; tired of Indians, Chinese tunapata misaada mingi toka Norway, Denmark and Sweden lakini hatuchukui utaalamu wao kwanini???
   
 12. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #12
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,178
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Mkuu usalama wa taifa ilikuwa zamani, siku hizi kazi zao ni:-kuratibu wizi wa kura kwny chaguzi mbalimbali, kudhibiti wapinzani, kushughulikia wanaotongoza mahawala wa viongozi, kukusanya, kuficha na kudhibiti vielelezo vya ufisadi visijulikane kwa umma, kulewa pombe na kujitapa kwamba wao ni usalama wa taifa. .da list goes on!
   
Loading...