Binti Msichana
Senior Member
- Oct 9, 2016
- 109
- 249
Nikiwa kama mzazi mzalendo nachukua nafasi hii kujulisha umma kuhusu watumishi wachache wa serikali wanaorudisha nyuma juhudi za Mh.Rais John Pombe Magufuli katika kuhakikisha kila mwanafunzi anapata elimu bure.
Ninasikitika Afisa wa elimu sekondari Bagamoyo akiwemo mkuu wa shule ya sekondari Dunda kufumbia macho vitendo vya walimu wa kiume wa shule ya sekondari Dunda kufanya mapenzi na wanafunzi huku baadhi yao wakikesha kwenye mabaa na wanafunzi wa kike wanaofanya nao ngono wakinywa pombe hadharani.
Tunajua kwamba walimu hawa ni marafiki wa karibu wa mkuu wa shule, urafiki huo usiwe kigezo cha walimu hawa kufifisha ndoto za wanafunzi hawa kwa kuwaharibia maisha yao.Taarifa za walimu hawa mkuu wa shule Dunda Sekondari anazo lakini hakuchukua hatua yeyote.
Mh.Rais Magufuli asihujumiwe katika jitihada zake za kutoa elimu bure na baadhi ya watumishi wachache wasiokuwa hata na chembe ya uzalendo.
Iweje Mwalimu ikiwa kama mlezi unakaa baa ukinywa pombe na mwanafunzi unaetembea naye kingono hadharani?
Nashauri serikali hii tukufu ya rais John Pombe Magufuli iunde tume kuchunguza kashfa hii inayofifisha elimu yetu.