Kasheshe la Mafuta: Dar kimeanza kuwaka, vituo kadhaa vyaanza kutoa mafuta!

Kwa hisani ya WATANABE:
avatar41784_2.gif
 
kutokana na hali ilivyo sasa naunga mkono serikali kushinikiza wauza mafuta kutoa mafuta tyao kwenye maghala ili kuepusha taifa kudondoka kiuchumi na kufa lakini hili jawabu la muda mrefu


suluhisho la muda mrefu

kama lita moja ya mafuta inatozwa zaidi ya shs 500 wakati bei yake ni shs 1911

nini tunapata kutoka katika gram moja ya dhahabu ambayo ni zaidi ya shs 50,000


majumuhishoserikali imeshindwa kutoza kodi stahiki kwenye migodi na hii imepelekea kulazimisha kutoza kodi kubwa kwenye mafuta na vinywaji hari hii haikubaliki
 
Twenty four hours inaishia baada ya 24hrs - right?

EWURA wanasema : Compliance Order = High Court Decree - right?
 
hii inatakiwa isambe nchi nzima-kuna wahindi wapumbavu wanataka watuletee mambo ya ajabu kwenye nchi ambayo si yao.
VIONGOZI WETU NAO WAMESHIKWA WANAJIKUTA WAPO KAMA VIPOFU-

NCHI ZOTE KUBWA SWALA LA MAFUTA NI SENSITIVE SANA-MAANA KITENDO CHA NCHI KUWAZUIA KUWAUZIA MAFUTA,INAKUWA UMEWATANGAZIA VITA-NA MARA MOJA WANAREACT NA WANASHINDA-NASHANGAA SISI MHINDI ANATOA MASAA 24 KWA SERIKALI.

HUU NI UPUMBAVU-KUGOMA KUUZA NI SAWA NA KUTANGAZA VITA-HIVI HAWA VIONGOZI WETU HAWAONI WENZAO WANAFANYEJE?
 
We unadhani tatizo hili ni la Dar tu?! Nipo Morogoro nimeona Lake Oil ndo wanauza mafuta .KAMA UNATOA SOLUTION JIKITE KWA TANZANIA YOTE. Me nasema vijana Tanzania yote tuhamasishane kupitia FB na JF Kila mkoa tupange meeting point kwa ajiri ya kufanya maandamano makubwa.

Mimi nimepropose kwa Dar, si mbaya na wewe ukafanya hivyo kwa huko Moro ulipo, na mwingine akafanya hivyo kwa Mtwara.....n,k.
 
hatutaki uhuni tanzania.
Serikali iwache biashara iwe huria.
Wanaopiga mawe wakome mara moja.wasituharibie swaumu zetu

Ustake watu wa tukanwe bure kwa ajili yako! Kama ume funga kimpango wako hauna sababu ya kutujulisha sis. Nenda kajifungie msikitini watu wakomboe nchi yao,kwanza wenye vituo wengi ni jamaa zako wamefunga kama wewe hvyo endelea kuwatetea!.
 
lakini kutokana na utafiti wangu naungana na serikali katika kuwalazimisha wafanyabiashara wa mafuta watoe mafuta kwani usalama na uchumi wa nchi huko kwenye hari mbaya sana sasa jamii inateseka kutokana na ukosefu wa mafuta lakini ili liwe ni suruhisho la muda mfupi kabla ya kukaa na wafanyabiashara wa mafuta .


nini liwe suruhu la muda mrefu?

serikali imekuwa ikitoza kodi kubwa sana kwenye kila lita moja ya mafuta( shs zaidi ya 500 kwa lita inayouzwa 1911)
lakini imeshinda kutoza kodi japo ata ya 500 kwa gramu ya dhahabu na madini mengine (1 gm ya dhahabu ni zaidi ya shs 50,000)

kutokana na hili natambua kuwa ni fika kuwa serikali inawaonea wafanyabiashara wa mafuta na vinjwaji na kuwaacha huru wenye migodi hii inapelekea wenye biashara ya mafuta kuumia na wenye migodi kutolipa kabisa kodi


lazima serikali iongeze kodi kwenye madini yetu na kupunguza kodi ya mafuta na vinywaji
 
Huu Ni mtazamo for those who cant think loudly around issues!!!!, narrow minded person anaeendeshwa na ushabiki usiokuwa na maana. Watendaji sisi hatuwatambui.

Sisi tunawatambua viongozi wa kisiasa, kwani wao ndo wamepewa dhamana ya kusimamia mali za watanzania, wakawateua watu ambao wao wanawaamini, sasa kama hawatendi kwa mujibu wa matarajio ya watanzania kwa nini hawawawajibishi?

Hatuwezi kuwalaumu watendaji hata siku moja, kwa kuwa sisi hatuwajui na wala hatujawapa hiyo kazi.

Umenisoma bwana mzee!!!. Sisi tutaendelea kulia na viongozi wa kisiasa, wanao wakabidhi usimamizi wa mali zetu hawa watu wanaoshirikiana kula nao, matokeo yake ikifika wakati wa kuchukua hatua serikali inakuwa na kigugumizi.
Mkuu uko sahihi kwa hili. Hata mtoto anapodokoa ukimkanya huacha, lakini ikiwa utanyamaza ataendelea kudokoa tu. Kazi ipo kweli kweli.
 
Sisi tunaelekea BP Kurasini maana hawa ndiyo "sugu" zaidi! Petrol niliyobaki nayo kwenye tank inaweza kutengeneza japo BOMU moja la petrol! Kwa mlio mitaa hii muda msiyo mrefu mtaanza kuona "flames of hope"!
 
Poleni sana watu wa Dar (na kwingineko kusiko na mafuta). Pambaneni, kama vipi tutawaunga mkono ingawa huku Morogoro mafuta yapo kama kawa kwa bei ya zamani (kabla ya tangazo la ewura); Petroli 2029, dizel 1970...
 
Nainoea huruma sana serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania kwani imejiingiza kwenye tatizo ambalo viongozi wasipokuwa makini litawadhalilisha wao p0amoja na serikali yao kwa ujumla,kutangaza bei ya mafuta na kushindwa kuwa na power of command juu yake ni aibu kwa serikali japo hakuna sheria yeyete ya liberal economy inayoruhusu hicho kilichofanya na serikali ya ccm. Jambo kama hili lilishatokea kwa serikali ya kikaburu iliyokuwa inatawala south afrika kuanzia mwaka 1960 hadi 1985 ambapo liberal banking ilipangiwa namna ya kuoperate

ila walifanikiwa kutimiza azma yao sasa serikali imeshindwa kwani mpaka hapo ilipofikia itakuwa ni aibu tena kubwa

hii inaonyesha wazi jinsi viongozi wetu hawafanyi mambo yao stratefically ma madhara huenda kwa raia

goverment where is the power of command?
 
tuanze kuandama hapa jf...
Miimi bango langu linasema

mafuta hakuna
umeme mgao
shilingi haina thamani

hatuna imani na selika
selikali ijizuruuuu

bango zuri, limekamilika, naunga mkono baada ya kubadili kido spelling,
hatuna imani na serikali
serikali ijiuzuluuu!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom