Kaseja Nimefurahi alivyoondolewa Simba SC

Kaseja Nimefurahi alivyoondolewa Simba SC

Kuondoka kwa kaseja kutafuata kuondoka kwa kibadeni baada ya mechi sita mzunguko wa kwanza,Na mtamkumbuka sana.
 
Uganda one = Abel Dhaira ndiye no.1 Mpya SIMBA.

Mlipomleta yule hakuffi hapana nimekosea Akuffo toka Ghana mliongea sana mwisho wa siku mkakaa kimyaaaa, subirini huyo Dhaira ageuke Delila ndipo mtakapomkumbuka Juma K Juma, mlipowafunga Zamaleki mlimbeba kama mfalme leo mmeshasahau mnamuona kama zile karatasi nyepesi za kule ofisi kuu, mkumbuke dua za aliyedhurumiwa haziendi bure.
 
Wengi hatukufurahishwa na Kaseja kuachwa lakini sasa inabidi tuelewe hakuna marefu yasiyo na ncha, Kaseja kaachwa lakini si kwa kufukuzwa bali ni mkataba kuisha, hatuwezi kuendelea kulaumu tu uongozi kwa sababu ya kutompa Kaseja mkataba mpya, yeye mwenyewe hajaongea hatujui mahitaji yake yalikuwa ni yapi kwenye mkataba wake.

Kingine ambacho kinachonishangaza ni hawa wadau wa upande wa pili pale kwenye majaruba yao, ni hawa hawa waliokuwa wanalalamika Kaseja kupangwa kila mechi na wengine walikuwa wanaenda mbali zaidi na kumwita majina ya ajabu lakini leo wamekuwa watetezi wakubwa wa Kaseja sijui hii huruma kwa Kaseja inatoka wapi, na waandishi wetu uchwara nao mara nyingi wanapenda kushauri kuwa timu zikuze vipaji na ziachane na magari ya mkaa leo Kaseja kaachwa kila mtu anailaumu Simba, tulaumu sawa lakini sio kupita kiasi na kuanza kuiombea timu ifanye vibaya, Simba ni timu itaendelea kuwepo bila ya Kaseja, ni kweli ameitumika timu kwa muda mrefu lakini sasa sisi inabidi tujifunze kukubali ukweli kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, mwisho wa Kaseja kuitumikia Simba umefika tuwaacheni viongozi wa Simba wafanye kazi yao maana timu ikifanya vibaya wao ndo watawajibika.
 
Hili la Kaseja inabidi watu mkumbuke kisa cha Romario de Souza na Big Phiri (Scolari). Wabrazil waliapa Kumuua Scolari kama hawatachukua W.C kisa kamuacha Romario. Lakini Scolari alimpa nafasi Ronadinho Gaucho kuziba hilo gap la Romario. Wanao kumbuka nadhani mliona vitu alivyofanya bwana mdogo Gaucho enzi zile. Hivyo Pengo la Kaseja simba litazibika tu.

Ni kweli Mkuu, Scolari alipeta yuko hai hata leo, lakini Kibadeni mmh!
 
Weye Masuke unamdanganya nani? Pamoja na Yanga kuwa majalubani wana eneo kubwa la kutosha na jengo zuri kuliko kile kijengo cha pale Msimbazi. Nimepita pale leo na kugundua kuwa mtaa mzima wa Msimbazi hakuna jengo la ovyo kama la Simba hadi fungi wameliandama sasa. Kumwacha Kaseja ni furaha sana kwetu, ninyi hamjui tu hadi tunawashangaa kwa uamuzi wa kumwacha. Kaseja is the man of his time, shauri yenu.
 
Mkuu kwani kuna chochote cha uongo hapo, ni rahisi mtu kuwa na eneo kubwa nje ya mji kuliko katikati ya mji, ulitaka na sisi tuwe na kiwanja kikubwa pale mjini kati kama kile chenu cha majarubani, fanyeni land reclamation ili mpate kiwanja kikubwa zaidi maana pale hakuna tofauti na bahari mvua ikinyesha.

Kuhusu Kaseja hata mimi sijafurahi lakini kwa nini niendelee kulaumu upande mmoja bila kusikiliza upande wa pili? Mbona wachezaji wengi Simba wameachwa hapakuwa na kelele nyingi kiasi hiki, huko kwenu hamkumbuki mlivyomwacha Lunyamila. Bado narudia tujifunze kukubalina na ukweli, Kocha na viongozi ndo wanajua nini wanafanya sisi mashabiki tubaki kuwa mashabiki na ukiona timu yako haikufurahishi unaiadhibu kwa kutoenda uwanjani. Na kama kweli mnafurahia Kaseja kutokuwepo nini kinafanya muanze kumruhumia au ndo huruma za mamba anatoa machozi huku anatafuna?
 
... Kuondoka kwa Kaseja Simba kutafungua fursa nyingine kubwa kwa wengine Kufahamika, kutaibua vipaji... ambao watakuwa na uchungu na klabu....Simba ni Simba itaendelea kuwa Simba... watapita wengi na webgi wameshapita.... si wachezaji tu bali hata viongozi..kumbuka alivyoachwa Mwameja hali kadhalika alivyoachwa George Magere Massatu walikuwa wanaonekana kama ndo wao tu lakini siku ikifika imefika....
 
MAXIMO alilijuahili la mtu KUHONGEKA/KUKOSA UZALENDO kwa timu yake..... tukazusha kuwa walichukuliana......mtu asiye na uzalendo hata kama ana kiwango cha sayari nyingine HAFAI
 
Kaseja katemwa coz alitaka mkataba mpya wa shilingi milioni 40 wakati hana thamani hiyo. Aende Rhino ya TBR lakini sidhani ka kuna team itamsajili
 
Nimefurahishwa sana na kufarijika kupita maelezo kusikia kwamba uongozi wa Simba SC umeamua kuachana kabisa na mchezaji wao golikipa Juma Kaseja Juma.....na nimatumaini yangu kwamba uongozi utaendelea na msimamo huo bila kurudi nyuma... hali hii imetokana na Kaseja kuonyesha kucheza jinsi anavyotaka jinsi anavyoamua kulingana na mechi hadi mechi.... akiamua leo adake sana na hakuna goli litakaloingia inakuwa hivyo.... akiamua leo afungwe magoli ya kizembe anafanya hivyo... lakini yote kwa yote hakuna kitu kibaya kama ulivyotufungisha mechi ya mwisho na Yanga (wengi SSC wanaamini hivyo) ... iliniuma sana...najua unakana kwamba hukuhujumu lakini wana Simba wengi hatutaamini kamwe.... japo mambo kama haya yalishawahi kuwakuta magolikipa wenzako kama Nemes, Ivo Mapunda, Juma Pondamali, Peter Manyika, Idi Pazi, Issa Manofu, Chachala Muya, Mohamed Mwameja, Doyi Moke...na wengineo mimi natoa ushauri kwa wachezaji wengine....... bora kuwa mjanja kama umekula vya watu siku ya mechi jifanye mgonjwa kuliko kuliko kuwakosesha raha mamilioni ya wapenzi wanaokuamini.... binafsi nakutakia heri kwa kuwa riziki haipo kwenye mpira au simba tu unaweza kufanya biashara nyingine..
Kwa hiyo unataka kutuaminisha kuwa mechi ya mtani wa jadi ndo chanzo cha JUMA KASEJA Kuachwa?
 
Mimi binafsi sina tatizo na kipa Kaseja maana yeye ni binadam na mcheza soka, wanaonikera mno ni wapambe wake hasa wanahabari. Hawa wanataka kutuambia kuwa viongozi wa klabu ya Simba wamemuonea ilhali uongozi/kocha ni wajibu wao kujenga timu ya klabu na si kumjenga mchezaji mmoja mmoja.
 
Kaseja katemwa coz alitaka mkataba mpya wa shilingi milioni 40 wakati hana thamani hiyo. Aende Rhino ya TBR lakini sidhani ka kuna team itamsajili
Tena sio shilingi kaka ni dola elf 40 sawA na mil 64 hv
 
Wengi hatukufurahishwa na Kaseja kuachwa lakini sasa inabidi tuelewe hakuna marefu yasiyo na ncha, Kaseja kaachwa lakini si kwa kufukuzwa bali ni mkataba kuisha, hatuwezi kuendelea kulaumu tu uongozi kwa sababu ya kutompa Kaseja mkataba mpya, yeye mwenyewe hajaongea hatujui mahitaji yake yalikuwa ni yapi kwenye mkataba wake.

Kingine ambacho kinachonishangaza ni hawa wadau wa upande wa pili pale kwenye majaruba yao, ni hawa hawa waliokuwa wanalalamika Kaseja kupangwa kila mechi na wengine walikuwa wanaenda mbali zaidi na kumwita majina ya ajabu lakini leo wamekuwa watetezi wakubwa wa Kaseja sijui hii huruma kwa Kaseja inatoka wapi, na waandishi wetu uchwara nao mara nyingi wanapenda kushauri kuwa timu zikuze vipaji na ziachane na magari ya mkaa leo Kaseja kaachwa kila mtu anailaumu Simba, tulaumu sawa lakini sio kupita kiasi na kuanza kuiombea timu ifanye vibaya, Simba ni timu itaendelea kuwepo bila ya Kaseja, ni kweli ameitumika timu kwa muda mrefu lakini sasa sisi inabidi tujifunze kukubali ukweli kwamba hakuna marefu yasiyo na ncha, mwisho wa Kaseja kuitumikia Simba umefika tuwaacheni viongozi wa Simba wafanye kazi yao maana timu ikifanya vibaya wao ndo watawajibika.
Maneno kuntu mzee let him go,walipoachwa kina boban watu walilamika mwisho wa cku watt wakapiga ball tukawasahau aliachwa beckham yupo kwenye peak pale man u,viongoz wameongea wamemuita mara kadha wazungumze yy anataka dola elf 40 angalia hali ya club kwasasa inayumba cos of money,nyinyi mnataka club iwe mzalendo kwa kaseja while kaseja hajataka kuwa mzalendo kwa club mwaka huu alitakiwa atufanyie hisan,club haina ela tungemlipa nn sasa hata hivyo hujuma ndogo ndogo zitapungua u never know.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom