Kaseja Nimefurahi alivyoondolewa Simba SC

Kaseja Nimefurahi alivyoondolewa Simba SC

pilau

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
1,595
Reaction score
450
Nimefurahishwa sana na kufarijika kupita maelezo kusikia kwamba uongozi wa Simba SC umeamua kuachana kabisa na mchezaji wao golikipa Juma Kaseja Juma.....na nimatumaini yangu kwamba uongozi utaendelea na msimamo huo bila kurudi nyuma... hali hii imetokana na Kaseja kuonyesha kucheza jinsi anavyotaka jinsi anavyoamua kulingana na mechi hadi mechi.... akiamua leo adake sana na hakuna goli litakaloingia inakuwa hivyo.... akiamua leo afungwe magoli ya kizembe anafanya hivyo... lakini yote kwa yote hakuna kitu kibaya kama ulivyotufungisha mechi ya mwisho na Yanga (wengi SSC wanaamini hivyo) ... iliniuma sana...najua unakana kwamba hukuhujumu lakini wana Simba wengi hatutaamini kamwe.... japo mambo kama haya yalishawahi kuwakuta magolikipa wenzako kama Nemes, Ivo Mapunda, Juma Pondamali, Peter Manyika, Idi Pazi, Issa Manofu, Chachala Muya, Mohamed Mwameja, Doyi Moke...na wengineo mimi natoa ushauri kwa wachezaji wengine....... bora kuwa mjanja kama umekula vya watu siku ya mechi jifanye mgonjwa kuliko kuliko kuwakosesha raha mamilioni ya wapenzi wanaokuamini.... binafsi nakutakia heri kwa kuwa riziki haipo kwenye mpira au simba tu unaweza kufanya biashara nyingine..
 
Binafsi sijapenda kabsa, kwan naamin JK Juma bado mchango, na uzowefu wake unahitajika sna SSC ukizingatia asahiv tuna timu ya vijana zaid!
 
subiri waje mkia aka Tahiti mwenzio mjibizane

FIFA defends Tahiti's right to play at Confed Cup Associated Press - 24 June 2013

RIO DE JANEIRO (AP) - World football's governing body has defended Tahiti's right to play at the Confederations Cup despite the Pacific Islanders scoring just once and conceding 24 goals in three losses.

The 138th-ranked Tahiti is one of the eight teams at the FIFA tournament in Brazil after winning the Oceania Nations Cup final. Finalist New Caledonia surprisingly beat regional power New Zealand earlier in a competition without Australia.

But at the 2014 World Cup warm-up event, Tahiti, with just one professional player, lost 6-1 against Nigeria, 10-0 against Spain and 8-0 against Uruguay.

FIFA General Secretary Jerome Valcke says "it would go against all principles if one confederation is not as strong as the other confederations, they will not have access to our competitions."
 
Jamani, si huwa mnasema kuwa kuna siku mtu 'mchezo' unamkataa? Kwa nini msiamini kuwa na yeye kuna siku mchezo unakuwa siyo hivyo anafungwa hayo magoli ya kizembe?
 
subiri waje mkia aka Tahiti mwenzio mjibizane

Pamona na utani wako nakuuliza swali kama Tahiti alifungwa na Nigeria... Spain akamfunga Nigeria.... nipe utabiri wako Tahiti vs Taifa Stars.... Taifa Stars Vs Spain....
 
Nimefurahishwa sana na kufarijika kupita maelezo kusikia kwamba uongozi wa Simba SC umeamua kuachana kabisa na mchezaji wao golikipa Juma Kaseja Juma.....na nimatumaini yangu kwamba uongozi utaendelea na msimamo huo bila kurudi nyuma... hali hii imetokana na Kaseja kuonyesha kucheza jinsi anavyotaka jinsi anavyoamua kulingana na mechi hadi mechi.... akiamua leo adake sana na hakuna goli litakaloingia inakuwa hivyo.... akiamua leo afungwe magoli ya kizembe anafanya hivyo... lakini yote kwa yote hakuna kitu kibaya kama ulivyotufungisha mechi ya mwisho na Yanga (wengi SSC wanaamini hivyo) ... iliniuma sana...najua unakana kwamba hukuhujumu lakini wana Simba wengi hatutaamini kamwe.... japo mambo kama haya yalishawahi kuwakuta magolikipa wenzako kama Nemes, Ivo Mapunda, Juma Pondamali, Peter Manyika, Idi Pazi, Issa Manofu, Chachala Muya, Mohamed Mwameja, Doyi Moke...na wengineo mimi natoa ushauri kwa wachezaji wengine....... bora kuwa mjanja kama umekula vya watu siku ya mechi jifanye mgonjwa kuliko kuliko kuwakosesha raha mamilioni ya wapenzi wanaokuamini.... binafsi nakutakia heri kwa kuwa riziki haipo kwenye mpira au simba tu unaweza kufanya biashara nyingine..

Hapa naona unamwonea Kaseja bure kusema kwamba alifanya uzembe kufungwa yale magoli dhidi ya Yanga, kama uliangalia vizuri uzembe ulifanywa na mabeki na sio golikipa, angalia watu waliokuwa wanacheza ile mipira ndani ya kumi na nane walikuwa free kabisa na wala hawakuwa na beki wa kuwaghasi.

Mimi sijafurahishwa na visingizio vinavyotolewa mara hatuna hela ya kumlipa mara ameshuka viwango, kwa nini wasingekuwa wawazi tu na kusema kwamba tunao magolikipa wa kutosha na huyu kwa sababu mkataba wake umeisha ndo maana tumeamua kumwacha.
 
Hivi kati ya Simba SC na Yanga ni nani anastahili kuitwa Tahiti? Kwa kichapo cha mwaka jana cha 5-0 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi kwa nini Yanga a.k.a. Yeboyebo isiitwe Tahiti?
 
Kaseja sio kipa wa kuaminika. Tunamshukuru kwa mchango wake wa siku za nyuma, lakini kwa sasa atupishe tunataka kujenga timu yetu upya.
 
Hivi kati ya Simba SC na Yanga ni nani anastahili kuitwa Tahiti? Kwa kichapo cha mwaka jana cha 5-0 kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi kwa nini Yanga a.k.a. Yeboyebo isiitwe Tahiti?
Hivi wewe bado unakariri ngojera za mwaka juzi? wenzio wanaongelea Confederation Cup inayoendelea sasa, Ligi kuu inayoanza soon, kombe la dunia Brazil mwakani. any way kwa kukusaidia tu, hebu angalia jezi za tahiti halafu linganisha na jezi za simba ukiona mfanano hapo ujue Simba =Tahiti
 
Upumbaf...badala ya kukazia mawazo kwenye Confederation Cup bado unarudisha kwenye Simba = Tahiti...vipi wewe??
 
Wapenzi na viongozi wa Simba hamna shukrani, jinsi Kaseja alivyojitoa kwa timu yenu hamkupaswa kumuacha kwa lugha za maudhi hivyo ila sishangai sana kama mlishindwa kuonesha utu kwa marehemu (Mafisango) itakuwa kwa aliye hai? Tunawaombea kheri mumpate atakayewapa mchango kwa siku zake za mbele.
 
Simba lazima watajuta kumuacha Kaseja. Mechi 5 za awali ligi kuu zitatoa majibu. Kibadeni naye akifika mwisho wa msimu atakuwa mwenye bahati sana.
 
Simba lazima watajuta kumuacha Kaseja. Mechi 5 za awali ligi kuu zitatoa majibu. Kibadeni naye akifika mwisho wa msimu atakuwa mwenye bahati sana.

Nakushauri uweke kibao cha utabiri au unajimu hapo nje kwako..
 
Sasa ulitaka simba =spain?

Ile Tahiti ni timu ya Taifa ya kule, Simba ni club na si timu ya Taifa, Bora uweke Taifa Starz nitakuelewa!

Yaani ukisepa Yanga = Spain nitatoa alama sifuri kabisa! Yanga ni club wakati Spain ni timu ya Taifa!
 
Kaseja ata-kama kiwango kimeshuka kama baadhi ya viongozi wanavyodai, akustahili kufungashiwa virago kihivyo, mchango wake bado unaitajika; anyway siwezi jua labda demands zake zimekua za juu sana kiasi kwamba Simba imeona haitaweza kumudu; ila ni hasara kwa Kaseja na Simba vilevile.
 
Wapenzi na viongozi wa Simba hamna shukrani, jinsi Kaseja alivyojitoa kwa timu yenu hamkupaswa kumuacha kwa lugha za maudhi hivyo ila sishangai sana kama mlishindwa kuonesha utu kwa marehemu (Mafisango) itakuwa kwa aliye hai? Tunawaombea kheri mumpate atakayewapa mchango kwa siku zake za mbele.

Uganda one = Abel Dhaira ndiye no.1 Mpya SIMBA.
 
Simba lazima watajuta kumuacha Kaseja. Mechi 5 za awali ligi kuu zitatoa majibu. Kibadeni naye akifika mwisho wa msimu atakuwa mwenye bahati sana.

Hili la Kaseja inabidi watu mkumbuke kisa cha Romario de Souza na Big Phiri (Scolari). Wabrazil waliapa Kumuua Scolari kama hawatachukua W.C kisa kamuacha Romario. Lakini Scolari alimpa nafasi Ronadinho Gaucho kuziba hilo gap la Romario. Wanao kumbuka nadhani mliona vitu alivyofanya bwana mdogo Gaucho enzi zile. Hivyo Pengo la Kaseja simba litazibika tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom