Kasco yadhulumu wananchi mkoani Geita

Mzalauliwa

Member
Jul 31, 2014
89
30
Kampuni ya kuodhesha marudio ya dhahabu mkoani Geita, wilayani Geita vijijini jimboni Busanda kijiji cha Nyarugusu, KASCO, imekuwa ikidhulumu wananchi kijijini hapa pasipo na msaada wowote wa kisheria.

Kampuni hii imekuwa ikisimamiwa na Waarabu ambapo kazi za migodi zimekuwa zikitumia kemikali ambayo ni hatari kwa afya za Watanzania wenzetu. Kemikali hiyo aina Cyanide ni hatari katika maisha ya binadamu na watu huingia katika matanki hayo makubwa kufanya usafi bila vifaa maluumu ni sababu ya umaskini hupelekea vijana wengi kufanya kazi kwa kukosa ajira maalum na zenye mkataba.

Kampuni hii wasimamizi wake kuanzia nguzo ya meneja wote ni Waarabu. Inasikitisha sana kuona Watanzania wenzetu wakinyanyaswa.

Msaada unahitajika kwa watu husika wa jambo hili.
 
Mleta mada uko sahihi, Mimi naishi karibu na hiyo kampuni kunasiku MZEE mmoja alipigwa makofi kama kumi na Muarabu wa hapo Kasiko mchana kweupe, kisa ameenda kuomba PESA mkewe alikuwa anaumwa. Huyo MZEE alikuwa mlinzi hapo site. Alipigwa mbele za watu, nili umia sana japo sikuwa na namna ya kumsaidia. Fanya kazi KWA Mzungu bora kuliko Mwarabu NA Mhindi wana wachukulia watu weusi kama sio binadamu.
 
Back
Top Bottom