'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'- Karume Jnr

John Okello ambaye aliongoza Mapinduzi ya Zanzibar alizaliwa mwaka 1937 huko Uganda katika kabila la Langi ambalo pia ni la Rais wa Zamani wa Uganda Milton Obotte. Alizaliwa akiitwa John Gideon Etuku. Wazazi wake walifariki Akiwa bado mdogo na kulazimika kwenda kulelewa na mjomba wake pamoja na wadogo zake wawili lakini kutokana na utukutu wake hakuweza kuishi kwa mjomba sababu alikuwa akipigwa na akakimbia kwenda kuanza vibarua huko Soroti katika Gineri ya kuchambua pamba. Inasemekana alitaka kwenda kujiunga na jeshi lakini hakufanikiwa kutokana na umri mdogo.

Katika harakati za kutafuta maisha alifika hadi Nairobi nchini Kenya na kuendelea hadi Mombasa ambapo alikuwa ukifanya kazi za vibarua. Alichukia kiuitwa boy , mtumishi, au mtumwa . Mwaka 1955 aliwekwa gerezani huko na akiwa humo alikutana na wapiganaji wa maumau waliokuwa wakipinga Ukoloni nchini Kenya kutoka kwao alipata hamasa ya Kupambana na ukoloni na ukandamizaji.

Mwaka 1959 akiwa na rafiki yake Mluo walienda Pemba katika eneo la Vitongoji na akawa anafanya kazi ya kugonga na kuuza mawe. Huko alipendwa na kuwa na ushawishi na ndipo alipoanza kuonesha nia yake ya kuuondoa utawala wa Sultan. Wakati anaondoka Pemba alipatia chama cha ASP nyumba yake ili waifanye ofisi ya chama.

Mwaka 1963 alihamia Unguja na kuanza kufanya kazi za kupaka rangi nyumba pamoja na kufanya kazi katika kiwanda cha kuoka mikate na akaendelea na vuguvugu la kisiasa.
Kumekuwa na Tetesi kuwa aliwahi kuwa mwanajeshi na askari polisi na askari wa Mau mau lakini pia kuwa aliwahi kupigana wakati wa vita vya pili vya Dunia, dhana zote hizo si za kweli. Ukweli ni kuwa Okello hakuwahi kuwa mwanajeshi au kupata mafunzo ya kijeshi. Majigambo yake kuwa alikuwa na uzoefu wa kijeshi yalikuwa ni mbinu tu ya kumsaidia kuongoza mapinduzi

Alifanikiwa kuanzisha chama cha Mafundi rangi wa Unguja na Pemba na kupitia chama hicho aliweza kupenyeza ushawishi wake wa kufanya mabadiliko ya kumuondoa Sultan

Baada ya kufanikisha Mapinduzi aalimkaribisha Karume kuongoza serikali. Tatizo la Okello hakuwa na back up ya kisiasa na hakuweza kuaminika. Akatupwa na kufukuzwa bila shukrani. Mwanzoni alipelekwa Kenya lakini akafanya jitihada za kutaka kurudi nchini akakamatwa Mwanza na kufungwa. Lakini baadae akarudi Uganda.

Wakati Idd Amini alipompindua Obotte mwaka 1972 alikwenda kumpongeza. Lakini baadae akawa na Mawasiliano na kundi la Obotte lililokuwa Tanzania, katika harakati za kutaka kujiunga na kundi hilo alikamatwa na kuuwawa na Idd Amin.

Kwa hiyo tunaona kuwa Okello alikuwa Mwanamapinduzi. Kuongoza na kushiriki Mapinduzi ya Zanzibar haikuwa kwa ajili ya Mshahara, bali ilitokana na nia yake ya dhati ya kupinga ukoloni na ukandamizaji.
 
Sorry mie imenikalia kama alipelekwa na watu waliokuwa wakimtumia, na hao ndio baada ya mission kumalizika haraka haraka walijaribu kumuondosha (kufuta ushahidi).

P:S
  1. Picha imepigwa baada ya mapinduzi haina mashiko.
 
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Labda ungetupa more details kitu gani kinayafanya Mapinduzi yale yawe matukufu ? Roho za wazanzibari wasio na hatia ndio tunaadhimisha ? Keep in mind waislamu wote ni ndugu (dunia nzima), ndugu zetu walitolewa roho kwa kupigwa na Mapanga na akina Okello. Hiki ndio kinayafanya yawe matukufu (kutakwaswa ?).
 
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ndio jina rasmi la Mapinduzi yale, niliwahi kuuliza, Neno "Matukufu" Katika Mapinduzi ya Zanzibar, Lilitoka Wapi, na Yana Utukufu Gani?!,
P
 
Leo ni Karume Day, nami naomba kujiunga na Watanzania wenzetu maadhimisho mema ya Karume Day na kuwatakia mapumziko mema.
RIP Abedi Amani Karume.
Paskali
 
Leo ni Karume Day, nami naomba kujiunga na Watanzania wenzetu maadhimisho mema ya Karume Day na kuwatakia mapumziko mema.
RIP Abedi Amani Karume.
Paskali

Huyo jamaa alikua ni dikteta mmoja mbaya sana, Hata jiwe ni mtoto mdogo tu mbele yake.
 
Huyo jamaa alikua ni dikteta mmoja mbaya sana, Hata jiwe ni mtoto mdogo tu mbele yake.
Fikilia Kama Leo tumeadhimisha miaka 50 ya kifo chake,ukichanganya na miaka yake,lazima ujiulize huyo mkewe wakati anaolewa alikuwa na miaka chini ya 18 au alikuwa mtu mzima? Na mpaka leo huyo mama ana miaka mingapi?
 
Jamaa chini ya utawala wake yamefanyika matukio ya ajabu mingi sana.
 
Tarehe kama ya leo 11/01/1964 miaka 60 iliyopita, ndio Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalifanyika!. Alfajiri ya Tarehe 12 Januari, 1964 ilikuwa ni kutangazwa tuu!.

Nawatakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Si tulikubaliana ni mapinduzi matukufu ya Tanzania visiwani
 
Si tulikubaliana ni mapinduzi matukufu ya Tanzania visiwani
Tanzania visiwani ndio Tanzania Zanzibar kwa kifupi Zanzibar.
Nakutakia maadhimisho mema ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…