Karuka mkojo, kakanyaga mavi.

Kirikou Wa Kwanza

JF-Expert Member
May 24, 2013
3,564
1,991
Kuna Jamaa alikuwa safarini kuelekea vijiji vya mbali, bahati mbaya kiza kilikuwa kimeanza kuingia kabla ya kufika mwisho wa safari yake. Jamaa ikabidi kuomba hifadhi katika nyumba moja. Jamaa akakaribishwa vizuri na wenyeji wake wakamwambia, "Jisikie kama upo nyumbani utalala kwenye chumba hicho." Jamaa akawashukuru sana wenyeji wake kwa kumsitiri akajiona mwenye bahati. Basi muda wa kulala ulipofika Jamaa akaingia kulala; katika chumba hicho kulikuwa na vitanda viwili; cha kwanza alilala mtoto, cha pili akalala Jamaa. Usiku wa manane Jamaa akiwa katika usingizi mzito akastuka kuona ameshaharibu kwa kujikojolea. Jamaa akaona huu msala cha kufanya nimuhamishe mtoto kwenye kitanda changu, mimi nihamie kwenye kitanda chake. Wakati Jamaa akimuhamisha mtoto hakujua kama mtoto ameshaharibu kwa kujinyea kwenye kitanda chake. Kulipokucha wenyeji wake wakashangaa kuona mgeni wao nguo zake zina mavi wakajua kajinyea!

Tehe tehe kilichotokea nasikia Jamaa alipitia mlango wa nyuma kuepuka aibu akaondoka bila kuaga!
 
Last edited:

Similar Discussions

Back
Top Bottom