karibuni umalengani..

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,006
1,254
Vuvi lambwa vuvi nyika, jivuvi la madimbwini,
likawaza kadhalika, lingevua baharini,
Na sasa lafadhaika, chambo hakina thamani,
Samaki amezichambo, au twambe hakioni?

Karibuni katika uchambuzi.
 
Samaki amezichambo,kasahau kuna papa,
hula hata kilimbo,japo si wake kikwapa,
vuvi lambwa vuvi rembo,ndoano sio mshipa,
Tembelea kimwaloni,ujue neno jivuni,
 
Vuvi lambwa vuvi nyika, jivuvi la madimbwini,
likawaza kadhalika, lingevua baharini,
Na sasa lafadhaika, chambo hakina thamani,
Samaki amezichambo, au twambe hakioni?

Karibuni katika uchambuzi.

Ela uvuvi wa juya, kuvua siutamani
Sababuye 'takwambiya, ufahamiwe mwendani
Ni kwambakwe huingiya, samaki waso thamani
Jabali hulijilisi, jishipi ukilitupa

Na nivuapo maziyo, mavuvi ya kizamani
Kwa hino hali niliyo, huvua kwa kutamani
Hatafuta kiteweyo, cha wali mwema kombeni
Mshipi ukishimeli, samaki hutapatapa
 
Kisache vuvi juha, mbinuze zilidoda
Chamboche kikaoza shomboye 'kuijua!
Pweza wala kibua kikashindwa kupumbaza
Weledi waliukwaa kuzikabili mbinuze

Kabadili zake mbinu, kaibuka na baruti
Kama vile haitoshi, sumu sumu katumia
Samaki kuwaulia, sumu kawatia pia
Kwa ujuha alonao akadhani ameshinda

Ufukweni kaondoka akicheka kama zuzu
Akidhani umevuna pasi jasho kukuvuja
Samakize kajilia kufurahia mavuno
Siraeli 'kukawia, kajifia kwa sumuye.
 
Back
Top Bottom