Karibu uwekeze kwenye biashara ya magari used

Knowledge ya magari na opportunities kila mtu anaziona, Hakuna dalali atakayekulengesha gari kwa bei rahisi, haipo hiyo.

Kwa kifupi, kwenye biashara ya kununua na kuuza magari kila kitu ni marudio, hakuna fursa, wanao survive ni wenye capital kubwa.

Kwanza hakikisha hujizamishi kwa dalali wewe cheza na wapambanaji ukague gari kwa mmiliki ukiielewa na ukapiga hesabu vizuri ukiona inakulipa wewe lipuka nayo tu
 
Knowledge ya magari na opportunities kila mtu anaziona, Hakuna dalali atakayekulengesha gari kwa bei rahisi, haipo hiyo.

Kwa kifupi, kwenye biashara ya kununua na kuuza magari kila kitu ni marudio, hakuna fursa, wanao survive ni wenye capital kubwa.
hakuna mtu anayefanya biashara bila faida ndo maana nikasema ambaye yupo tayari kuwekeza mimi ndie nitayetafuta gari na mie ndie nitakayeliuza gari sababu ndio kazi yangu,lakini kwenye faida itabidi unipe 30% na hiyo 70% ni yako kama mmiliki
 
Biashara yoyote mtaji ni nguvu yako tahadhari kubwa uielewe biashara yenyewe na uipende lakini uifanye kwa uaminifu na ukikua kimtaji unaweza kwenda kulenga gari bei chee hadi zambia, malawi maana huko hua wanajiuzia magari bei chee tu, kikubwa tahadhari na umakini mkubwa unaelenga ist hauwezi kulingana na anaelenga greda au skaveta,
Na wewe ni mmoja wa wanachama wa Jerry empire,?!
 
Inavyoonekana inalipa, kuna baadhi ya watu wakimaliza kazi za Kuajiriwa unakuta Jioni anapiga zake Uber/Bolt kuongeza kipato.

Kuna jamaa nilikutana naye Mwanza, anafanya hizo mambo. Anasema akianza saa 11 jioni hadi saa 5 usiku alikuwa anaingiza elfu 40 ukitoa gharama za mafuta.

Ndio kikubwa usiwe mvivu tu maisha haya ukikaza kwa nia na malengo kutoboa ni suala la kawaida kabisa kikubwa fanya tafiti za kina kwa kitu unacholenga kufanya
 
Hivi ubber kama unafanya mwenyewe inalipa
zamani ilikuwa inalipa ila kwa sasa labda kama unataka hela ya mafuta na service na kula tu,sababu ukipiga kazi sana inakubidi kila week upige service ndogo na mwisho wa mwezi service kubwa hivyo unachobaki nacho kinakuwa kiduchu sana unaichosha gari.

Japo wale walioanza zamani wanakuwa na wateja wao parmanent mfano kupeleka watoto shule na kuwarudisha au wafanyakaz flani so akiunga na uber anaambulia otherwise ni kazi pasua kichwa na ukifanya kufa kupona ndivyo unavyoua gari
 
Watu wanalenga hadi bodaboda kwanza anajua kwa Dar boxer bei chee lakini akiifikisha bukoba ni hela, anajua kigoma na katavi wanataka pikipiki gani analenga hizo hizo, vibali anatia kwenye malori anazama hukohuko mikoani akishuka siku tatu au nne karudi na pesa yake nzuri
 
Na wewe ni mmoja wa wanachama wa Jerry empire,?!

Hapana, nilifanya hizo mishe miaka ya 2009, wale ulikua unasikia papa musofe, ndama mutoto ya ng’ombe hao ndio enzi hiyo akiuza ndinga kadhaa faida ipo anaenda kutuza watu wa bendi basi watu wanapagawa kwa siku hizi biashara imekua rahisi, kuna hadi broadcasting bana
 
zamani ilikuwa inalipa ila kwa sasa labda kama unataka hela ya mafuta na service na kula tu,sababu ukipiga kazi sana inakubidi kila week upige service ndogo na mwisho wa mwezi service kubwa hivyo unachobaki nacho kinakuwa kiduchu sana unaichosha gari.

Japo wale walioanza zamani wanakuwa na wateja wao parmanent mfano kupeleka watoto shule na kuwarudisha au wafanyakaz flani so akiunga na uber anaambulia otherwise ni kazi pasua kichwa na ukifanya kufa kupona ndivyo unavyoua gari
Umesema una uzoefu. Ni uzoefu wa muda gani? Huo muda wote uliofanya hii kazi hujapata mtaji hasa ikizingatiwa kuwa umesema ina faida nzuri sana? Huoni kuwa kuliko mtu ku-risk kununua magari mabovu ni bora awe anaagiza kutoka eg Japan hata mawili mawili na kuuza baada ya kulipia ushuru na kusajili?
 
Mkuu kuagiza japan utachelewa kupata pesa, hivi unajua hata wenye yard wanalenga magari na ni biashara yao kubwa? Jerryempire nilichoona ngefanya atoe tu uzoefu wake hiyo ya umkabidhi pesa mara mgawane asilimia ya faida kwa upande wangu haijakaa sawa kabisa
 
nna uzoefu wa miaka 5 kwenye hii biashara na nlikuwa naifanya hku nafnya biashara nyingne,pia kuna mambo yalitokea nika shake but ni business ya risk free.

kumbuka pia nmetoa starting capital ya kupata gari nzuri zisizo na changamoto na pia sijamwambia mtu anipe hela yake bali namtafutia gari ambayo mimi na yeye ote tutairidhia kutokana na uzoefu wangu na wake kwenye biashara
 
Nimekuelewa ila nilikuwa naulizia ili kujua zaidi. Kwa namna uliyoelezea kama kuna mtu yuko interested anaweza kujaribu na sidhani kama anaweza kutapeliwa.
 
Habari
Kwa majina naitwa Jerry na ninajihusisha na uuzaji wa magari used nikiwa kama dalali kwa muda mrefu ndani ya Dar es Salaam.

Leo ningependa kushare nanyi kuhusu biashara hii ya magari hasa used hapa Dar es Salaam, biashara ambayo ina faida kubwa ambayo wengi sana bado hawajaijua.

BIASHARA HII INAFANYIKAJE?

Biashara hii hufanyika kwa mtu(mfanyabiashara) kutafuta gari na gari hizi mara nyingi hupatikana kwa watu wenye shida, bima na taasisi za mikopo na bank.

Kwa mfano gari aina ya ist inaweza kuwa na changamoto ndogo mathalani ya shilingi 300k mpaka muda mwingine 1m na gari hiyo husika inauzwa na mmiliki kwa gharama za shilingi 6m, wakati thamani husika ya hiyo gari sokoni ni 11 au 10m ukitoa ile 7m unabakia na kama 4m au 3m ikiwa kama faida ya gari husika.

Mara baada ya mfanyabiashara kuipata gari husika, gari ambazo huitwa za kulengwa kwa jina maarufu, then huchukua gari hiyo na kuiweka sokoni kwa bei ya faida, mara baada ya kuiuza hutafuta nyingine na kazi huwa inafanyika hivyo.

JE KAZI HII INACHAGUA JINSIA?

Jibu ni hapana kazi hii inaweza kufanywa na mtu yoyote au mwanaume au hata mwanamke.Na ni biashara ambayo haitumii mda mrefu sana ni kitendo cha kukubaliana bei na mteja na biashara kufanyika.

GARI HUPATIKANA VIPI.

Kama nilivyosema hapo awali kuwa gari hizi za kulenga huwa zinapatikana kupitia watu wenye shida ya hela,taasisi za kifedha za mikopo,bima n.k,ili kuzipata gari hizo za kulenga unaweza kuzipata kupitia madalali wa kulengesha ambao huwa na connection na wamiliki wa gari husika.

MAMBO YA KUZINGATIA UNUNUAPO GARI,

Kama zilivyo biashara nyingine hii pia ni biashara yenye kuhitaji umakini na uzoefu hasa kwenye kuchagua gari nzuri ili upate kuiuza vizuri vile vile,bila kusahau kupiga hesabu sahihi endapo kama gari husika itahitaji matengenezo kwa kuwa na uzoefu wa spear husika .

KARIBU UWEKEZE KWENYE BIASHARA HII NAMI.

Nakukaribisha uje kuwekeza kwenye biashara hii kwa kutafuta gari na kuuza pamoja nami, Nitakusaidia kutafuta gari nzuri ambayo kupitia mimi nitatafuta wateja na kuiuza kwa faida nzuri.

Kinachofanyika baada ya kupatikana gari unaweza kuitumia gari husika/kubaki nayo ukiwa unaitimia wewe mwenyewe au unaweza kuiacha ofisini kwetu hadi pale mteja atakapotokea wakati huo ntakuwa naitangaza ukiaachilia mbali kuwatumia madalali ote wa magari ili nao waiuze,wakati huo documents zote ukiwa nazo mwenyewe mteja akifika unakuja nazo au tunakufata tunamaliza biashara.

Biashara hii haihitaji usimamizi wako labda kama utaamua mwenyewe sababu kuanzia kutafuta gari mpaka kuliuza mie ndo ntakayekuwa na pambana kwa maana hyo unaweza kuendelea kufanya kazi zako nyingine huku ukiendelea kufanya biashara hii ya magari.

Endapo kama utakuwa interested karibu tufanye biashara hii pamoja mie nipo magomeni na ni mzoefu wa hii biashara,endapo utakuwa tayari nakukaribisha japo katika faida ya kila gari ntakuwa nachukua faida ya 30%

Nikiwa na maana kam utabakia na documents na gari kunikabidhi basi gari hyo itabakia ofisini kwetu ambako tuna chama kabisa,ambako gjarama za parking na ulinzi wa gari zitakuwa juu yangu pamoja na hela ya mafuta ambayo wateja watakuwa wanakagulia itakuwa juu yangu pia,lakini gari ikishauzika mie ntakuwa nachukua 30% ya faida ile ambayo tutakuwa tumekubaliana,na ile 70% utabakia nayo wewe kama mmiliki,Karibu uwekeze kwenye hii biashara ambayo haina gharama nyingine yoyote na wala haikatwi kodi lakini yenye faida nzuri.

kwa mwenye kuhitaji anakaribishwa 0659756647 na mwenye maoni au kuhitaji ufafanuzi anaweza nitafuta au kuuliza hata hapa hapa
ahsanteni
Ukiona mchongo kwa Tanzania unatangazwa hadharani badi huo sio wa kukimbilia.
 
Mkuu kuagiza japan utachelewa kupata pesa, hivi unajua hata wenye yard wanalenga magari na ni biashara yao kubwa? Jerryempire nilichoona ngefanya atoe tu uzoefu wake hiyo ya umkabidhi pesa mara mgawane asilimia ya faida kwa upande wangu haijakaa sawa kabisa
umeniquote vibaya mkuu nilichomaanisha ni kwamba kama mtu yupo willing kufanya hii biashara na anamtaj wa kuanzia 8m au 10m anitafute.

Then ntamsaidia kupata gari nzuri ya kulenga kwa bei hyo ili baadae nitafute wateja tuiuze lakini nikishaiuza mimi faida yangu ni 30% ya faida hyo 70% ya kwake.

na hapo anaweza akaniachia gari abaki na documents gari iwe ofisini mteja aikagulie ofisini kwetu kama mmiliki atakuwa ni mfanyakazi au kama atataka anaweza kukaa na gari yake huku mie naipambania akipatikana mteja tunamfatavau anaitwa tunafanya biashara
 
Nimekuelewa ila nilikuwa naulizia ili kujua zaidi. Kwa namna uliyoelezea kama kuna mtu yuko interested anaweza kujaribu na sidhani kama anaweza kutapeliwa.
kutapeliwa ni ngumu sababu gari ni documents na documents zote unakuwa nazo wewe mmiliki mimi kazi yangu ni kukupa gari na kuhakikisha gari nnaiuza kwa wakati ili tununue nyingine
 
Back
Top Bottom